Kila mtoto chini ya miaka 18 kusafirishwa kutoka eneo moja kwenda jingine kwa kibali cha mzazi na cha Serikali ya mtaa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,520
9,322
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama nchini, kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 18, anayesafirishwa kutoka eneo moja kwenda jingine anakuwa na kibali cha mzazi na kile cha kiongozi wa serikali za mitaa.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu yaliyohusisha wadau mbalimbali ambapo biashara hiyohufanyika mataifa mbalimbali duniani.

Amebainisha kuwa Wizara itajikita kusimamia safari za ndani ya nchi kwa lengo la kubaini wanaojihusisha na vitendo hivyo ambapo amebainisha kuwa waathirika wakubwa ni wanawake na watoto vitendo ambavyop hutokana sababu mbalimbali ikiwemo tamaa ya pesa na kuibuka kwa soko la vitendovya ngono.

Akizungumzia Watanzania wanaotaka kufanya kazi nje ya nchi amewata kufuata sheria na taratibu zilizowekwa badala ya kuzamia kwa kutumia njia haramu kwa kigezo cha kutafuta maisha akisisitiza kujiridhisha kuhusu kazi husika kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wabinadamu, Amatus Magere katika amesema mapambano hayo wanakabiliwa na changamoto nyingi kwani hufanywa na binadamu wenyewe kwa siri kubwa, kukosekana kwa mfuko wa kusaidia waathirika na upungufu wa raslimali watu.
 
Ni wazo zuri sana hata kwa usalama wa nchi. Waangalie namna bora na rahisi sana ya kupata hivyo vibali.
 
Haitekelezeki na itahatarisha ustawi wa jamii kwa ujumla. Ni kama kuiongezea thamani bidhaa adimu, wenye kutoa hivyo vibali tayari mate yanawatoka, na hao wenye shughuli zao hizo za sijui kusafirisha au kuiba hao watoto nao ulaji utakuwa mzuri.

Kuna wakati nilikuwa nawaza, huyu mtoto wa miaka 13 amefeli darasa la saba, wazazi huko kijijini hawawezi kumpeleka shule binafsi, na hata wanaofaulu pia huwa kuna wazazi wanashindwa zile gharama ziambatanazo na mtoto kusoma.

Mzazi anaamua ni bora wawe wanalima na mwanaye kwaajili ya kupata chochote kitu, hapa mzazi hamtumikishi mtoto?

Au mtoto anafanya viajira, malipo yake analipia gharama za shule, huyu naye vipi? Ajira za utotoni hazimhusu?
 
Kule Kigoma hii biashara haramu imeshika hatamu.

Watoto wa kiha (7-16yrs) waliopaswa kuwa shule utawakuta usukumani wanachunga mifugo kwa mamia ilhali wale watoto wa kisukuma wa rika hilo wakienda shule.

Serikali isipolitilia maanani hili jambo litaleta shida siku za usoni.

Kauli kama,"Waislamu tulibaguliwa kupata elimu au watu wa Kigoma tulitengwa kwenye elimu". zinatengenezwa namna hii.

Kuna mawakala wanatoa watoto wa kiume Kigoma kwa ridhaa ya wazazi wao kuwapeleka Shinyanga na Tabora na wengine ni warundi wanatoroshwa kambini kwenda kuchunga usukumani.

Rai: Doria ifanyike Shy&Tbr ili hao watoto (7-18) warudi kwao wakasome.
 
Kule Kigoma hii biashara haramu imeshika hatamu.

Watoto wa kiha (7-16yrs) waliopaswa kuwa shule utawakuta usukumani wanachunga mifugo kwa mamia ilhali wale watoto wa kisukuma wa rika hilo wakienda shule.

Serikali isipolitilia maanani hili jambo litaleta shida siku za usoni.

Kauli kama,"Waislamu tulibaguliwa kupata elimu au watu wa Kigoma tulitengwa kwenye elimu". zinatengenezwa namna hii.

Kuna mawakala wanatoa watoto wa kiume Kigoma kwa ridhaa ya wazazi wao kuwapeleka Shinyanga na Tabora na wengine ni warundi wanatoroshwa kambini kwenda kuchunga usukumani.

Rai: Doria ifanyike Shy&Tbr ili hao watoto (7-18) warudi kwao wakasome.
Hata hapa dar watoto wa kigoma chini ya umri wa 18 wapo wanuza mayai wamepangishiwa mageto wamejanzwa kama kuku ni kutwa nzima kutembea juani wakiuza mayai.
 
Nafikiri wew hujamuelewa vizurimie nimemuelewa alisema maa ana maanisha kwamba , ikiwa mtoto anasafiri yeye mwenyewe bila uwepo wa mtu mzima ndio itahitaji kibali cha mzazi na serikali za mtaaa. Vinginevyo hayo ni mawazo yako tuu na huo mfumo ulikuwepo sana miaka ya nyuma sema kwa kipindi cha sasa cha dot. Con mambo yalirahisishwa sana.
 
Hii utekelezaji wake mgumu. Kwa hiyo na vijana wa kwenda form five na vyuo tuwe tunawakati kibali cha kusafiri na kuwasindikiza au mimi sielewi?
 
Kodi nyingine tena hii
Maana hii sirikali yawanyonge haiwezi kukupa kibali bila malipo


True kwa Tanzania watafanya ni biashara, ninachofahamu pale airport international departure ukipita na mtoto sio wako watakuuliza conset( kiapo) cha mzazi wake

alikadhalika na nchi unayoenda ukifika they will also ask the same kuthitibitisha huyo mtoto ni wa kwako kama sio wako wazazi wake wamekuluusu? Kiapo kiambatane na kitambulisho cha mzazi
 
Ni wazo zuri sana hata kwa usalama wa nchi. Waangalie namna bora na rahisi sana ya kupata hivyo vibali.
Ofisi ya serikali ya mtaa hupati barua bila pesa si chini ya TShs. 3,000 hadi 5,000. Waziri kawapelekea ulaji hawa jamaa
 
Back
Top Bottom