Kila Mtanzania Mwenye chembe ya Mafanikio, naoombe dua hii

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,188
7,490
Sema!
"Ewe Mwenyezi Mungu , naomba unikinge na Shari ya Hasidi anapo Husudu!" Fanya hivyo asubuhi, mchana na jioni bila kuchoka. Hali sio nzuri wakuu. Baadhi yetu wamekuwa hawapendi kabisa kuona mtu aliyewazidi mafanikio, basi watakuandama hadi wahakikishe unakwama, unafilisika, unadhalilika, unakosa raha au jambo lolote baya linakufika. Sijui ni roho gani imetuingia ila ambalo nina uhakika nalo ni kwamba husuda imekuwa husuda na hali si nzuri hata kidogo. Leo kwa ndugu yako kesho zamu yako. Unakuta mtu mzima na akili timamu anajichelelesha huku anasema " eeh kweli, nimefurahi sana, ni bora na fulani amefilisika/afilisike ili tuwe sawa". Yaani inahuzunisha sana. Sadism "Unoko" umazidi siku hadi siku.

Ndugu zangu, huu ni muda wa kufanya dua na kila aina ya maombi kuliko kipindi kingine kwa yule anayefikiri kuwa inafaa.
 
Sadism ni unokoko wakuu, kokote unaposikia neno sadism ujue linamaana ya unoko! Tufanyeni sana dua ndugu zangu, kwa siri na kwa dhahiri, kwa makundi na mtu mmoja mmoja. Kila mtu kwa dhati na kwa yakini yake mwenyewe. Tumeingiliwa na jitu la ajabu ndani ya akili, fikra, mioyo na hisia zetu wakuu! huu si muda wakuchekacheka wakuu kwa mtu wenye akili timamu ni muda wa kuwa mtulivu sana.Ile roho ya ubinadamu sijui inmeenda wapi? si sisi ndio tulikuwa tunasifika kwa ukarimu, upendo na utu? imekuwaje tunapenda kuona mwanadamu mwenzetu akidhalilika kuliko akifanikiwa au akifurahi?
 
Watu wengi hawapendi uwapite kimaendeleo.

Wakikuona umefanikiwa roho zinawauma cha ajabu utakuta una msaada mkubwa kwao.
 
Watu wengi hawapendi uwapite kimaendeleo.

Wakikuona umefanikiwa roho zinawauma cha ajabu utakuta una msaada mkubwa kwao.
ila hii ni kwa watanzania tu, mbona wenzetu wakiona mwenzao kafanikiwa wanampongeza na kumuomba afundishe kuwa kafanya je, ili nao wafanikiwe? yaani sijui watanzania tumekuwaje aisee! yaani wewe fuatilia nyuzi tu zinazohusu watu wenye mafanikio kwenye masuala mbali mbali wakipata matatizo watanzania tunavyofurahi na kushangilia. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom