Kila Mtanzania Anahitaji Upinzani Imara

BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
May 5, 2013
781
1,000
Wakuu Habari za jumapili

Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu kubwa la wanachama maarufu, na viongozi wa vyama vya Upinzani kuhamia chama tawala, yani CCM.

Uhamaji wa viongozi pia umekuwa ukitafsiriwa kama, sio Uhamaji bali ni ukwapuaji wa viongozi wa Upinzani, jambo ambalo linaonekana kama njia ya kuudhoofisha Upinzani. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wanashangilia kwamba Upinzani unaenda kufa. NIANZE KWA KUSEMA HII SIO HABARI NZURI KWA MTU YOYOTE.

Dhana ya umuhimu wa uwepo wa Upinzani kwanza inajikita kwenye UWEPO WA NJIA MBADALA. Mimi ninaamini kila binadamu anapenda kuwa na mbadala, kwamba njia moja inaposhindikana basi awe na wigo wa kutumia njia nyingine. Hii dhana ni maarufu sana kwa jina la PLAN B.

Embu imagine, hapo unapoishi kungekuwa na duka moja tu la bidhaa za chakula, bila kununua hapo ni kulala na njaa hatimae kufa, ni mateso gani ambayo ungeyapata. Mwenye duka angekuuzia unga wa ugali, mchele, sukari n.k kwa bei anayotaka kwa muda anaotaka au pengine anaweza amua asikuuzie kabisa kwasababu anayoijua yeye. HII NI SABABU YA KUKOSA MBADALA. Haya mazingira ndio yatakayojitokeza kama hakuna vyama vya Upinzani vyenye nguvu.

Je nani asiyefahamu kuna wakati JPM alihitaji vyama vya Upinzani imara. Nani asiyejua kwamba yeye alipata nafasi alionayo kutokana na mivutano ndani ya chama? Nani asiyejua hiyo mivutano ililetwa na makundi ndani chama yaliyokuwa influenced na msukumo wa wapinzani nje ya chama? Nani asiyefahamu kwamba CCM waliona JPM ni mtu sahihi kutokana na aina za siasa zilizokuwa zinaendeshwa wakati huo na wapinzani, Ufisadi, Uhitaji wa mtu wa Maamuzi magumu na mabadiliko.

Pia hata Lowasa alihitaji Upinzani imara, kwani mpaka leo ninaamini Upinzani imara ndio uliompa kiburi kwenda kugombea urais kupitia Upinzani, vinginevyo bila Upinzani imara nina uhakika angebaki CCM akiwa na hasira lakini asingejua la kufanya. Nakuhakikishia Upinzani ungekuwa dhaifu kama wa PPT Maendeleo au CHAUMA Lowasa asingehama. Hii pia ni kweli kwa Sumae na wengine wote waliohama, walihitaji Upinzani imara ili wawe na guts za kuhama.

Akina Nape, akina Bashe, akina Mwakyembe, akina Sita (RIP) na wengine wengi wote kuna Nyakati walihitaji/wanahitaji Upinzani imara. Vijana wa propaganda mitandaoni wa CCM mnahitaji Upinzani imara kwani, Upinzani ukiwa dhaifu, CCM haitahitaji tena huduma zenu.

Pia watumishi wa uma, wafanya biashara, Wakulima wote wanahitaji Upinzani imara. Upinzani ukifa, ama ukiwa dhaifu serikali haitakuwa na hofu tena katika kushughulikia matatizo yenu, sababu hata serikali ikiwatelekeza mtakimbilia wapi.

Dhana ya umuhimu wa Uwepo wa Upinzani imara pili inajikita kwenye KUEPUKA KUWA NA MTU/KITU KIMOJA CHENYE NGUVU NA KUSHINDWA KUKIDHIBITI.

Kwa wanahistoria, mtafahamu vizuri dhana ya BALANCE OF POWER. Mfano China hapendi mambo mengi ambayo Korea Kaskazini anayofanya lakini hawezi hata siku moja kuunga mkono Marekani kushambulia Korea ya Kaskazini. Kwanini, sababu anaogopa Korea ya Kaskazini (ambaye kiitikadi wanaendana na China) akishadhibitiwa, kwenye eneo la Mashariki ya mbali China atabaki mkiwa akiwa amezungukwa na Japan, Korea ya Kusini (ambao kiitikadi wapo pamoja na Marekani). Mifano ipo mingi ila naomba niishie hapo.

Kwa Tanzania pia tunahitaji balance of power ya vyama vya siasa, ni hatari sana chama kimoja kuwa na nguvu kubwa ambayo hamna namna ya kuidhibiti. Hata wanaume wengi (pengine hata wanawake) wamekuwa wakiitumia hii mbinu ili kudhibiti mwenza wake kuwa na nguvu juu yake isiyodhibitika. Mbinu hiyo ni maarufu kwa jina la MCHEPUKO.

Mwisho nimalizie kwa kusema hivi, hata hawa wapinzani wanaohama sasa hivi na kupokelewa kwa mbwembwe nyingi ni sababu wanatoka Upinzani imara. Sijawahi sikia wanachama wa UDP, JAHAZI ASILIA ama CCK wamehamia CCM. Sio kwasababu hawahami la hasha, ila kwasababu vyama vyao dhaifu ndio maana hata kusikia hatujawahi.

Tafakuri njema.
 
Drop

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
570
500
WANAO HAMIA CCM NI WATU JASIRI NA WALIO JUFUNZA MENGI KUHUSU UPINZANI
Hakuna upinzani Tanzania hao wanao odoka huko kunako itwa upinzani ni watu weredi wasio na hofu watu watasema nini juu yao ni watu serious walio kuwa tayari kupigania haki na kuleta demokrasia ya kweli. Baada ya kufika huko kunako itwa Upinzani wakagundua wamepotea njia wakakutana na viongozi mafisadi kupitiliza wasio ambilika mambo ya chama yana jadiriwa nyumbani kwa mwenyekiti dio yanapelekwa kupitishwa kwenye vikao. vta chama kazi kubwa ya viongozi wa upinzani ni kula ruzuku za vyama kugawa madaraka kwa familia zao kugawa viti maalum kwa vimada vyao kuuza vyama kwa walio na fedha mafisadi ambao ndio walio wakimbia huko sasa ndio walio nunua vyama vya upinzani nakupewa unyapala wa vyama na viongozi wa upinzani wanawaita mashujaa ndio wanakuwa wamiliki wa vyama vya upinzani. Viongozi wa upinzani pasipo na soni wanawashangilia mabeberu na wezi wa mali ya uma wenyeviti wa vyama wanateua viongozi wanao wataka wapo tayari kuua demokrasia kwa sababu ya umimi kama ilivyotokea kwa Sosopi huko kanda ya Nyasa mwenyekiti mbowe kamweka msigwa bila mshindani na kumtoa mgombea Sosopi. vyama vya jinsi hiyo ni makampuni binafsi na sio vyama vya siasa nawapongeza sana waliojitambua vyama serious vitakuja lakini hivi vilivyopo vipo kuzuia demokrasia ya kweli kujifanya ni upinzani Mbowe amekuwa Mgabe wa Tanzania toka alipowekwa na mkwe kuwa mwenyekiti inakaribia miaka ishirini bado mwenyekiti na hakuna dalili za kutoka hapo kuna upinzani kweli? Maoni yangu acha upinzani uchwara ufe tupate upinzani unao mwogopa Mungu. Endeleeni kutoka huko kwenye sacos ukipotea njia unarudi.
 
Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
3,671
2,000
Hakuna upinzani imara sasa...anza wewe anzisha chama....upinzani sio mbuzi ni watu kama wewe...ila wameshindwa tangu aondoke dr Slaa...nakushauri wewe ndo uanzishe chama
 
BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
May 5, 2013
781
1,000
Hakuna upinzani imara sasa...anza wewe anzisha chama....upinzani sio mbuzi ni watu kama wewe...ila wameshindwa tangu aondoke dr Slaa...nakushauri wewe ndo uanzishe chama
Comment yako inaonesha umeelewa mada. Asante.
 
BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
May 5, 2013
781
1,000
WANAO HAMIA CCM NI WATU JASIRI NA WALIO JUFUNZA MENGI KUHUSU UPINZANI
Hakuna upinzani Tanzania hao wanao odoka huko kunako itwa upinzani ni watu weredi wasio na hofu watu watasema nini juu yao ni watu serious walio kuwa tayari kupigania haki na kuleta demokrasia ya kweli. Baada ya kufika huko kunako itwa Upinzani wakagundua wamepotea njia wakakutana na viongozi mafisadi kupitiliza wasio ambilika mambo ya chama yana jadiriwa nyumbani kwa mwenyekiti dio yanapelekwa kupitishwa kwenye vikao. vta chama kazi kubwa ya viongozi wa upinzani ni kula ruzuku za vyama kugawa madaraka kwa familia zao kugawa viti maalum kwa vimada vyao kuuza vyama kwa walio na fedha mafisadi ambao ndio walio wakimbia huko sasa ndio walio nunua vyama vya upinzani nakupewa unyapala wa vyama na viongozi wa upinzani wanawaita mashujaa ndio wanakuwa wamiliki wa vyama vya upinzani. Viongozi wa upinzani pasipo na soni wanawashangilia mabeberu na wezi wa mali ya uma wenyeviti wa vyama wanateua viongozi wanao wataka wapo tayari kuua demokrasia kwa sababu ya umimi kama ilivyotokea kwa Sosopi huko kanda ya Nyasa mwenyekiti mbowe kamweka msigwa bila mshindani na kumtoa mgombea Sosopi. vyama vya jinsi hiyo ni makampuni binafsi na sio vyama vya siasa nawapongeza sana waliojitambua vyama serious vitakuja lakini hivi vilivyopo vipo kuzuia demokrasia ya kweli kujifanya ni upinzani Mbowe amekuwa Mgabe wa Tanzania toka alipowekwa na mkwe kuwa mwenyekiti inakaribia miaka ishirini bado mwenyekiti na hakuna dalili za kutoka hapo kuna upinzani kweli? Maoni yangu acha upinzani uchwara ufe tupate upinzani unao mwogopa Mungu. Endeleeni kutoka huko kwenye sacos ukipotea njia unarudi.
Mkuu ungeandika kwa para basi maana dah, nimepata shida sana kusoma Andiko lako.

Embu tuangalie hoja zako, unasema huko Upinzani kuna mafisadi(watuhumiwa) kwa sasa, je huko CCM hawapo? Na je hao waliotoka CCM kwenda Upinzani walifukuzwa kwa kosa la ufisadi, kisha Wakahamia Upinzani au Waliondoka kwa hiari yao na wengine wakiwa tayari kuachia nafasi zao nyeti ndani ya chama?

Hoja ya pili ni kupeana vyeo. Je hizi tuhuma CCM hazipo? Viongozi kuwapa vyeo mahawara, je hizi tuhuma CCM hazipo?

Nitajie sababu kwani watu watoke Upinzani waende tawala, ambayo pengine inatajwa Upinzani lakini haiitajwi CCM.

Kuhusu swala la Rushwa, unazungumziaje swala la Mnyeti kupandishwa cheo mara baada ya kugundulika anatumia Rushwa kushawishi viongozi kutoka Upinzani wahamie CCM?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom