Kila Mtanzania anadaiwa milioni 137

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
52,369
24,090
Upinzani:Kila Mtanzania anadaiwa milioni 137

Na Joseph Lugendo, Dodoma

KAMBI ya upinzani bungeni, imeibua madai ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali yaliyosabisha kupotea kwa asilimia 30 ya fedha za bajeti sawa na sh. trilioni 1.098 zinazodaiwa kufujwa na kada ya viongozi serikalini mwaka 2006/2007 huku ikidai kuwa kwa sasa, kitakwimu, madeni ya Serikali yanamfanya kila raia wa nchi hii kudaiwa takribani sh. milioni 137/-.

Madai hayo yapo katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Upinzani bungeni, Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohammed (CUF), kuhusu bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi, iliyosomwa bungeni juzi na Mbunge wa Viti Maalum,Bi. Fatma Fereji (CUF).

Katika hotuba hiyo, iliyokusanya tathimini ya taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) ya mwaka 2006/2007, kambi hiyo pia ilihoji matumizi ya sh. milioni 551 zilizotumika kununulia picha zenye sura ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Dkt. Daud Balali kwa ajili ya kuwekwa kwenye majengo pacha ya benki hiyo.

Aidha, kambi hiyo ilipendekeza kuundwa kwa tume maalumu itakayofanyia tathimini ya majengo hayo na kuhoji sababu za serikali kupuuza ushauri wa kufanyia tathimini majengo hayo

Pia ilielezea kuwa ungezeko la deni la Taifa la nje na ndani linasababisha kila Mtazania popote alipo sasa kudaiwa jumla ya sh. 136,875.05/- wakati ambao kwa mujibu wa kambi hiyo mpaka kufikia Juni 2008, serikali imejikuta ikipoteza mapato yaliyofikia sh. bilioni 819, kwa kutoa misamaha ya kodi.

Walitoa mfano wa msamaa wa kodi ya mafuta yanayoingizwa ndani ya nchi na makampuni ya uchimbaji madini ambapo kuanzia 2004 mpaka 2006, makampuni sita ya migodi ya dhahabu yaliingiza lita milioni 178 za mafuta ghafi na kupotezea serikali sh. bilioni 62. 8 kutokana na kusamehewa kodi.

Pia walilalamikia ukwepaji wa kodi ya mapato (PAYE) unaofanywa na wafanyakazi wa kigeni wanaokadiriwa kufikia 500 katika makampuni mbalimbali ambao wanalipwa kati ya sh. milioni 5 na 20 huku wakikwepa kodi hiyo.

Kwa mujibu wa hesabu ya kamvi hiyo kodi ya mapato kutoka kwa wafayakazi hao ingeweza kuipatia serikali sh. bilioni 1.5 kwa mwezi sawa na sh. bilioni 18 kwa mwaka.

Mjadala wa bajeti ya wizara hiyo ulioanza juzi, unatarajiwa kuendelea kesho kwa wabunge kuchangia zaidi.

Kichanga afa katika mazingira tata-ANCHOR
 
Tunaomba ufafanuzi zaidi Visenti hivi vya Selikari ni pamoja na visenti vinavyotumika kwenye Ziara za kikazi za Rais nje ya nchi?
 
Huo mzigo inabidi wabebeshwe mafisadi waliojivisha ngozi ya uongozi ambao wanailundikia nchi yetu madeni kila kukicha yasiyo na manufaa yoyote kwa nchi yetu wakati wenyewe wakifanya ufisadi na kuwa matajiri wa kupindukia na kuishi maisha ya hali ya juu kama ya wacheza sinema wa Hollywood.
 
Upinzani:Kila Mtanzania anadaiwa milioni 137

Na Joseph Lugendo, Dodoma

KAMBI ya upinzani bungeni, imeibua madai ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali yaliyosabisha kupotea kwa asilimia 30 ya fedha za bajeti sawa na sh. trilioni 1.098 zinazodaiwa kufujwa na kada ya viongozi serikalini mwaka 2006/2007 huku ikidai kuwa kwa sasa, kitakwimu, madeni ya Serikali yanamfanya kila raia wa nchi hii kudaiwa takribani sh. milioni 137/-.

Nimependa walivyotumia huo mfano ili tuelewe vizuri hizi figures. Hata hivyo, nikizidisha 137 mil. X 40 mil. napata 5480 Trillion.
Pia walilalamikia ukwepaji wa kodi ya mapato (PAYE) unaofanywa na wafanyakazi wa kigeni wanaokadiriwa kufikia 500 katika makampuni mbalimbali ambao wanalipwa kati ya sh. milioni 5 na 20 huku wakikwepa kodi hiyo.

Ndiyo maana Kikwete ametamani sana kumsweka ndani Dr. Slaa na wenzake. Amejikuta akitamka fikra zake hadharani. Uzi ni ule ule wapinzani, mpaka kieleweke!

.
 
Back
Top Bottom