Kila Mpigania nchi hii afuatilie utekelezaji wa ahadi zilizoolewa na JK nazo ni hizi

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
521
234
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
  67. TUJITAHIDI KUFUATILIA AHADI HIZI ILI TUONE KAMA KWELI ZOTE ZINATEKELEZEKA NA TUWEZE KUONA UKWELI WA MAMBO
 
Hivi huyo Triple Doctor ameshaanza kutekeleza chochote kweli? Vinginevo atakuwa nyuma ya wakati.
 
Atatekeleza kama ataamua na kuweka pembeni ufisadi wa watendaji wake. Nothing is impossible, lets wait
 
You never make a promise which you cant keep, and am very sure jk will never keep his promise he is unreliable unless you are in his inner circle
 
Lets look his CV. Ahadi za 2005, zikuwa 52. Alitelekeza 1. Kafungua bank ya wanawake. Bahati mbaya, ... Nani kati yetu anaejua wanawake wanaofaidika na kuwepo kwa bank hii?
 
Shinyanga awamu iliyopita tuliahidiwa kiwanda cha CEMENT akapayuuuuuka weeee lakini saivi kiiiimya.
Tutazidi kuipiga chini Si Si Em:A S 114:
:peep:
 
  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini ( MCHAKATO UMEANZA)
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga (Waziri wa maji ameisha litolea utatuzi)
  3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga (Ulipaji wa Tshs 5bn umeisha fanyika)
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma (Waziri wa Ardhi ameisha lisemea hili)
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini (Serikali inatoa pesa kwenye halmashauri kwa ajili ya PowerTyler)
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma (Serikali inatoa pesa kwenye halmashauri kwa ajili ya PowerTyler)
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera (Mkuu wa mkoa Kagera ameisha sema hawataondolewa)
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera (Bajeti ijayo ya 2011/12, ila upembuzi yakinifu waendelea)
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini (Bajeti ijayo ya 2011/12)
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini (Mh. Magufuli ameisha toa maelekezo kwa watendaji wake)
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera (Mazungumzo yanaendelea)
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera (zoezi linaendelea)
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera (Zoezi linaendelea, sheria imeboreshwa tayari na majengo wanajengewa)
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya (Hati za kifo zipo mezani kwa Rais)
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera (Bajeti ya 2011/12)
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali (Uundwaji wa SACCOs na VICOBA waendelea kwa kasi)
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza (Mafunzo ya kuviimarisha yanaendelea)
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza (Boti za kudhibiti uharamia zimeagizwa tayari)
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita (Tayari Geita ni mkoa)
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba (Muungano unalindwa na kero za muungano zinashughulikiwa)
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro (Serikali kuu yaanza kupeleka pesa Halmashauri)
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini (Bajeti ya 2011/12)
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa (Upembuzi yakinifu umeanza)
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea (Waziri wa Elimu ameisha litolea tamko)
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya (Waziri wa Madini analifuatilizia)
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga (Waziri wa mazingira analifuatilizia)
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa (Mchakato unaendelea)
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro (Mchakato waendelea)
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini (Mchakato waendelea)
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora (Mchakato waendelea)
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu (waalimu wote wanaomaliza kuajiriwa na serikali )
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini (Usambazaji wa vyandarua unaendelea)
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara (Muhimbili hivi sasa imeboreshwa na majengo mengi ya hospitali hizo yanajengwa)
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma (ameisha litolea tamko na waziri ameteuliwa)
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete (sheria ya walemavu kupelekwa bungeni mwaka ujao)
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini (mchakato waendelea)
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha (mchakato waendelea)
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini (mchakato waendelea)
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora (mchakato waendelea)
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini (mchakato waendelea)
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma (mchakato waendelea)
  42. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga (mchakato waendelea kuwabaini wanaostahili kulipwa)
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini (Mchakato waendelea)
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .(SACCOs za wavuvi zaendelea kuundwa)
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido (Mchakato waendelea)
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro (Mchakato waendelea)
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara (Mchakato waendelea)
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini (Waziri wa maji ameisha litolea mkakati)
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa (Fedha zipo ndani ya bajeti ya 2010/11)
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa (Waziri wa maji ameisha litolea mkakati)
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa (Waziri wa ujenzi ameisha litolea mkakati)
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda (Jeshi la polisi laendelea kuimarishwa)
  53. Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara (Mradi wa malaria haikubaliki waendelea vizuri)
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa (Spika wa bunge ni mwanamke)
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar (Waziri wa Muungano analishughulikia)
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar (Waziri wa afya Zanzibar amelitolea tamko)
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti (Linaendelea na tunawasaidia)
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma (Mchakato waendelea)
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma (Mchakato waendelea)
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma (Mchakato waendelea)
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma (Misaada inaendelea kuja toka marekani)
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam (Halijatokea)
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara (Mchakato waendelea)
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha (Mchakato waendelea)
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha (Mchakato waendelea)
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha (Mchakato waendelea)
  67. TUJITAHIDI KUFUATILIA AHADI HIZI ILI TUONE KAMA KWELI ZOTE ZINATEKELEZEKA NA TUWEZE KUONA UKWELI WA MAMBO
Kama uonavyo ahadi nyingine zimeisha tekelezeka na zingine zinaendelea kutekelezwa na zingine zipo kwenye mipango ya kutekelezwa. Kwa mwendo kasi huu, JK anaweza timiza ahadi zake ndani ya miaka 3 tu na zikaisha
 
^^^ @GeniousBrain, i have a very strong feeling that you are very close to Mr. President (ila serikali ya kichwa changu haimtambui)...Or u are in a position to make a potential change we need! Besides the fact that you backed him up very collectively but i admit "oh boy, that's 63 promises" so it may be hard to go into details...but honestly speaking, tell J.M.K that comparing to when he was stepping into office in 2005 ,this year it's only the smallest fraction of Tanzanians are optimistic with his administration! He really should worry about his legacy when he leaves office, just to mention the least significant thing in his mighty long things-to-worry list"
 
^^^ @GeniousBrain, i have a very strong feeling that you are very close to Mr. President (ila serikali ya kichwa changu haimtambui)...Or u are in a position to make a potential change we need! Besides the fact that you backed him up very collectively but i admit "oh boy, that's 63 promises" so it may be hard to go into details...but honestly speaking, tell J.M.K that comparing to when he was stepping into office in 2005 ,this year it's only the smallest fraction of Tanzanians are optimistic with his administration! He really should worry about his legacy when he leaves office, just to mention the least significant thing in his mighty long things-to-worry list"

Tusibiri tu miaka mitano inaweza kwisha kama maji, tutaanza kuulizana tu baadaye
Ukiangalia hizo kauli hapo chini unaona ni usanii tu

Bajeti ijayo...........
Waziri amelisemea...........
Mchakato unaendelea.......
Upembuzi yakinifu unaendelea.......

Nashangaa sana kusikia ahadi kuwa serikali itajenga uwanja wa ndege, sijui kama kweli ni uwanja a ndege au ni kutengeneza runway ya vumbi na kuimwagilia maji.

Kununua meli kubwa, wakati pantoni Kigamboni mpaka leo anajua Mungu lini itakuja.

Maji nchi nzima wakati Dar kwenyewe maji issue kubwa sana.
 
Tusibiri tu miaka mitano inaweza kwisha kama maji, tutaanza kuulizana tu baadaye
Ukiangalia hizo kauli hapo chini unaona ni usanii tu

Bajeti ijayo...........
Waziri amelisemea...........
Mchakato unaendelea.......
Upembuzi yakinifu unaendelea.......

Nashangaa sana kusikia ahadi kuwa serikali itajenga uwanja wa ndege, sijui kama kweli ni uwanja a ndege au ni kutengeneza runway ya vumbi na kuimwagilia maji.

Kununua meli kubwa, wakati pantoni Kigamboni mpaka leo anajua Mungu lini itakuja.

Maji nchi nzima wakati Dar kwenyewe maji issue kubwa sana.

Nimekusoma mkuu, mkoa kuwa jiji JK anadhani ni kubadilisha jina tu inatosha! Hospitali kuwa ya rufaa bila madaktari bingwa,ndo hapo utaona hosp ya rufaa nayo inatoa referral kwenda muhimbili na si nje ya nchi...Kweli hayo majibu ya upembuzi yakinifu sijui makini,mara waziri katoa mkakati ndo yale yale WANAKUJA LEO WANATUPIMA SIZE ZA MIGUU YETU ILI WATUNUNULIE VIATU AFU WANARUDI TENA BAADA YA MIAKA MITATU WANATUULIZA "MNATAKA VYA RANGI GANI VILE,MANAKE FUNGU LIMESHATENGWA"!
 
68. Tatizo la Maji Morogoro mjini, Kilosa na Kilombero kuwa historia
67. Tatizo la msongamano wa magari Dar kumalizwa kabisa
69. TUKUMBUSHENI NA NYINGINE
 
Mengi yanatekelezeka, tatizo kubwa la kikwete hana uamuzi kama mkuu wa nchi ni lazima apate ridhaa ya Rostam Aziz, Lowassa, Makamba, Mafisadi+vifisadis and Co Ltd
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom