Kila Mpiganaji wa JWTZ arudi nyumbani.

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
26,456
45,521
..every combatant must return home.

..nimesikitishwa sana na habari kwamba askari wetu aliyetumwa Comoro alizama baharini na mwili wake haujapatikana mpaka leo.

..kilichonishangaza ni kwamba askari huyo hakuzama kutokana na shambulio la adui. inadaiwa alianguka majini wakati wakipakua mizigo.

..hisia zangu ni kwamba askari huyo hakuwa na ujuzi wa kuogelea, na hata wenzake ambao wangepaswa kumuokoa hawakuwa na ujuzi huo pia.

..inawezekana kabisa Tanzania ilipeleka askari kufanya amphibious invasion bila kuwa-train ktk masuala ya kuogelea na kuchupa mbizi.

..askari wetu were not under enemy's fire kwanini hawakumuokoa mwenzao? je askari wetu walipewa vifaa gani vya kuokoa majeruhi na haswa ktk mazingira ya baharini?

..naomba wanaohusika wahakikishe kijana, askari wetu, aliyefariki Comoro anarudishwa nyumbani na kuzikwa kwa heshima zinazostahiki.

..EVERY SOLDIER MUST RETURN HOME.
 

Icadon

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
3,583
178
Mkuu hii niliuliza kwenye ile thread ya majeshi yetu Comoro na sikupata jibu.
 

Nzokanhyilu

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,078
87
JokaKuu na demand kali na ngumu. Sasa atapatikana vipi sasa hivi? Au unataka uletewe maiti feki ndio uamini?
 

Icadon

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
3,583
178
Hili la mwili, nadhani tukubali hautopatikana tena, ila swali langu liko kwenye haya maswala ya kuogelea na kupiga mbizi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom