Kila Mkuu wa Wilaya afanye haya, mtaona mabadiliko

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,341
2,000
Naomba Kilwa Mkuu wa wilaya katika wilaya yake amwagize afisa elimu (W) ampe idadi ya madawati yanayohitajika katika shule zote wilayani. Baada ya hapo amwite mkurugenzi wa wilaya/mji/manispaa pamoja na mkuu wa idara ya ujenzi na idara ya misitu na mkuu wa idara ya mali asili.

Kisha awaagize kama ifuatavyo:

1. Mkuu wa idara ya misitu na yule wa mali asili wahakikishe wanachukua mbao ama kwa kutafuta mpya au zilizotaifishwa zinazotosheleza kutengeneza madawati yote yanayohitajika na wazilete wilayani

2. Mkuu wa idara ya ujenzi aagizwe kwa kutumia kitengo cha mafundi selemala wa wilaya watengeneze madawati yote kwani wanalipwa mshahara kwa ajiri hiyo.

3. Mkurugenzi wa wilaya ahakikishe mahitaji ya gari, misumari, na vitu vingine vinapatikana.

4. Mkuu wa wilaya awape miezi 3 yawe yamekamilika. Hapo kazi ya mkuu wa wilaya itaonekana

Hatuhitaji kuomba misaada na kuchangisha wananchi kwa ajiri ya madawati wakati tunauza mbao na magogo china na kwingineko.

Kama maelezo yangu hamuyaelewi nitafuteni niwasaidie!!

Mh. Pinda, nipe kazi ya ukuu wa wilaya hata miezi 3 tu uone mabadiliko!!!

Siku njema wakuu wa jamvi.
 
Chumchang Changchum

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
5,232
2,000
Nnali si mwenyeji wa uko uko,Aliwafundisha walimu wajibu wao wakamfukuza kazi sasa wakikupa ukuu wa wilaya miezi mitatu si watajisuta wenyewe?
 
Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,341
2,000
Hivi wakuu wa wilaya mbona hamchangii hii mada? au kwa kuwa haina sitting allowance???
 
kagangana

Member
Jan 30, 2015
96
95
Kazi hii ingekuwa jukumu la Waziri Mkuu au hata Rais. Wakati wa Mwalimu, Ukuu wa Wilaya haukuwa ulaji. Rais alikuwa anaagiza:Kila Mkuu wa Wilaya anapewa miezi 6 kuhakikisha Shule zote zina madawati, vinginevyo anafukuzwa. Ingekuwa hivyo tusingekuwa na aibu hii ya kukaa watoto wetu kwenye vumbi, mawe au ndoo. Vinchi vilivyojaa jangwa kama Chad watoto hawakai chini. Kuhusu watengenezaji wa hayo madawati wapewe vikundi vya vijana na au wafungwa. Kipato kitakachopatikana kisaidie hao vijana na idara ya magereza pamoja na familia za wafungwa. South Africa na Malaysia wanaendesha magereza yao kwa njia hii.
 
Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,341
2,000
Nilitaraji wahusika wa mada kama hii (wakuu wa wilaya, mikoa, n.k.) wachangie ni kwa nini wanashindwa kutekeleza majukumu yao ili hali mali asili kama misitu tunavyo, lakini naona kimya tu. Sijui watanzania tukoje, ukileta mada ya porojo au mapenzi au ujinga mwingine kama wa CHADEMA ni magaidi inachangamkiwa kweli lakini ukileta mada ambayo ni muhimu kwani inagusa maisha ya watu wetu huoni hata mchangiaji.

Nauliza tena hivi wakuu wa wilaya Tanzania hii mada hamuioni??? au mko Dodoma mnadani???
 
kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
4,125
2,000
Nilitaraji wahusika wa mada kama hii (wakuu wa wilaya, mikoa, n.k.) wachangie ni kwa nini wanashindwa kutekeleza majukumu yao ili hali mali asili kama misitu tunavyo, lakini naona kimya tu. Sijui watanzania tukoje, ukileta mada ya porojo au mapenzi au ujinga mwingine kama wa CHADEMA ni magaidi inachangamkiwa kweli lakini ukileta mada ambayo no muhimu kwani inagusa maisha ya watu wetu huoni hata mchangiaji.

Nauliza tena hivi wakuu wa wilaya Tanzania hii mada hamuioni??? au mko Dodoma mnadani???

Wanaangalia wapi pakuegemea wanawapa kampani watia nia.
Wakimaliza watakuja...
 
Sorrow to Joy

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
292
0
Kwa bajeti ipi? Kazi za umma watu hawakurupuki kutoka machakani. Kila kitu kina utaratibu. So wakurugenzi wasinunue madawa wakuchongee hizo mbao?

naomba kilwa mkuu wa wilaya katika wilaya yake amwagize afisa elimu (w) ampe idadi ya madawati yanayohitajika katika shule zote wilayani. Baada ya hapo amwite mkurugenzi wa wilaya/mji/manispaa pamoja na mkuu wa idara ya ujenzi na idara ya misitu na mkuu wa idara ya mali asili.

Kisha awaagize kama ifuatavyo:

1. Mkuu wa idara ya misitu na yule wa mali asili wahakikishe wanachukua mbao ama kwa kutafuta mpya au zilizotaifishwa zinazotosheleza kutengeneza madawati yote yanayohitajika na wazilete wilayani

2. Mkuu wa idara ya ujenzi aagizwe kwa kutumia kitengo cha mafundi selemala wa wilaya watengeneze madawati yote kwani wanalipwa mshahara kwa ajiri hiyo.

3. Mkurugenzi wa wilaya ahakikishe mahitaji ya gari, misumari, na vitu vingine vinapatikana.

4. Mkuu wa wilaya awape miezi 3 yawe yamekamilika. Hapo kazi ya mkuu wa wilaya itaonekana

hatuhitaji kuomba misaada na kuchangisha wananchi kwa ajiri ya madawati wakati tunauza mbao na magogo china na kwingineko.

Kama maelezo yangu hamuyaelewi nitafuteni niwasaidie!!

Mh. Pinda, nipe kazi ya ukuu wa wilaya hata miezi 3 tu uone mabadiliko!!!

Siku njema wakuu wa jamvi.
 
10Shoka14

JF-Expert Member
May 10, 2012
305
250
Kwa bajeti ipi? Kazi za umma watu hawakurupuki kutoka machakani. Kila kitu kina utaratibu. So wakurugenzi wasinunue madawa wakuchongee hizo mbao?

Dawa zipi hizo wanazonunua?
Unajua bei ya mafuta yanayojazwa kwa matumizi ya Serikali?
Uwe unatafakari kwa kina kabla ya kukurupuka toka machakani,na sijui ulikuwa unafanya nini huko machakani
 
Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,362
2,000
Mie nilifikiria utasema wananchi.

Wananchi wabishiiiii,wazazi mashuleni wakiabiwa mchango wa madawati utawasikia kwamba serikali ndio wafanye hivyo.

Shule ya Olypmio na Bunge ni za Serikali,lakini angalia wazazi walivyozibadilisha na kuwa Kama International Schools,na mpaka kufikia kwamba kupata nafasi pale ni mbinde.

Suala ni wazazi kubalidika.Kuna Mbunge Mmoja wa CUF bungeni yeye alisema kabisaa kwamba watoto ni mali ya serikali kwa hiyo ibebe majukum
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom