Kila mkoa utakuwa na kikombe chake, kama kile cha Babu wa Loliondo! Sasa Rukwa Kipo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila mkoa utakuwa na kikombe chake, kama kile cha Babu wa Loliondo! Sasa Rukwa Kipo.

Discussion in 'JF Doctor' started by nkyandwale, Apr 5, 2011.

 1. nkyandwale

  nkyandwale Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Hivi karibuni kwa imani, Mungu anaonesha vipaji vya utambuzi na matumizi ya mimea, na kwa madai kuwa baadhi ya miti imekuwa tiba tosha kwa maradhi sugu yanayowasumbua watu kwa kitambo kirefu kama vile, kisukari, saratani, shinikizo la damu...na pamoja na UKIMWI.
  Mwishoni wa wiki Bibi Eva Machelela mkaazi wa Mazwi katika Manispaa ya Sumbawanga ameibuka na kikombe kama kile cha Babu Ambilikile wa Arusha-Loliondo, Bibi Machelela ameitaka jamii ijitokekeze kupata kikombe kwa gharama ya shilingi mia tano hata pungufu ya pesa hiyo, kwani lengo lake ni tiba kwa waathirika wa magonjwa hayo.
  Bibi huyo ameeleza kuwa dawa hiyo ameonesha na Mungu zaidi ya mara tatu katika maombi yake ya kila siku na kwa mara ya kwanza aliinywa na familiya yake na baadaye alimnywesha mgonjwa wa kifua kikuu na Mshipa. Baadhi ya viongozi wa serikali, wanasiasa na dini wameonja kikombe hicho. TUTAWA O NA WENGI!:hug:
   
Loading...