Kila la kheri Prof Kabudi ila chonde chonde usiende kujibishana na Lissu kazi hiyo waachie mabalozi!

Nachukua fursa hii kuwapongezeni nyote Dr Mahiga na Prof Kabudi kwa kubadilishana majukumu.
Sina wasiwasi na Dr Mahiga kwenye wizara ya Sheria kwani hata Kombani rip na Mary Nagu waliimudu hii wizara japokuwa si wabobezi/ wataalamu wa sheria. Wewe ukiwa mwanasheria sina shaka yoyote.

Pia Prof Kabudi wewe unaaminika katika kujua mengi lakini zaidi ikiwa historia na sheria za ndoa. Sina shaka ubobezi wako katika historia utafanya majukumu yako kuwa mepesi.
Ombi langu kwako ni moja tu usimpuuze Tundu Antipas Lisu aliyeko ulaya ila usimtilie maanani. Usijibizane naye bali jukumu hilo waachie mabalozi kama alivyofanya Dr Mahiga maana wadhifa wako ni wa juu.

Jumapili njema
Maendeleo hayana vyama!

how do you say kabudi asimjibu lissu, na hadhi ipi unayoizungumzia??

under common wealth tradition lissu ni waziri kivuli likewise kabudi ni waziri wa serikali hawa watu hawakwepani
 
Wazungu ndio wanaume?........ Chadema bhana!
Umesau kuwa wanaokufanya uandike unafiki humu walimwita mwenyekiti barrick ambaye ni mzungu kuwa amekuja mwanaume kwa ndege binafsi.....Najua huwezi kukumbuka we kenge kwakua kazi yako ni unafiki kwa kupiga vigeregere tu mithili ya wamama wajane!!
 
Hahahaa...... Umesikia Arusha wanavyozigombea

2020 Bwashee Lema kwaheri!

Ni kweli ila sio kwa kura bali Magufuli atatumia madaraka yake kuagiza tume na jeshi kuhakikisha hilo linatimia. Arusha hamna fala wa kununua plastiki kwa 20,000. Ukitaka kujua kuna wizi wa mchana kweupe unaendeshwa na rais na genge lake, hizo pesa za hizo plastiki zinaingizwa account gani na nani anasimamia na kuzikagua matumizi yake?
 
Kwanini kabudi asinge teuliwa kuwa katibu mwenezi ccm?! Lowasa awe naibu waziri wa habari akafanye kazi na mwakyembe hahgaha.
Shonza akarithi yule bibi Mugagama awaachie vijana wizara yao.
Mkuu nani mshauri wa Magufuli?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli Kabudi ni mwalimu, anachofahamu ni historia na ni mpiga porojo mzuri. Magufuli Kampa Kabudi hiyo wizara kwakuwa anajua kiingereza na anaweza kwenda kusema chochote alichomtuma. Kwa bahati mbaya Kabudi hajui wazungu hawana muda wa porojo na Mahiga hilo analijua. Kabudi kakaa kikao cha makinikia na wazungu kashindwa. Sheria zenye vimelea vya kupora haki na uhuru wa wananchi zimepita chini yake. Juzi kaingizwa mjini na kampuni fake ya Wakenya kuhusu korosho. Sasa kama anasaini mkataba na kampuni fake ataoongea nini kwa wanaume huko duniani?
Kwa hiyo we n mwanamke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
John Unataka kuniambiaje.... kwamba Palamagamba Kabudi ni Msirikali?
 
Back
Top Bottom