Kesho inshallah, mawakili wetu watakuwa wanawasilisha majumuisho yao yenye kuonyesha kwanini maelezo ya mshitakiwa #2 yanakosa uhalali mbele ya mahakama.
Haiyumkiniki kurasa zisizozidi 5 zitawatosha wasomi hawa kulithibitisha hilo pasipo na shaka yoyote.
Staajabu ya Mussa uyaone ya Firauni.
Bila shaka upande wa pili nao watakuwa hivi sasa wamepinda migongo wakisaka kuthibitisha kuwa mshitakiwa wa pili aliyatoa maelezo tata haya kwa Kingai kwa mujibu wa sheria na taratibu zote zikifuatwa.
Ama kweli moyo wa mtu msitu!
Katika timu mbili hizi kuna moja ni waongo wa kupindukia na wanajua kuwa wanadanganya. Macho makavu! Hata kama wanachoshudia ni uongo.
Wenyewe wanasema Dua la kuku.
Sirro alikwenda mbali zaidi kusema tukamwulize Mbowe. Ajabu ni kuwa hakudhani tungemwuliza Kingai pia? Kumbe pia tumwulize haswa:
Yuko wapi Moses Lijenje?
Kila La Kheri Mawakili wetu. Mola akawasimamie. Kazi yenu hii ya kuisaka haki kwa niaba ya wengine ikapate baraka zake.