Kila La Kheri Mawakili wetu Kuelekea Kesho

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,852
2,000
Kesho inshallah, mawakili wetu watakuwa wanawasilisha majumuisho yao yenye kuonyesha kwanini maelezo ya mshitakiwa #2 yanakosa uhalali mbele ya mahakama.

Haiyumkiniki kurasa zisizozidi 5 zitawatosha wasomi hawa kulithibitisha hilo pasipo na shaka yoyote.

Staajabu ya Mussa uyaone ya Firauni.

Bila shaka upande wa pili nao watakuwa hivi sasa wamepinda migongo wakisaka kuthibitisha kuwa mshitakiwa wa pili aliyatoa maelezo tata haya kwa Kingai kwa mujibu wa sheria na taratibu zote zikifuatwa.

Ama kweli moyo wa mtu msitu!

Katika timu mbili hizi kuna moja ni waongo wa kupindukia na wanajua kuwa wanadanganya. Macho makavu! Hata kama wanachoshudia ni uongo.

Wenyewe wanasema Dua la kuku.

Sirro alikwenda mbali zaidi kusema tukamwulize Mbowe. Ajabu ni kuwa hakudhani tungemwuliza Kingai pia? Kumbe pia tumwulize haswa:

IMG_20210930_170832_807.jpg

Yuko wapi Moses Lijenje?

Kila La Kheri Mawakili wetu. Mola akawasimamie. Kazi yenu hii ya kuisaka haki kwa niaba ya wengine ikapate baraka zake.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
19,641
2,000
Kesho inshallah, mawakili wa wetu watakuwa wanawasilisha majumuisho yao yenye kuonyesha kwanini maelezo ya mshitakiwa #2 yanakosa uhalali mbele ya mahakama.

Haiyumkiniki kurasa zisizozidi 5 zitawatosha wasomi hawa kulithibitisha hilo pasipo na shaka yoyote.

Staajabu ya Mussa uyaone ya Firauni.

Bila shaka upande wa pili nao watakuwa hivi sasa wamepinda migongo wakisaka kuthibitisha kuwa mshitakiwa wa pili aliyatoa maelezo tata haya kwa Kingai kwa mujibu wa sheria na taratibu zote zikifuatwa.

Ama kweli moyo wa mtu msitu!

Katika timu mbili hizi kuna moja ni waongo wa kupindukia na wanajua kuwa wanadanganya. Macho makavu! Hata kama wanachoshudia ni uongo.

Wenyewe wanasema Dua la kuku.

Sirro alikwenda mbali zaidi kusema tukamwulize Mbowe. Ajabu ni kuwa hakudhani tungewauliza Kingai pia? Kumbe pia tumwulize haswa:

View attachment 1961688

Yuko wapi Moses Lijenje?

Kila La Kheri Mawakili wetu. Mola akawasimamie. Kazi yenu hii ya kuisaka haki kwa niaba ya wengine ikapate baraka zake.
Mungu abariki kazi za mikono yao. Mkono wa Bwana tumeuona ktk menendo wa mshitaka haya.

Hakina mwenye haki huishi kwa imani.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,584
2,000
Namlilia Lijenje.

Hao waliomtupa Lijenje wakamatwe na wahojiwe walikomtupa. Au la, mkono wa Bwana, tunaomba uingilie kati ili hao waliomtupa wajenje wajute, walie na kusaga meno mara mia zaidi ya wanafamilia wa Lijenje.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,584
2,000
Leo Kanisani CHADEMA tumeomba Misa kwa ajili ya mawakili wetu.Baada ya padre kusoma ujumbe wote kanisa lote likawa kimya !!Mungu ni mwema
Nami naungana nanyi kwa sala hii.

Mungu wetu umtazame mtumishi wakp Freeman Mbowe, ukamjaze afya njema mara 10 zaidi ya awali, ukamjalie ujasiri usiotetemeshwa, nao wenye kumfanyia hila, wakakutane na mkono wako wenye nguvu hata wasiweze kunyanyuka kufikia urefu wa magoti yao. Amani isipatikane popote wawapo.

Nao wafanyao kazi Takatifu, ya kuipigania haki ya Freeman Mbowe, ukawajalie uelewa mpana, wakaikumbuke hekima yote, yaani kama ile ya Sulemani. Nao wateteao uovu, wakafubazwe ufahamu wao, hata mawakilisho yao yakawashangaze wote wenye uelewa na ufahamu. Lakini hao wateteao uovu, nao wala wasipate nafuu tofauti na wenye kuutenda uovu wenyewe.

Kila mateso na fadhaa alizozipitia mtumishi wako, watesi wake zikawandame mara 100 zaidi. Bwana naijua hekima yako, naijua huruma yako na uaminifu wako. Kama ulivyoyasikia maombi mengine ya mtumishi wako mnyonge lakini mwenye ujasiri mkubwa kwaajili ya neno lako, hata ukatenda zaidi ya nilivyotarajia, ndivyo ilivyo imani yangu katika hili maana uliniahidi kupitia mtumishi wako kuwa wao wenye kuyatekeleza maagizo yako, maombi yao lazima yataifikia nafsi yako.

Amina.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,852
2,000
Namlilia Lijenje.

Hao waliomtupa Lijenje wakamatwe na wahojiwe walikomtupa. Au la, mkono wa Bwana, tunaomba uingilie kati ili hao waliomtupa wajenje wajute, walie na kusaga meno mara mia zaidi ya wanafamilia wa Lijenje.

Dua

Dua la kuku lilimpata bwana yule sembuse hawa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom