Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Katibu Mkuu wa chama mheshimiwa Vincent Mashinji alimteua Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Babu Nyarembe Chadema (Bavicha) na Diwani wa kata ya Butimba John Pambalu Comrade kukiwakilisha chama katika mkutano mkuu wa vyama vya kidemokrasia duniani nchini Finland.
John Justine Pambalu ameambatana na kamanda Doricas Francis ambaye ni msaidizi katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa mheshimiwa Julius Gabriel Mwita.
Mheshimiwa John Justine Pambalu na Doricas Francis watashiriki vikao hivyo vya mkutano Mkuu wa vyama vya Kidemokrasia Duniani nchini Finland kwa siku nne (4) kuanzia leo tarehe 08/11/2018 mpaka tarehe 12/11/2018.
Nawatakia kila la kheri makamanda. Mkiwakilishe chama chetu vizuri ili tuweze kuvuna maarifa kutoka vyama vingine kutoka mabara yote duniani kupitia ninyi. Kila la kheri. Mungu awalinde na kuwapigania