Kila Kukicha Kamati za Bunge Zanusa Ufisadi: Fisadi Yuko Wapi?

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
Wana JF hivi karibuni kamati za Bunge zilikuwa zikipitia hesabu za mashirika na idara mbalimbali za serikali ila jambo la kushangaza ni kwamba kila Kamati ilipokuwa ikienda kesho yake nilishuhudia kwenye magazeti vichwa vya habari kama, "Kamati ya Bunge Yanusa Ufisadi TCRA." Kingine "Kamati ya Bunge Yanusa Ufisadi Mamlaka ya Korosho" bado kingine "Kamati ya Bunge Yanusa Ufisadi Halmashauri". "Kamati ya Bunge Yakataa Tena Hesabu za Bodi ya Utalii". n.k, n.k, n.k!!

Nimebaki najiuliza hivi fisadi yuko wapi sasa? Ina maana Tanzania yote imejaa mafisadi? Ina maana wote wanaofanya ufisadi huo ni wana CCM? Mbona CCM inatuambia kuna mafisadi watatu? Kama nchi inanuka ufisadi kiasi hiki nini kinatakiwa kufanyika ili hata serikali yenye viongozi ambao si mafisadi ikiingia madarakani iondoe ufisadi uliotamalaki kila mahala? Mwisho kabisa ukiniondoa mimi, nani si fisadi?
 
Mkuu kuna jamii za waTanzania ambao wanajiona wamesoma sana ndo wanoongoza hayo mashirika na taasisi mbalimbali za serikali na ndo haohao wanaofanya ufisadi.
 
Kwa lugha ya wenzetu, UFISADI ni KLEPTOCRACY. Google 'kleptocracy' utaelewa fisadi wa bongo ni nani na yuko wapi! Kila kijana wa kibongo mwenye akili timamu akielewa ufisadi ni nini, nina uhakika hatasita kujiunga na harakati ukombozi wa pili wa tiafa hili!!!!:lol:
 
Nionavyo mimi kamati za bunge kazi yao iliyobakia ni KUNUSA tu!Action hamna.
 
Kamati za.bunge zinajitafutia umaarufu tu,hazina meno pili wafanya kazi kwa kukurupuka
 
Mkuu hazina meno wakati huwa nasikia mara zimeagiza watumishi fulani wakatwe mishahara baada ya kufisadi mahala. ila jambo lingine ni hili la wabunge kuwa wajumbe wa bodi na wengine wenyeviti wa bodi hizo! Tunaambiwa dr. Limbu aliingia mitini jana baada ya kuwa wabunge wenzake wamenusa ufisadi kwenye bodi ya pamba ambayo yeye ni mwenyekiti!
 
Alafu waandishi wa habari nao wanakuwepo naona kama mambo ya kuuza sura zaidi kuliko kudiscuss mambo ya maana!
Utashangaa wamepayuka vya kutosha kwenye follow up utakuta zero apo ndo utajua walikuwa wanauza sura!
 
Wakishanusa huo ufisadi wanapewa hela kdg kama milioni za kuwapoteza izo harufu
 
Alafu waandishi wa habari nao wanakuwepo naona kama mambo ya kuuza sura zaidi kuliko kudiscuss mambo ya maana!
Utashangaa wamepayuka vya kutosha kwenye follow up utakuta zero apo ndo utajua walikuwa wanauza sura!
Mkuu usanii hauwezi kuisha nchi hii! Waandishi wa habari nao wasanii watupu, wabunge wasanii, viongozi wasanii, nk. makelele bila ufuatiliaji hayana tija hata kidogo!
 
Wana JF hivi karibuni kamati za Bunge zilikuwa zikipitia hesabu za mashirika na idara mbalimbali za serikali ila jambo la kushangaza ni kwamba kila Kamati ilipokuwa ikienda kesho yake nilishuhudia kwenye magazeti vichwa vya habari kama, "Kamati ya Bunge Yanusa Ufisadi TCRA." Kingine "Kamati ya Bunge Yanusa Ufisadi Mamlaka ya Korosho" bado kingine "Kamati ya Bunge Yanusa Ufisadi Halmashauri". "Kamati ya Bunge Yakataa Tena Hesabu za Bodi ya Utalii". n.k, n.k, n.k!!

Nimebaki najiuliza hivi fisadi yuko wapi sasa? Ina maana Tanzania yote imejaa mafisadi? Ina maana wote wanaofanya ufisadi huo ni wana CCM? Mbona CCM inatuambia kuna mafisadi watatu? Kama nchi inanuka ufisadi kiasi hiki nini kinatakiwa kufanyika ili hata serikali yenye viongozi ambao si mafisadi ikiingia madarakani iondoe ufisadi uliotamalaki kila mahala? Mwisho kabisa ukiniondoa mimi, nani si fisadi?

Uongozi kuanzia juu mpaka chini zimekuwa timu za ulaji tu. Hakuna agenda nyingine
 
wanajulikana.....Lowassa, Rostam na Chenge..mpaka akili zitakapowaingia kila kitu kitakuwa hakimo!!
 
Back
Top Bottom