Kila kitu unachopaswa kujua kuhusu Cryptocurrency na Bitcoin na kwanini siyo uwekezaji mzuri kwako kwa sasa

Kuhusu Forex na Bitcoin nk

Nitajaribu kuelezea kidogo kwa kadri ya ufahamu wangu na uzoefu nilionao juu ya hizi biashara.

Kinyume na watu wengi wadhaniavyo ama walivyoaminishwa Forex au Bitcoin sio utapeli na wala sio biashara ya Pyramid Scheme kama DECI,QNet na zinginezo.

Forex:

Kama jina lilivyo hii ni biashara halali ya kuuza na kununua fedha(Foreign Currency Exchange) ili kupata faida ndogo kutokana na utofauti wa thamani ya fedha hizo.

Biashara hii tunaweza kuifananisha na Bureau de Change iliyokuwa simplified na kuweza kufanyika kidijitali kwa kutumia Computer ama simu ya mkononi.

Mfano mwingine mzuri ni soko la hisa ambalo pia mfumo ni ule ule wa kuuza au kununua hisa za makampuni mbalimbali ambazo pia hupanda au kushuka kutegemeana na hali ya kibiashara ya kampuni husika.

Ikumbukwe pia hizi ni biashara kama zilivyo biashara zingine hivyo kuna pande mbili za matokeo,kupata faida ama kupata hasara japo lengo na jitihada huelekezwa kupata faida zaidi na ku-minimize hasara.

Forex hulenga kuwahi kununua fedha inayoonekana kupanda thamani mapema kwa bei ndogo na pale inapokuwa imepanda thamani kuiuza kwa bei ya juu na hivyo kutengeneza faida kwa utofauti uliotokana na bei ndogo ya kuinunua na bei kubwa ya kuiuza.

Thamani ya fedha hubadilika kupanda au kushuka kutokana na mambo mengi kama kukua au kuanguka uchumi wa nchi kutokana na uzalishaji bidhaa,uuzaji au ununuaji nje(Import/Export)Vita,Migogoro,Majanga kama hili la Corona nk.

Kujua taarifa hizi mshiriki wa biashara hizi ni lazima awe mfuatiliaji wa habari za kiuchumi kwa karibu kwani ndio hasa dira ya biashara yake kujua ni wakati upi sahihi kuuza fedha aliyohodhi kwa kuwa ipo kwenye demand kubwa ama kununua fedha inayopanda ili aiuze baadae.

Formula ni ile ile ya kiuchumi kuwa demand ikizidi bei huongezeka na soko likifurika ama demand kupungua na bei hushuka.

Mfano mzuri ni wa wafanyabiashara wa mazao huyanunua wakati wa mavuno wakati yako mengi na bei ni ndogo na kuja kuyauza baadae wakati kuna uhaba na bei ikiwa imepanda maradufu.

Tatizo la Forex Tanzania ni kuvamiwa yaani watu wametaka kuifanya kama ni get rich quick scheme kwa haraka bila jasho ili mradi wana mitaji.

Forex yahitaji kuisoma kiundani,kufanyia mazoezi makali (demo accounts) na kujifunza saikolojia ya uvumilivu na kutosheka na faida yaani kuwa na trading plan ya kufuata na sio kuyumba kwa kuendeshwa na tamaa.

Wengi wamepata shida kwa kutaka kufanyiwa trading na wengine waliowaaminisha ni wataalamu kumbe nao labda wana ufahamu wa kijuu juu tu na labda walishaanguka kimitaji kwa kutofuata principles sasa wanatafuta fursa za kupata mitaji kupitia kwa watu wengine ambao nao hawafanyi utafiti wa kina kabla ya kuamua kushirikiana na hao wataalamu.

Kiukweli inashauriwa kama mtu hajajifunza hii biashara asiifanye kwani sio Upatu wa kuweka fedha na kusubiri mzunguko ufike alipwe.

Forex yataka elimu,yataka ufuatiliaji na yataka dedication ya full time na sio part time.

Ikibidi kutumia mtu basi yapaswa kuwa na hakika ya uwezo wake na njia rahisi ni kumuomba akupe investor password ya akaunti anayoendesha(iwe ya mfano/demo ama iwe ya ukweli/real) na uifuatilie kwa minimum period ya wiki tatu na hasa vizuri kwa mwezi kuona uhodari wa mtaalamu katika biashara, consistency yake na asilimia ya kufanikiwa faida against asilimia ya losses kabla ya kuamua kushirikiana.

Ni muhimu pia kuwa na mikataba ya kisheria baina ya mtoa fedha na mtaalamu.Hii humpa adabu ya kutrade mtaji wa mtu kwa umakini-responsibly!

Hii ipo duniani kote kuwapo watu wenye mitaji ila hawana knowledge na skills ama muda wa kufanya forex tradings na hivyo kutumia watu wenye skills na muda kwa makubaliano fulani baina yao.

Shida hapa kwetu ilikuja kama wimbi la mafanikio fulani kwamba fulani kapata fedha kwa kuimba basi kila mtu anataka awe mwanamuziki na kusahau kuwa kuna vipaji,elimu,mazoezi ubunifu na determination ya kufanya jambo husika na sio kuingia studio tu na kurekodi.

Kuna mahali nimeona DSE(Dar es salaam Stock Exchange) au soko la hisa wamefungua App ya watu kuweza kushiriki kununua na kuuza hisa viganjani mwao kwa kutumia simu ama computer lengo in ikiwa ni kuwafikia watu wengi na kwa urahisi zaidi.(ni kama platforms za Forex na MT4 au MT5)

Bitcoin:

Hii ni sarafu ya kidijitali iliyoanzishwa na Mjapan aitwaye Satoshi Nakamoto mwaka 2009.

Ni sarafu iliyoendelea kukua na kupanda thamani na huenda hapo baadae ikachukua nafasi ya sarafu nyingi kutokana na uimara wake na umataifa wake(Kuna sarafu za nchi nyingine hazijana nguvu na umaarufu katika masoko ya kimataifa hivyo kutothaminjwa) Kuzigeuza cheap currencies kuwa Bitcoin huzipa thaman na kuzitambua thamani.

Mfano rahisi ni kama Dhahabu inavyowekwa katika mabenki na watu wanaweza kununua au kuwekesha kama amana zinazokubalika duniani kote

Sarafu ya Bitcoin imeanza kutumika kama mfumo wa malipo kwa huduma mbalimbali na mabenki mengi makubwa ya nchi zilizoendelea kiuchumi na kiteknolojia kuzipokea ba kuzitumia
Nachokiona kwa Tanzania na Watanzania ni uoga wa mabadiliko na uelewa mdogo.

Nakumbuka yalipoingia magari yenye mfumo wa Automatic Gear Box watu waliaminishwa kuwa si imara,hamna spare wala mafundi na ilikuwa ngumu sana hata kuyauza.i

Sasa hivi ndio magari mengi na maarufu na wengi hawataki kusikia magari ya manual na wengi wamesahau hata namna ya kuyaendesha au hawajui kabisa.

Dunia sasa inaenda kidijitali na mifumo inabadilika.. Hapa kwetu tumeanza na mifumo ya simu kama M-Pesa.tiGo Pesa,Airtel Money,Z Pesa,T Pesa na Halopesa..

Mwanzoni pia watu walikuwa wagumu sana kuiamini na kuitumia,walipenda zaidi mifumo ya hard cash kwenye kulipa bidhaa,kulipana,kuuza na kununua huduma mbalimbali kama umeme,maji,vocha na muda wa Televisheni.
Wengi wabakumbuka kutuma pesa kwa njia za Telegram Posra,EMS,Kutumia mabasi kama Scandnavia,Kupanga foleni kulipia au kununua umeme,Vocha za kukwangua,Kupanga foleni Mobitel kulipia Airtime nk

Lakini sasa mengi hayo unaweza kuyafanya kirahisi kwa simu na kuokoa muda au gharama za mafuta/ usafiri kwenda benki au vituo vya huduma husika.
Sass hivi kuna Lipa Namba,Masterpass nk unalipa bill za,Hotel,Bar,Maduka unalipia Petrol nk
Ni rahisi kulipa ada za Shule nk.

Ni rahisi kutuma fedha na hata kudeposit na kuwithdraw kweda Benki au kutoka Benki na hii ni kwa muda wowote hata usiku wa manane.

Hizi pia ni e-money(Digital) sio hard cash sasa Bitcoin ni Advanced Digital Currency ambako ndio muelekeo wa dunia yote kwa sasa.
Bitcon moja kwa sassa nadhani ni sawa na Milioni 43 za kitanzania- unaweza ku-google kupata thamani halisi.

Ukiangalia Benki nyingi zinahamasisha kufungua online accounts kwa kutumia Apps zao,kitendo cha dk 5 hadi 10 mtu anafungua akaunti na anaweza kudeposit
Au anacreate debit card kama Master Card au Visa na kuanza kuitumia instantly. Ikiexpire kama ilikuwa na balance inarudishwa kwenye akaunti yako ya simu.

Makampuni ya simu yanahimiza kutumia Apps zaidi kufikia huduma zao na hadi wanatoa ofa kama kutoa bonus ya fedha unapofanya miamala kati yao na mabenki.
Kununua huduma kwa Apps ni rahisi na bafuu kuliko ukitumia USSD codes yaani zile Menu za kubonyeza *150*XX#
Mfano ukinunua bundle la data la wiki la voda kwa USSD code kwa TZS 5,000 utapata GB 2 lakini ukitumi App utapata GB 4 au ukinunua Data bundle la mwezi tiGo kwa USSD utapata GB 21 wakati kwa App pesa hiyohiyo utapata GB 34 (tofauti ya GB 13!)

Dunia inabadilika kuwa Cashless tunaenda Dijitali hivyo si kweli kusema Forex au Bitcoin ni Scams.

Udanganyifu upo kila mahala na wapigaji wapo kote na hupenda kujipenyeza mahali kwenye jambo jipya au lenye uelewa mdogo kwa watu.

Wapo scammers wa makusudi kabisa na wapo makanjanja wa hizi biashara na matokeo huwaingiza hasara sponsors waliowashawishi,ukute hata mtu anasema amepoteza zake alizotoa kuwekeza kuwa katapeliwa isi kwelo ukute ni ameingia loss kwenye real & legal trades na hata huyo mtaalamu wake hajaambulia hata mia na mtaji umenufaisha soko na dalali(Broker)

Tuwe tunajifunza vitu kabla ya kukurupuka kuvivamia na pia tusipende kuita vitu vya ukweli kuwa ni hoax au scams bila kuwa na uelewa navyo(kuvijua) au kuchukulia vile experience mtu aliipata binafsi.

Amini Forex ni real business na watu wanaishi kwa biashara hiyo tena kwa mafanikio makubwa tu.

Tatizo la kuita FX scam ni pale unapotaka kufanyiwa ukiwa huna study kwa uwezo wa anayekufanyia na haraka ya Return of Investment jambo ambalo mara nyingi ni faulo kubwa kwenye hiyo biashara.

Kuhusu Kuku Farm ni farming nzuri kama umeifuatilia mfumo wake ni Cloud farming ambao upo na efficiency nzuri nachokiona ulikwama kutokana na sheria zetu na uelewa(Remember sometimes kuna sheria mbovu) au zisizoenda na wakati.

Ufugaji au Ukulima jumuishi(kutumia washiriki wengi) hukuza mtaji na kupata access ya huduma nyingi na kurahisisha zoezi kuliko kwa individuals wenye mitaji midogo,hawana skills na hawama facilities.

Tunaona hata Mabenki yakiungana ili kukuza mitaji kama mfano wa hivi karibuni tumeona Bank ya CBA ikiungana na Bank ya NIC na hivyo kukuza mtaji na kujipanua kuhuduma na biashara.

Kwa wanaojua mabasi kama ya Super Feo au New Force) yanayoenda mikoani hasa Songea,Mbeya nk ni muunganiko wa wamiliki wengi tofauti (unaweza kuthibitisha hilo kwa kusoma anuani za wamiliki zilizoandikwa chini ya mlango wa dereva) Hivyo biashara za kuinvest mtaji zipo nyingi za ukweli na sio Upatu.
Hata gari nyingi za Uber wanatumia lesseni za tours za kuchangia kupunguza makali na tozo kwa mtu mmoja mmoja.

Sasa DSE imekuja na hiyo program ya kununua na kuuza hisa Online je utaita ni Scam?

Hisa wapo waliobenefit kwa kampuni xa hisa walizonunua kupaa kama CRDB na TBL na wapo waliopata loss kwa hisa walizonunua kudepreciate values mfano kama hisa za TOL(Tanzania Oxygen Limited).

Wanaoinvest kiukweli kwenye Forex au Bitcoin hawana hata time kushawishi watu.Wao wanafanya kwa maslahi yao au ya Investors wanaotafuta ubia kwao.

Ukiona mtu anakushawishi basi huyo bado ni small scale trader anatafuta njia ya kupata kipato kupitia mtaji wako au commission kwa broker kwa kila profit utakayopata(wanaitwa IB au Introducing Broker)
Na hilo unaweza kulikwepa kwa kujisajili binafsi bila kupitia kwa refering person.

Nimeona mtu akisema unafungua akaunti kama Facebook.Hizo zote ni operations za Online huhitaji kuvisit ofisi ya mtoa huduma au kuwakilisha makaratasi.Utatakiwa kuwakilisha nakala za vitambulisho kama cha NIDA,Pasi ya kusafiria,Leseni ya udereva au utility bills kama za umeme au maji zenye jina lako au bank statement kwa aiili ya usalama wa akaunti yako.
Mungu atupe baraka na uhai ili huko mbeleni tushuhudie mabadiliko ya hizi digital business ambazo kwa sasa tunaziona kama gari za automatic.

Kwenye You Tubes na Instagram watu wanaingiza mamilioni kwa kuwa na viewes wengi wa post au musicd na pia followers wengi.Ukimuulizs mtu kama Millard Ayo au Kansiime Anne wa Uganda wanaweza kuthibitisha pay check wanazolipwa kwa activities zao You Tube.

Ujanja upo kila sekta.Counterfeit note zipo,viwanja hewa vipo nk hivyo ni kuwa makini tu huwezi kusema kuwa kuagiza gari Japan ni utapeli labda uliagiza kwa fake agent ukapoteza pesa zako.

Jisomee zaidi hizi links chini na pakua Apps za kujifunza zaidi

APP NZURI NA RAHISI YA KUJIFUNZIA BASICS WEWE MWENYEWE BILA KUHITAJI MWALIMU

IMG_20201211_013138_389.jpg
IMG_20201211_013921_011.jpg
IMG_20201211_025139_866.jpg
IMG_20201211_022707.jpg
IMG_20201211_030249_304.jpg
IMG_20201211_024454_782.jpg
 
Attachments

  • IMG_20201211_024712.jpg
    IMG_20201211_024712.jpg
    45 KB · Views: 5

IMG_20201211_005809.jpg
IMG_20201211_022707.jpg
IMG_20201211_024712.jpg
IMG_20201211_024454_782.jpg
IMG_20201211_030249_304.jpg
 
Tatizo matapeli walishachafua hizi dili kwa kufanya wenzao fursa.
Watu wamepigwa sana.
 
Hivi TMT ya bwana Ontario bado ipo,

Aah wakuu naombeni mnisaidie njia ya kudeposit na withdraw pesa kwa broker,
Challenge hiz nd zilifanya niache kutrade
Kuwithdraw na tatzo kubwa ,

mpesa airtel mastacard aziwezi kupokea hela kabisa
 
nataka niulize huyo mjapani aliyegundua hiyo sarafu ya bitcoin yupo mpaka sasa hivi au kama kuna mtu atakuwa na picha zake atuwekee ili tumuone hata cc outfashioned tung'aze macho
 
Hamna kitu cheapest duniani kwenye mafanikio, haya yote yana risk kubwa kuliko unavyo yapamba wewe, watu wamepoteza pesa wengi sana ila walio fanikiwa ni wa kuhesabu
 
Uzi Mpya ila contents ni zamani sana. Upande Mwingine hata mtoa mada hajui alichoandika ni Sawa na kulazimisha watu kuamini kuna maisha baada ya kifo ili hali wewe hujawahi kuyashuhudia
 
Forex na Bitcoin ni biashara halisi,ukiingia kichwa kichwa unaliwa kichwa kweli.Badala yake ukiwekeza kwenye maarifa utafaidika.Nakupongeza mtoa mada uko sahihi sana.
Screenshot_20201212-002153_MetaTrader%204.jpg
Screenshot_20201212-002210_MetaTrader%204.jpg
 
Back
Top Bottom