Nchi hii inapoteza mwelekeo! Kila kitu sasa ni kwa jina la Nyerere! Eti hata chuo kikuu cha Dar es Salaam kinabadilishwa jina kuitwa Mwalimu Julius Nyerere University. Hii ni sawa? Mbona tunapoteza mwelekeo na historia ya nchi yetu!! Kama tunamuenzi, kwa nini tusifuate maneno na matendo yake, yale yaliyokuwa mema?
Haina maana kuviita vitu kwa majina ya mtu wakati huku nyuma tunafanya kinyume na mapenzi yake. Hii ni tabia mbaya. Tulivyokwisha viita kwa majina yake vinatosha na au kama tunataka tujenge vingine tuviite jina hilo!!