Kila kitu kwa jina la Nyerere ni sawa?

mangifera

Member
Oct 15, 2011
47
34
Nchi hii inapoteza mwelekeo! Kila kitu sasa ni kwa jina la Nyerere! Eti hata chuo kikuu cha Dar es Salaam kinabadilishwa jina kuitwa Mwalimu Julius Nyerere University. Hii ni sawa? Mbona tunapoteza mwelekeo na historia ya nchi yetu!! Kama tunamuenzi, kwa nini tusifuate maneno na matendo yake, yale yaliyokuwa mema?
Haina maana kuviita vitu kwa majina ya mtu wakati huku nyuma tunafanya kinyume na mapenzi yake. Hii ni tabia mbaya. Tulivyokwisha viita kwa majina yake vinatosha na au kama tunataka tujenge vingine tuviite jina hilo!!
 
Nish

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
730
111
yaha mambo yanakifu basi wabadilishe na jina tanzania liwe nyerere
 
kituro

Senior Member
Dec 25, 2010
176
14
Nchi hii inapoteza mwelekeo! Kila kitu sasa ni kwa jina la Nyerere! Eti hata chuo kikuu cha Dar es Salaam kinabadilishwa jina kuitwa Mwalimu Julius Nyerere University. Hii ni sawa? Mbona tunapoteza mwelekeo na historia ya nchi yetu!! Kama tunamuenzi, kwa nini tusifuate maneno na matendo yake, yale yaliyokuwa mema?
Haina maana kuviita vitu kwa majina ya mtu wakati huku nyuma tunafanya kinyume na mapenzi yake. Hii ni tabia mbaya. Tulivyokwisha viita kwa majina yake vinatosha na au kama tunataka tujenge vingine tuviite jina hilo!!

kupakana mafuta kwa kutumia mgongo wa chupa huko!, wanataka waonekane wanamuenzi mzee wa watu wakati wizi mtupu!

sifa hizo anazipenda mtu mmoja hivi anatamani hata nchi iitwe jina lake ili ionekane aliwahi kuwa kiongozi wa ngazi fulani!
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,466
nadhani hapa mkandala kapotoka, lazima historia ilindwe na kuheshimiwa.angetaka mwenyewe angeomba kibadilishwe jina kabla hajafa,
kwanini wasikiite chuo cha kata kwa jina hilo?
duniani UDSM inafahamika itakapobadilishwa jina itakuwa tabu sana kufahamika
sioni umuhimu huo hata UDASA hawajapendekeza kiitwe hivo
Je kile chuo pale kigamboni kitaitwaje kama sio kuchanganya majina.
Let UDSM be UDSM kama ni kumuenzi vipo wajenge kingine au UDOM iitwe hivo.
 
Maamuma

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
853
302
Ukiona hivyo ujue ubunifu hakuna!

Nakubaliana na wewe Mkuu. Hata me nshachoka na hii habari ya "kunyerere" vitu kila uchao. Huko tunakoelekea tutakuwa na:

Nyerere Hospital (Muhimbili)
Air Nyerere (ATCL)
Nyerere Line (Reli ya Kati)
Nyerere Transport (UDA)
Nyerere Market (Kariakoo)
Nyerere Game (Bao)
Nyerere Radio/TV (TBC)
Nyerere stick (?)

It's just too much jamani! Imetosha aah!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom