Kila kitu kilichobuniwa kina mbunifu wake.

Internal

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
3,579
3,913
RNinaamini kabsa kila tunachokiona leo kimebuniwa.

Ni lengo kwenye shabaha moja kwa moja.

Muundo wa mwili wa binadamu unafanya iwepo haja ya kuwako mbunifu wake.

Wanasayansi wanatuambia kwamba ubongo wetu hukusanya na kukumbuka picha elfu nyingi katika mawazo yetu,huyaunganisha matatizo yetu yote na kuyatatua,hufurahia uzuri,huitambua nafasi ya mtu, na kutaka kukuza yaliobora ndani ya kila mtu.

Chaji za umeme zitokazo katika ubongo huongoza shughuli zote za misuli ya miili yetu.


Compyuta pia zinafanya kazi kwa njia ya mkondo wa umeme.lakini ilichukua akili ya mwanadam katika kutengeneza hio kompyuta na kuiambia lakufanya.

Si ajabu, basi, kwamba mtunzi wa Zaburi alihitimishs kwa kusema kwamba mwili wa mwanadam unasilimulia habari za muumbaji wake huyo wa ajabu kwa sauti kubwa ilio wazi:

"Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu,matendo yako ni ya ajabu, wewe wanijua kabsa kabsa" Zaburi 139:14.

Hatuna haja yakwenda mbali ili kuyaona hayo matendo ya ya Mungu.


Umbo la ubongo wetu wenye sehemu nyingi za ajabu na viungo vyetu vingine ni matendo ya Mungu,nayo husonda kidole chake kwa yule mbunifu stadi kabsa.

Hakuna pampu yoyote iliotengenezwa na mwanadamu inayoweza kulinganishwa na moyo wa mwanadam.
 
That's why I love Kitimoto
184523_321779021269572_1835146101_n.jpg
 
Back
Top Bottom