Kwame Nkrumah
JF-Expert Member
- Dec 2, 2008
- 886
- 376
Sijazunguka sana dunia hii, lakini katika nchi mbili tatu zilizoendelea nilizobatika kupita nimeona kuna tofauti kubwa katika baadhi ya taratibu na namna nchi hizi zinavyoendeshwa na nyumbani. Kama una tofauti nyingine umeona au mambo yanayofanana tufahamishe pia.
1. Kazi za serikalini katika nchi hizi ni kazi za wito.Watu huenda serikalini kuhudumia jamii. Watu wanalipwa hela ambayo kwa mtu wa sekta binafsi ni some changes in the pocket.
Kwa nyumbani serikalini ndiyo sehemu ya kuibuka na utajiri, dili za kifisadi kila mahali, Polisi, TRA, Mawizarani n.k
2. Nchi zilizoendelea viongozi ni WATUMISHI, wametumwa kutumikia wananchi.Wanakaa ofisini na kufanya kazi.
Sisi viongozi ni semi-gods, wasemalo ndiyo sheria. Hawapo ofisini kila mara ukienda unaambiwa njoo kesho.
3. Asilimia 90 ya magari ya serikali utakayoyaona ni magari ya huduma kwa wananchi kama vile kuzoa taka, magari ya polisi, ujenzi wa barabara,fire brigades au snow cleaning kama ni sehemu ya winter kali.
Sisi asilimia 90 ya magari ya serikali ni magari ya kupeleka viongozi kazini, kupeleka watoto wa boss shule, mke wa mkurugenzi saloon na kubebea majani ya ng'ombe wa meneja.
3. Bunge ni chachu ya maendeleo.
Kazi ya bunge letu ni "kushauri" serikali. Kila mbunge anayesimama anasema "mimi namshauri waziri......" na kupiga mihuri kila kiletwacho na chama tawala.
4. Wageni wanaheshimu sana sheria za nchi husika.
Kwetu wageni ni "superior" kuliko sisi.Watapewa ardhi mara moja, watapewa kazi nzuri na kwa haraka sana, bila hata vibali vya kazi. Wakati huohuo wazalendo wakiitwa bungeni wezi na Waziri wa Kazi. Wageni watapewa madini na kutuachia mashimo, watatesa na hata kuua raia.
5.Benki zinabembeleza wateja kuchukua mikopo.
KwetU tunabembeleza benki kutupa mikopo.
6. Vyombo vya usalama vina nguvu za kisheria kumchunguza kila mtu. Hakuna mtu ambaye hagusiki. Sheria ni msumeno kwa kila mtu.
Nyumbani utaanzia wapi? Akina yakhe ndiyo tumejaa Keko, Isanga na kule Zanzibar kwenye vyuo vya mafunzo.
7.Cabinet ni ndogo na maendeleo yao tunayaona.
Sisi Cabinet ni kubwa. Ufanisi close to zero.
8. Malalamiko na kashfa mbalimbali huchunguzwa kwa kina na kutolewa majibu mara moja.
Sisi licha ya malalamiko chungu mzima, kwa mifano tu ya Bandari, Airport na Ardhi.hamna hatua yoyote inayochukuliwa. Sana sana ni mkuu wa kitengo kinacholalamikiwa kuongezewa madaraka.
9.Watu wanaoongoza vita dhidi ya mafisadi [ yes, wao pia wana mafisadi], kutetea haki na kusimamia sheria ni mashujaa na wanaheshimiwa na nchi na kuenziwa.
Kwetu watu hawa ni maadui wa umoja, wanataka kuvunja amani na kuigawa nchi.
10.Wananchi wanapiga kura kwa kupewa sera na njia mbadala za kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii husika.
Kwetu sisi wananchi tunachagua viongozi kwa kufuata nani alitupa fulana na kanga nyingi na kupika pilau kushinda mgombea mwingine. shame on us wananchi !!!
11. Wananchi kupata habari ni haki ya kikatiba, a very deep, enshrined and cherished aspect of life.
Sisi kupata habari ni kwa kudra tu.
12. Ukiona ajira inatangazwa gazetini ujue nafasi kweli ipo.
Kwetu ukiona hivyo ujue tayari shemeji wa Mkurugenzi ameishaajiriwa toka mwezi uliopita na tayari yupo nje ya nchi kwenye semina.
13.Wanajeshi wanaheshimiwa, kupendwa na kuenziwa kwa mapenzi waliyonayo kwa nchi yao hata kujitoa kujiunga na jeshi.
Wanajeshi wetu ni maarufu kwa kupiga raia.