Kila kitu bei ipo juu: Je, Rais Magufuli anapambana na umasikini au anapambana na watu masikini?

Mkuu hebu shauri wapi pa kuanzia kuhusu hili maana ni dhahiri wananchi hawakubaliani na hili hasa ukizingatia waziri aliapa kwamba bei ya umeme haitapanda na serekali ilisema gas ikianza kutumika tu umeme utashuka bei. Nadhani mchana ulisema petition inafaa. Hebu toa mwongozo tuanzie wapi.
Unajua kutumia Petition inasaidia kuwaambia wazi viongozi/wafanya maamuzi kuwa wananchi (tena kwa idadi yao) hawapendezwi na hatua iliyochukuliwa.

Mwanzoni viongozi wanaweza wakadharau tu lakini jinsi watu wengi zaidi wanavyozidi ku-sign Petition itasaidia kuleta "attention" kwa jamii na kuona kweli hili jambo linagusa wananchi wengi na si kikundi tu cha watu wachache.

Kule umasaini niliona Petition ikitumika kushinikiza serikali ya Tz kuacha kuziondoa community za kimasai kwenye maeneo serikali iliyotaka kuwauzia wawekezaji. Na hii issue ilifanikiwa.......mimi pia nili-sign Petition.

Mkuu watu kama Avaaz.com huwa haiishii tu watu ku-sign Petition. Wanaowatu wao wenyeushawishi wanawatumia kufikisha ujumbe kwa serikali au shirika kuhusu wananchi wanachodai. Na kama idadi ya signature ni kubwa basi serikali kamwe haitoweza kupuuza.
Hapa kinachotakiwa ni umoja tu
 
Ni masikini daima ataendelea kuishi kama shetani na si tajiri. Kauli ya mkuu sikuwahi ikubali. Eti Dewji, Mengi, Bahresa, Lowassa nk mambo yageuke waishi kama shetani? thubutuu.
 
Unavyopandisha bei ya umeme humkomoi mwenye kiwanda mana na yeye atapandisha bei ya bidhaaa yake kufidia ongezeko la operational cost na mwananchi anaathirika direct. Tuliambiwa kodi kwenye vocha,mobile money transactions,banks transactions hazitamgusa mwananchi lakini leo zigo lote lipo kwa mwananchi. Maisha yanazidi kuwa magumu siku hadi siku. Serikali badala ya kudeal na haya wanamkomalia faru john. Tuna safari ndefu sana.
Nchi ya kusadikika hii mkuu
 
kwani pesa hii ina chapa ya nani?

ya kaisariii

basi mpeni kaisari kilicho chake kaisari, na mpeni mungu kilicho chake mungu.
 
Kwa kweli nchi haielekei vizuri tuna mfumuko wa bidhaa muhim na hili la kupandisha bei ya umeme litazidi kupandisha mfumuko huo, naona msemo wa hapa kazi tu unakua hapa maumivu tu
 
Unajua kutumia Petition inasaidia kuwaambia wazi viongozi/wafanya maamuzi kuwa wananchi (tena kwa idadi yao) hawapendezwi na hatua iliyochukuliwa.

Mwanzoni viongozi wanaweza wakadharau tu lakini jinsi watu wengi zaidi wanavyozidi ku-sign Petition itasaidia kuleta "attention" kwa jamii na kuona kweli hili jambo linagusa wananchi wengi na si kikundi tu cha watu wachache.

Kule umasaini niliona Petition ikitumika kushinikiza serikali ya Tz kuacha kuziondoa community za kimasai kwenye maeneo serikali iliyotaka kuwauzia wawekezaji. Na hii issue ilifanikiwa.......mimi pia nili-sign Petition.

Mkuu watu kama Avaaz.com huwa haiishii tu watu ku-sign Petition. Wanaowatu wao wenyeushawishi wanawatumia kufikisha ujumbe kwa serikali au shirika kuhusu wananchi wanachodai. Na kama idadi ya signature ni kubwa basi serikali kamwe haitoweza kupuuza.
Hapa kinachotakiwa ni umoja tu

mkuu tusiandikie mate, toa muongozo tuanze.
 
jibu liko wazi kabisa, debe la mahindi kutoka elfu 10 mpaka 16 sasa hivi, anachofanya ni kutukomesha sisi maskini.
 
Back
Top Bottom