juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,463
Binafsi namheshimu sana raisi wangu Magufuli japo sikumpa kura yangu(huo ndio ukweli) lakini tunapaswa kuzitii mamlaka tulizonazo.
Wakati anaingia madarakani aliapa wazi kwamba anataka kila mtanzania aifaidi keki ya taifa... Zile ziara zake za kushtukiza hazikunishtua sana. Na hata tumbua tumbua yake haikunishtua kabisa. Maana shida yangu ni kuona unafuu wa sisi walala hoi. Nikashangaa sana kwanza kwa jinsi ishu ya sukari alivoipotezea juu kwa juu na sukari bei haijashuka wala nini!!
Unga/sembe nao bei juu, na sasa umeme unapanda bei. Hivi rais anayajua haya au hajui? Najiuliza, hivi kwa namna ambavyo vitu vinapaa juu bei je raisi anapambana na umasikini au anapambana na sisi masikini? Au haya hayaoni?
Mara nyingi anasema tunaolalamika ni wale tuliozoea pesa za dilidili, jambo ambalo huwa napingana nalo sana kwa kuwa wengine hata kuajiliwa hatujawahi na tunapata pesa ya uhalali na kwa jasho letu, hata dili dili hizo hatuelewi ni kitu gani?!!
Watu tunafanya kazi sana, wengine tunalala saa saba za usiku na kuamka saa 12 au 11 kwenda makazini tena.
Huu msemo wa hapa kazi tu inabidi uendane na maisha jamani.