Kila kitu anafanya Rais Magufuli, wengine kazi yenu ni nini?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,292
33,903
Ukiangalia sasa hivi kwenye kila taarifa watoa taarifa wanasema kuwa kama si Rais Magufuli kufanya hiki na kile jambo fulani lisingefanyika.

Shirika la umma likipata faida, mradi ukijengwa, Helkopta ikinunuliwa na mambo kadha wa kadha lazima isemwe kwamba bila ya Rais Magufuli jambo hilo lisingefanyika. Picha ninayoipata inawezekana huko serikalini hakuna mipango zaidi ya kusubiri maelekezo toka kwa Rais.

Nimegundua pia kwamba tuna lundo la watu wasiohitajika kwani mambo mengi yanafanywa na Rais Mwenyewe. Kumbe Tanesco hawakuwa na mpango wa kupata faida mpaka Rais ndiye amesababisha wao wapate faida.

Inakera kuona kwamba kumbe inawezekana kodi yetu ingefanya mambo mengi sana ya maana kama hao wangoja maagizo wangepunguzwa serikalini na kwenye mashirika ya umma. Huu mzigo ambao watumishi wa umma wanamtwisha Rais Magufuli ndiyo maaana inafika mahali anawaza yeye akiondoka kama haya yanayofanyika sasa yataendelezwa.

Rais asingesema hivyo kama wengi wa walio chini yake wangekuwa wanatoa mchango kwa yale anayoyafanya. Hata CCM hivi sasa kila kitu ni Magufuli. Kwa maoni yangu tupunguze watu serikalini na kwenye mashirika ya umma ili kuongeza tija kwani wengi wao kazi zao zinafanywa na Rais Magufuli mwenyewe.

Viongozi wa CCM nao wakae pembeni maana chama chao hakuna kinachofanya bali ni kutegemea nguvu ya Magufuli kujiendesha!!
 
Tusione aibu kumpongeza Mzalendo Magufuli anafanya kazi kubwa mno
Swali ni kuwa kama hakuna wanachofanya viongozi walio chini yake,kwa nini wasiachishwe kazi?Hilo litampunguzia Rais Stress na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi.Pia itatoa fursa mujarab kwa Mr President kufanya mambo makubwa zaidi.Wampishe apige kazi.
 
Wakati JPM hajateua baraza la mawaziri alikuwa anafanya kazi yeye, Waziri Mkuu Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo, Balozi Ombeni Sefue.

Hizo kazi nyingi zilifanywa na hao watatu kwa weledi mkubwa na mambo yakaenda.

Nataka kuamini hata mawaziri wanafanya kazi, ila Mawaziri walio chini ya huyu JPM wakifanya business as usual watapwaya sana.

So far, wakiongeza ubunifu kwa kushirikiana na watu wengine; bado fursa ya kung'ara ipo.

Teamwork ni kila kitu ili kupata matokeo makubwa na mwisho wa siku sifa watazipata.
Changamoto kuna watu wanataka wao wafukiri na kutekeleza. Yet watokee kwenye media, badala ya kupata matokeo makubwa wanakuwa mediocre.

Bado mna nafasi ya kuobesha uwezo wenu na kwa kuwa mzee anaamini, tunawatakia kila la heri ili mng'are kwenye kuwatumikia Watanzania.
 
Ndivyo walivyo,tunahitajika kuwaambia ukweli.
Utafikiri hawaoni,hawasikii wala hawahusiki.
Wanahitaji kuhurumiwa.
 
Hao wa chini wana kazi kusifia na kushangilia kama ilivo kwa mpira wa miguu.
Swali ni kuwa kama hakuna wanachofanya viongozi walio chini yake,kwa nini wasiachishwe kazi?Hilo litampunguzia Rais Stress na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi.Pia itatoa fursa mujarab kwa Mr President kufanya mambo makubwa zaidi.Wampishe apige kazi.
 
Tusione aibu kumpongeza Mzalendo Magufuli anafanya kazi kubwa mno
Sasa hivi unaongoza kwa upoyoyo jf, hata mbumbumbu Elitwege/Etwege hafui dafu!
Kila Uzi lazima uuparamie tu na nyimbo zako za kumuabudu mungu mtu.
Sijui ni ukoo mmoja na Wakudadavua? ambae hanaga cha kuandika/kukomenti zaidi ya Mbowe na Chadema!
Ndo maana mnaitwa nzi wa kijani khaa!
 
Back
Top Bottom