saidi kindole
JF-Expert Member
- Sep 21, 2012
- 310
- 792
leo tumetembelewa na watu toka manispaa ya kinondoni katika viduka vyetu vyote vilivyopo katika kata ya Tandale tukiambiwa kila mtu mwenye kiduka lazima awe na mtungi wa gas wa kuzimia moto ambao wanatoza Shs. 40,000/- kwa kila mtungi. Tulipowahoji je mitungi hiyo ipo? Wakajibu kuwa mitungi haipo ila tunapaswa kulipia baadae moto ukitokea Fire Brigade watakuja kuzima wakati wakisubiri mitungi hiyo kuagizwa toka nje ya nchi hakuna muda maalumu uliowekwa. je hiyo imekaaje.