Kila kesi mahakama ya Kisutu, hivi Dar nzima kuna mahakama moja tu?

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,899
3,683
Mmeckia nyie wana JF.
Kwanza mambo vp..
Mko bwaxxx!!!

Napenda kuwapa POLE SANA kwa leo hii kuanza rasmi implementation ya bajeti mpya ambayo mnakatwa 18% ya VAT kwa kila transaction ktk bank ATM.

Anyway, hao walikua wadhamini kabla ya habari za michezo (sio zile za Sports HQ za 93.7 FM)

SASA ISSUE IKO HIVI :

Hivi utaratib wa level za mahakama uko vipi mazee..
Je, mahakama ya level zero kabisa ni ile wanaitaga "mahakama ya HAKIMU MKAZI au kuna ingine"

Je katika mkoa panakua na hizo mahakama ngapi vile, moja kwa wilaya.... mkoa???

Je kila kesi lazima ianzie mahakama ya HAKIMU MKAZI ndipo ipande juu zaidi au zingine zinaweza kwenda straight foward??

Je jiji letu kubwa la Darisalama lina mahakama hizo ngapi??
Kisutu peke yake??

Kwanini kila kesi dar utackia inaanzia mahakama ya kisutu tuu???

Lulu alipelekwa KISUTU....
Shekh Ponda KISUTU...
Lissu KISUTU...
Mwaka 2011 wakat wa mgomo pale UDSM (nilikua first year wakat huo) wanafunz waliokamatwa na FFU nao KISUTU...
Kuna yule mhamiaji haramu kutoka Guinea alikimbia mahakaman akataka kuruka fensi akapigwa shaba ya kichwa, nae ilikua KISUTU...

Nina mifano kibao tatizo sina muda nawahi khotuba ya ijumaa masjid..

Ukiona maelezo hapo juu marefu yanaku CHANGANYA achana nayo ww jibu swali hili la msingi kuwa :

Kwanini karibu kila kesi dar inapelekwa mahakama ya HAKIMU MKAZI Kisutu??
Je dar nzima kuna mahakama ya HAKIMU MKAZI moja tuu???

Naenda ibada, nikirud nikute majibu wakuu, nipate kuelimika japo sheria sio fani yangu (nimesoma engineering)
 
moderator peleka jukwaa la sheria hapa sio mahala pake,kule utakuta na na akina shivji watakujibu
 
Mkuu nadhani wakati umefika Jiji la Dar likawa na mahakama kila wilaya level ya mahakama ya Kisutu ili kupunguza msongamano wa kesi katika mahakama moja.Mfano Temeke,Kinondoni & Ilala zote zikawa na mahakama za mahakimu wakaazi.
 
uzito wa kesi ndio unaoipeleka kesi hiyo ktk mahakama husika. Dar kama ilivyo mikoa mingine ina mahakama kuanzia ngazi za mahakama mwanzo kisha ya wilaya kisha za mkoa (Kisutu) na kisha mahakama kuu na rufaa. ukiona kesi zinapelekwa Kisutu ujue zina uzito wa kusikilizwa na mahakama ya mkoa.
 
Kisutu ni mahakama ya mkoa au rufaa??
nieleweshe am little bit confused
 
Kuna Mahakama Ya Mwanzo (W) Ilala - Japo naona kama zipo mbili pale Ilala Wilaya (Ile ya pale Lumumba, na ile iliyo pembeni kabisa mwa Mt. Joseph, kanisa Katoliki).

Kuna Mahakama Ya Mwanzo (W) ya Temeke, ipo mbagala kule,

kuna Mahakama ya mwanzo (W) ya Kinondoni, hii ipo Kinondoni B kama sijakosea, na maarufu Kinondoni Mahakamani.

Kuna Mahakama ya Mkoa wa Dsm, na Ndiyo hiyo Kisutu, maarufu kama Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Kuna Mahakama Kuu, vile vile kuna Mahakama ya Rufaa.

Mahakama Kuu pia zipo kikanda mikoani huko, na siyo kila mkoa kuna Mahakama Kuu,
(mf; Mahakama kuu Kanda ya ziwa, ipo Mwanza).

Zanzibar Pia kuna Mahakama Kuu kule.

Mahakama ya Rufani, ipo moja tu Tanzania, nayo ipo kule kule Dsm.

Kuna Mahakama zingine, zipo ndani ya Mahakama kuu, ila zina mamlaka yake na uzito wake pia. Mfano, Mahakama ya Biashara, na Mahakama ya Kazi.

Mahakama pia zinazidiana uwezo wa gharama, na aina (nature) ya kesi / shutuma. Mf; Kisutu pale ina uwezo wa kushughulikia kesi za tsh kiasi fulani hadi kufikia kiasi fulani, halafu itapanda kuelekea Mahakama Kuu, hadi Rufani.

Kuhusu aina ya kesi, itategemea na uzito wake, japo pia zinaweza kuanzia mahakama za awali, mfano Kesi za Mauaji, zinaweza kuanzia chini kimahakama ila mtuhumiwa hatotakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka (nguvu) dhidi ya kesi hiyo na kuhamishiwa Mahakama ya Mkoa, Kuu, hadi Rufaa.

Nahisi nimejitahidi kumjibu mdau ailyeuliza kuhusu Mahakama ya Kisutu.

Naruhusu kukosolewa ama kuongezwa nililoliacha hapo juu na wabobezi wa Sheria.

Ahsante!
 
Wewe umejuaje kuwa ni msomi wa chuo kikuu? au ndio zile kila aliye humu ni msomi au mwanafunzi wa chuo?
Jamaa ameuliza jambo linalotakiwa kupewa maelezo sio wote wanafahamu.
Soma vzr post yake utajua kwamba n msomi wa chuo kikuu kwa mujb wa maelezo yake. "uckurupuke"
 
Katika Miji mikubwa kama Dsm, mara nyingi Mahakama za Mwanzo, zimo humo humo ndani ya Mahakama ya Wilaya. Na ndiyo maana nimechanganya hapo juu kwa pamoja, kama ukinisoma vizuri.

Ukiwa na shida / tatizo, ndiyo utaelekezwa ni wapi pa kuanzia. Nililiona hili kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Ila ni tofauti na mikoa mingine, mfano mkoa wa Mara, mahakama ya Mwanzo kwa Rorya, ipo Shirati, ila ya Wilaya, ipo Tarime (by then), na hadi sasa naamini wanaitumia hiyo hiyo ya Tarime (ingawa sina uhakika sana, maana ni siku sikufika huko), japo Rorya ishakuwa Wilaya, na wapo kwenye Ujenzi wa Jengo lao wenyewe.

Naruhusu tena Marekebisho na kukosolewa, maana ndiyo kujifunza huku, na wengine naamini wanajifunzia pia mengi kupitia nyuzi kama hizi.

Ahsante!
 
Nadhani swali lako lilipaswa kuwa mapendekezo kwa tume ya utumishi ya Mwahakama na sio swali.

Mahakama ya Kisutu ni ya Mkoa wa Dar es salaam. Mahakama hii ina jurisdiction yake tofauti kidogo na mahakama za wilaya.

Mahakama hii ina uwezo wa kusikiliza mashauri ya rufaa kutoka Mahakama za wilaya lakini ina commital jurisdiction ya kuisikiliza baadhi ya mashauri yanayopaswa kusikilizwa na High Court lakini ili kusevu muda wa mahakama kuu basi Mahakama hii husikiliza kwanza kwa mfano makosa kama ya ujambazi wa kutumia silaa nk.

Kila mkoa una mahakama ya Hakimu Mkazi ambayo ndiyo Mahakama ya mkoa. Pia kuna mahakama za wilaya na Mahakama za mwanza katika kila wilaya.

I hope kwa elimu hii ndogo itakuwa imekupa mwanga kwa nini unaona kesi nyingi zinasomwa kisutu. Hata hivyo sio kweli, mahakama za wilaya zina kesi lukuki sema haujafuatilia tu labda sababu makosa yanayopelekwa Kisutu ni makubwa zaidi na hii ni kutokana na uwezo wa mahakama iliyopewa.

Yawezekana unaona kila kesi inaenda kisutu sababu wewe sio mwanasheria na haufuatilii mambo haya ila unasoma kwenye vyombo vya habari. Wao lazima waende kisutu ndio kwenye kesi kubwa zenye public interest ili wauze magazeti.
 
Mmeckia nyie wana JF.
Kwanza mambo vp..
Mko bwaxxx!!!

Napenda kuwapa POLE SANA kwa leo hii kuanza rasmi implementation ya bajeti mpya ambayo mnakatwa 18% ya VAT kwa kila transaction ktk bank ATM.

Anyway, hao walikua wadhamini kabla ya habari za michezo (sio zile za Sports HQ za 93.7 FM)

SASA ISSUE IKO HIVI :

Hivi utaratib wa level za mahakama uko vipi mazee..
Je, mahakama ya level zero kabisa ni ile wanaitaga "mahakama ya HAKIMU MKAZI au kuna ingine"

Je katika mkoa panakua na hizo mahakama ngapi vile, moja kwa wilaya.... mkoa???

Je kila kesi lazima ianzie mahakama ya HAKIMU MKAZI ndipo ipande juu zaidi au zingine zinaweza kwenda straight foward??

Je jiji letu kubwa la Darisalama lina mahakama hizo ngapi??
Kisutu peke yake??

Kwanini kila kesi dar utackia inaanzia mahakama ya kisutu tuu???

Lulu alipelekwa KISUTU....
Shekh Ponda KISUTU...
Lissu KISUTU...
Mwaka 2011 wakat wa mgomo pale UDSM (nilikua first year wakat huo) wanafunz waliokamatwa na FFU nao KISUTU...
Kuna yule mhamiaji haramu kutoka Guinea alikimbia mahakaman akataka kuruka fensi akapigwa shaba ya kichwa, nae ilikua KISUTU...

Nina mifano kibao tatizo sina muda nawahi khotuba ya ijumaa masjid..

Ukiona maelezo hapo juu marefu yanaku CHANGANYA achana nayo ww jibu swali hili la msingi kuwa :

Kwanini karibu kila kesi dar inapelekwa mahakama ya HAKIMU MKAZI Kisutu??
Je dar nzima kuna mahakama ya HAKIMU MKAZI moja tuu???

Naenda ibada, nikirud nikute majibu wakuu, nipate kuelimika japo sheria sio fani yangu (nimesoma engineering)
usiulize kitu usichokijua Kama vile unakijua, maana mpaka umetoa Ushauri, yaani umeandika vitu visivyokuwepo
 
Back
Top Bottom