Kila kabila lina stahili yake

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Haya madudu wanayofanyiwa baadhia ya wanaume na akina mama yapo kwa kila kabila, utafiti umebaini kuwa ni moja ya taaluma ya Kibantu katika kuongeza au kuthibiti chachu ya mapenzi na ambayo ikitumiwa vibaya inaweza kumfanya mwanaume kuwa chizi wa akili na pengine kupoteza maisha au kazi yake kabisa.


Ukiacha makabila yaliyozoeleka kwa mambo haya ya wanawake kutumia mbinu hizo za asili kuwavuta wanamume katika mapenzi(!) kama vile waTanga, Wahaya, Wanyakyusa, Wapemba, na makabila ya Pwani, inasemekana yapo makabila mengine, ambayo wanawake wanatumia teknolojia kali zaidi na yenye kutia kichefuchefu kama ukijua kuwavuruga wanaume.


Inadaiwa taaluma hiyo ya asili ambayo kwa sasa imeanza kupotea kutokana na wadada na akina mama wengi kuanza kumjua Mungu inaambatana na matumizi mabaya ya baadhi ya viumbe hai ambavyo huwezi kuvidhania vinaweza kulegeza ujanja na nguvu za mwanaume. Inasadikika kuwa wataalamu wa kutengeneza madudu haya ni wanaume wenyewe (waganga wengi wa kienyeji ni wanaume).


Viumbe hivyo ni pamoja na yule mjusi mweupe na laini anaypenda kuishi katika nyumba zetu (mjusi kafiri) wa jamii hii:

4118780.jpg

3199765.jpg

Ukichaganyiwa kwenye menyu (chakula maalumu), hapo utakuwa huchungulii hata barazani, wewe unakuwa ni mtu wa chumbani taulo tu, kila kitu huko huko. Hata kazini hutaki tena.

Pia kuna mijusi wale wanaokaa kwenye mawe au miamba ya mtoni au ziwani:
giantlizard.jpg
4923947.jpg


Ukifanyiwa na mjusi wa aina hizi, inadaiwa kuwa maisha yako ni mdura, ukitoka ndani waenda kazini au kanisani au msikitini, ukirejea tu ni ndani kwenye TV au chumbani na pengine kama ni mtu wa kinywaji wewe kinyawji chako ni cha kuagizia na kuwekewa kwenye jokofu, (friji) mtaani na viwanja unaona nuksi na mama una:

Inasadikika pia yapo makabila mengine wanawake wanawarekebisha ujanja wanaume zao kwa mti unaoinama kama uke wa maua maarufu wanayotumikaa kwa uzio wa nyumba (fenching plants)sijui kwa kigeni uitwa "Bougainvillea plant" kama hii hapa:


PL30000024_Bougainvillea_lg1.jpg



Mzee ukirekebishiwa wewe, kila kitu ni "YES"....unainama kama huo mti muda wote na hapo hutajua kakataa chochote utakachoelezwa na hata kumtukana mama yako mzazi pasipo sababu inakuwa ni kawaida!

Kuna makabila mengine inasemekana wanachanganya na ngozi ya mamba, magamba ya kobe, konokono au kenge.

MAMBA: Wataalamu wanasema mamba ujanja akiwa kwenye maji na nguvu zake nyingi kwenye mkia, ukimshika mkia au ukitaka kushughulika nchi kavu umemmaliza. Mamba akisikia harufu ya mtu akiwa nchi kajavu au jua lkiwa kali sana au mvua ikanza kunyesha huwa anazama majini haraka sana.

alligator_reptile_land.jpg


Ukitengenezewa hiyo ya mamba, yasemekana unaogopa hadi kichaka na upepo, ukisikia kishindo au sauti ya mamsapu, unanywea totally, kama umemwagikiwa maji baridi na pengine kama kuna jambo ulikuwa ukifanya barazani (sebuleni) unakimbia kwenda chumbani au kama anakuja na mizigo unakimbia kwenda kumpokea kwa heshima nyingi.


KOBE: Ukichanganyiwa ya kobe au konokono, tabia zinakuwa kama hao viumbe,(kurudisha kichwa ndani kila ukihisi hatari hata pasipo kushududia nini na ujiami vipi)

african_tortoise.jpg



Hapo mzee ukifokewa tu, unanywe kabisa na kumsii mama akusamehee na pengine kuuliza umfanyie nini ili akuelewe unampenda, kichwa yako muda wote ni aibu tu kil a akisema hata kama ni utumbo wewe una unga mkono, akikaa na watu atakuzuia hata kuongea na unakubali "hakuna shida" kufua utafua, vyombo uatosha, kupika na kupiga deki siku zote iwe kwako na kitanda utatandika, mshahara wote mama ndo atoe maamuzi ya kutumia.
shutterstock_407045.jpg




Mama akitoka na mashosti usiku unamruhusu aende tu wewe utabaki nyumbani ili umfungulie muda wote atakao rudi. Wanaume wenzio wataletwa hapo na kutambulishwa kwako kama mjomba au kaka na wewe utaafiki tu haina shida!



Kenge: Ni shapu wa maamuzi ya uwoga wa kuvurugwa ngozi. Ukimkuta kenge barabara hata kama hajakuona au unapita na hamsini zako, atakimbia zaidi zaidi ya maili ishirini kujificha. Mzee ukichanganyiwa chakula yako na ngozi ya kenge inasemekana wewe ukiambiwa kitu unakuwa mwepesi wa maamuzi ya utekeleza, hata kama kwa mtu wa kawaida angeona hakiwezekan au kama ni masuala ya hela basi hata kukopa utakopa !!!!!!>…

410933.jpg


Kinyonga: IPO ya kinyonga , hiyo baa, ni wale wanaume wapole kupitiliza! hata kuongea ni kazi ndani ya nyumba hata ofisini anakuwa ni mtaratibu katika kila jambo na daima ni mtu wa kupenda kuomba misamaha hata akikosewa yeye.Siku zote ukimwona ni mwenye huzuni tele machoni lakini ukimdadisi kuhusu mkewe anaweza hata kukutusi.
zvt-zimp%20chameleon%20cape%20dwarf%20MdV%20june%202008.jpg








 
...:D concoction of Abracadabra and "mumbo-Jumbo!"
 
Back
Top Bottom