Kila binadamu hufa kwa tatizo la upumuaji, hakuna anayekufa na kuendelea kupumua

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,902
Kila binadamu hufa kwa tatizo la upumuaji pumzi ikikata ndipo hufariki hakuna akaendelea kupumua

Siku hizi kuna ujinga unasambaa mtu akifa tu utasikia lilikuwa tatizo la kupumua!!

Tafsiri ya kifo chochote ni pumzi kukatika ndio maana kuangalia mtu kama kafa huangaliwa upumuaji.

Sasa haya maneno ya kusema mtu kafa kwa tatizo la kupumua yanatoka wapi?
 
Unataka kusema nini?

Ni hivi hakuna sababu za kueleza sana tuacheni tutakaokufa tutakufa na tutakaopona tutapona.

Endeleeni kula mema ya nchi.
 
Wanapoandika sababu ya kifo kuwa ni tatizo la upumuaji au kushindwa kupumua, kitabibu maana yake wanamaanisha kuwa tatizo la mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi ndio chanzo.

Na 'injini' ya mfumo wa hewa huwa ni mapafu, hivyo kwa lugha nyingine ni sawa tu na kusema mapafu yamefeli.

Sababu nyingine za vifo huwa haziwi sababu mama ya mapafu kushindwa kuchakata uingiaji na utokaji wa 'oksijeni' ama 'kabonidayoksaidi'
 
Bora ukiambie hiki kiazi, huyu ni kiazi tu Ila nadhani kwa maelezo yako huenda akaelewa, huenda.
 
Akili za vijana wa ccm huwa zinanishangaza sana.sijuwi kwanini mna uelewa mdogo hivi.
 
Kila binadamu hufa kwa tatizo la upumuaji pumzi ikikata ndipo hufariki hakuna akaendelea kupumua

Siku hizi kuna ujinga unasambaa mtu akifa tu utasikia lilikuwa tatizo la kupumua!!

Tafsiri ya kifo chochote ni pumzi kukatika ndio maana kuangalia mtu kama kafa huangaliwa upumuaji.

Sasa haya maneno ya kusema mtu kafa kwa tatizo la kupumua yanatoka wapi?

Shithole !! Utter Non Sense!!!
 
Wanapoandika sababu ya kifo kuwa ni tatizo la upumuaji au kushindwa kupumua, kitabibu maana yake wanamaanisha kuwa tatizo la mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi ndio chanzo.

Na 'injini' ya mfumo wa hewa huwa ni mapafu, hivyo kwa lugha nyingine ni sawa tu na kusema mapafu yamefeli.

Sababu nyingine za vifo huwa haziwi sababu mama ya mapafu kushindwa kuchakata uingiaji na utokaji wa 'oksijeni' ama 'kabonidayoksaidi'
Mfano: Kupigwa kabali ile ya kisawasawa mpaka miguu inaning'inia juu juu!
 
Amepoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi mwilini.sio kuzibwa pua au kutolewa mapafu.

Imeekaaje hiii.
 
Back
Top Bottom