Kila bibi harusi angetafutwa hivi kungekuwa na ndoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila bibi harusi angetafutwa hivi kungekuwa na ndoa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 9, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,448
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  [h=3]Bikira[/h]

  [​IMG]Mabinti wa kizulu huko Lamontville Afrika kusini wakisubiri kukaguliwa kama bado ni mabikira huku nyuso zikiwa zimepakwa udongo.
  (Picha kwa hisani ya Ellen Emendorp wa NYT)


  Kutokana na desturi za huko Sri Lanka bibi harusi ni lazima athibitishe kwamba ni bikira usiku wa harusi yake.
  Kila bibi harusi hutakiwa kubeba kitambaa cheupe ambacho huwekwa chini wakati wa tendo la ndoa kwa mara ya kwanza usiku wa kwanza kwa maharusi ili kuthibitisha kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
  Kitamba kuwa na damu ni certificate kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
  Na wapo mabibi harusi hukutana na wakati mgumu baada ya kujikuta hawakutoa damu yoyote ingawa ni kweli wao ni mabikira.
  Hii ni kwa sababu wasri Lanka kama jamii zingine duniani bado wanaamini bikira yeyote hutoa damu siku ya kwanza na Yule ambaye hakutoa damu huonekana alijihusisha na ngono kabla.

  Hiki ni kipimo cha kitambaa kuwa na damu ni kipimo potofu kwani na unscientific, wanawake wengi innocent huumizwa na kuonekana hawana quality ya kuitwa bikira wakati ni bikira.
  Ni vizuri watu kujua uhusiano uliopo kati ya kizinda (hymen) na ubikira (virginity)

  Bikira ni nani?
  Bikira ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kufanya mapenzi (penetrative sex) na si lazima awe mwanamke ambaye atatoa damu siku ya kwanza ya tendo la ndoa.
  Ni vizuri kufahamu kwamba asilimia 20% - 25% ya mabikira huwa hawatoi damu yoyote kutokana na muundo wa kizinda (hymen)
  Wakati mwingine kizinda huondolewa kwa kufanya mazoezi mazito, kupanda baiskeli, kukwea miti na ifahamike kwamba kufanya mazoezi hakuwezi kuondoa ubikira.

  Kizinda ni nini?
  Kizinda ni ngozi nyembamba sana (membrane) ambayo huziba entrance kwenye uke.
  Ina matundu ambayo hutofautiana kwa size ambapo damu ya mwezi kwa mwanamke huweza kupita kila mwezi.

  Kuna aina Nne za vizinda
  1. Kizinda cha kawaida (normal hymen),
  2. Kizinda kisicho na tundu lolote [huhitaji surgery wakati mwingine] (Imperforated hymen),
  3. Kizinda chenye tundu dogo sana (Microperforated hymen)
  4. Kizinda chenye tishu za ziada na kufanya matundu mawili (septate Hymen)

  Bado haijajulikana kazi ya kizinda ni nini, kwani baada ya sex mara ya kwanza huchanika na kuachana na kubaki historia.

  Kizinda kiligunduliwa mwaka 1544 na Daktari wa kiarabu Ibn Sinna hata hivyo kufika karne ya 16 watu walikuwa wana imani potofu kwamba kizinda ni ugonjwa na dawa yake ilikuwa ni sex inayofuatana na mwanamke kuolewa.

  Kutokuwa na kizinda au kutokutoa damu siku ya kwanza ya sex si evidence kwamba mwanamke si bikira wapo wanazaliwa hawana wengine nyembamba sana na wengine huweza kutoka kutokana na aina ya mazoezi au accidentally.
  Damu ambayo hutoka siku ya kwanza ya sex ni kidogo sana linaweza kuwa tone hakuna mwanamke amewahi kutoa damu na kulazwa au kuhatarisha maisha yake kwa sex mara ya kwanza.
  Pia ifahamike kwamba mwanamke huweza kujisikia maumivu kidogo au discomfort wakati wa tendo la ndoa.
  Hata hivyo maumivu mengi huhusiana na woga na ignorance (knoweledge is power), wakati mwanamke anakuwa na hofu, woga wakati wa tendo la ndoa misuli ya uke hukaza na uke huwa tight na mwembamba na wakati mwingine hushindwa kutoa lubricants kwenye uke kutokana kuwa na hofu na matokeo yake ni kusikia maumivu wakati wa penetration.
  Pia inawezekana mwanaume hakumuandaa vya kutosha na pia inawezekana wakati wa kumuandaa mwanamke mwenyewe hakuwa relaxed na kuwa tayari kupokea tendo zuri la sex akihofia kuumizwa.

  Je, mwanamke kutunza bikira hadi wakati wa kuolewa kuna heshima au fahari yoyote?

  Kwa nini suala la kuwa bikira kwa wanaume katika jamii zote linakuwa halina uzito bali wanawake tu?

  Je, wakati wa kuoa au kuolewa karne hii ya 21 suala la bikira ni muhimu kuzingatiwa?

   
 2. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Hakika kama tungelikuwa tunaangalia vigezo vya ubikira wengi wasingeolewa wala kuoa,hivyo vitu sa hivi ni historia tu,
   
 3. The great R

  The great R Senior Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanaume wenyewe wanataka mwenye maujuzi yake ampe raha,nani anataka bikra waanze kufundishana.
  lala hivi,panua mguu,oo shuka tubadili style ya nini hayo. Mtu anachukua kitu roho inapenda jamani.
  Ila kwa wale wanaoweza wanachkua mabikra,nae akishajua mchezo ataanza kuangaza wakumfikisha zaidi yako,hapo sasa kasheshe ndio inaanza.
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ina tegemea, unaweza ukatolewa bikira na akakuoa huyohuyo mwanaume wako, na bikira sio kipimo cha ustaarabu wa msichana
   
 5. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa Tanzania, ubikira ni ancient history. Kama katoto ka darasa la nne amabacho hata hakijitambui, tayari kana boyfriend na kanapiga mzigo unadhani kuna chochote hapo?
   
 6. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Je bikira (celibacy) ya mwanamme ni muhimu pia katika ndoa?
  kama ni hivyo, yenyewe inapimika kivipi??
   
 7. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mmhh umetoa shule ya ngv
   
Loading...