Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,272
- 23,046
Huu ni wendawazimu. Ingekuwa hivi kule Magerezani kusingekuwa na wafungwa hata mmoja. Wote wangekuwa wameomba msamaha na wakasamehewa.
Wanasiasa wezi huwa wanaamini wao si Watanzania wa kawaida. Huamini wao ni watu special so wanahitaji special treatment. Huku ni kuwatusi Watanzania.
Kauli za kusema wasamehewe, Rais aanze upya si kauli za waliotendwa. Ni kauli za waliotenda Uovu. Na kila aliyeishi kwa upanga basi afe kwa Upanga.
Wananchi wameteseka sana na baadhi ya wahuni wa kisiasa. Hawa wamenyanyasa sana wananchi, wamewatesa, wameiba mali ya umma, wamejinufaisha wao binafsi. Kwa kutumia mwamvuli wa Chama au Serikali.
Mimi nasema wakutwe na kitu. Sabaya awe ni mmoja wao si mfano wao. Kila mmoja awajibishwe. Waliotendewa hayo waende kushtaki na si kulalamika tu kwenye mitaa. Waende kushtaki.