Kila aliyemchagua Kikwete sasa ametambua kuwa ni miongoni mwa waiolaaniwa nchini.

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,732
Hakuna sehemu nchini humu ambapo wananchi wanafurahia maisha. Leo hii mtu angeangalia channel 10 hadi mda huu zinaoneshwa picha za walioumia kutokana na maji yalichafuliwa na Mgodi wa Mara, wananchi wanaonesha ngozi zao zilivyobabuka lakini hakuna anayewasikiliza hata kidogo . Mwananchi mmoja wa Nyamongo aitwaye Omari Bina anasisitiza kuwa Manager mmoja aliyekuja na kuwa anaongoza mgodi wa Barrick aliyemtaja kwa jina la Mr. Jeff aliwaambia kuwa waache kelele maana yeye anamuhonga Rais sembuse Ofisi ya kijiji.

Wengine kama bwana Mseti anasema hakuna kiongozi yeyote aliyewasaidia. Viongozi wengi sana wameenda pale hadi Rais akaona na ngozi za watu waliochubuka na kama angesogea karibu angesikia harufu za watu wanaumia na vidonda lakini hakuna kilichofanyika. Tume iliundwa na mkemia mkuu alishiriki ambapo damu zao zilichukuliwa na maji vikaenda kupimwa lakini hadi muda wa miaka miwili hakuna majibu. Serikali inajali mgodi kuliko wananchi. Hata kanda maalum iliyopelekwa Tarime kule si kwa wananchi bali ni kulinda mgodi.

Cha ajabu taarifa inaendelea kutolewa na uongozi wa kijiji kuwa watumie tu hayo maji hayana shida wahote na kunywa. Matokeo yake mwananchi mmoja anasema ni lengo la Serikali ya kikwete na wazungu wananchi wafe ili wachukue ardhi kabisa. Wananchi wanaomba walau tamko kuwa yale maji yana nini? Ni vipimo gani vinamaliza miaka miwili bila majibu. Mr Jeff wa Barrick anasema ameshamuhonga Rais Ikulu, sasa diwani na VEO watawafanya nini? Bwana Andrew Thomas wa Tarime anasema hata pale baada ya mgodi kukubali kuwa watawapeleka walioathirika hospitali. Mtanzania mwenzao kiongozi akasema maji ni salama hivyo hakuna kilichofanyika.

Hii inatisha, inasemekana kamati ya bunge ilitoa mapendekezo kuwa waathirika wapatiwe huduma haraka iwezekanavyo, lakini hakuna kilichofanyika tu, bunge nao wakaonekana wasanii tu, wanasubiri 90 milioni wakanunue magari.

Ukienda Babati kwenye nyumba ya wazee nako ufisadi, mwenye dhamana ya kuwatunza anachakachua bajeti na kusema kuwa serikali haitoi chochote na badala yake wazee ambao hawana meno wanalishwa makande na maharage mabichi wamechoka na wanasema serikali haiwajali. Ukiangalia nyumba hizo wanazoishi zinanyufa kibao lakini hakuna matengenezo. Kisingizio ni kuwa eti serikali haina Tsh. 3,000,000/= kwa mwezi kuwasaidia wazee!!! Mie nimeshashangaa vya kutosha.

Wananchi walioweka tiki kwenye picha ya kikwete wakati wa uchaguzi na viongozi wengine wa ccm wanajisikia vibaya sana. Kila tunapoangalia taarifa za habari kupitia chanel mbalimbali hapa nchini na kuona jinsi watanzania wanavyoteseka mmaeneo mablimbali, wanaona aibu wanainama chini, pia utasikia wakisema "kwa kweli kikwete katuangusha", "yaani hii ni aibu". Na hii ndo tujue kwamba JK hawezi fanya kitu maana hata yule Bwana Jeff wa Barrick amesema yeye anahonga Ikulu kwa pesident hicyo matatizo yao wapeleke Ikulu!!!

My Take;

Jamani tufanye lolote tuwezalo basi tu angalau wananchi waelewe, loh!!mie naanza kuona aibu kujitangaza kuwa mie mtanzania.Sijui niende wapi. Nionavyo mimi nafasi ya President Tanzania iko vacant, aliyeko anakaimu, hawezi kusema lolote maana Rais hayupo!!!sijui uchaguzi lini??!!



Anayesema sisi tunaoanika maovu hatuna lolote, tuandamane tuhesabu siku, Mungu kaiona dhamira yake lakini haitachukua muda pasipo wewe usiyeona kuonja uchungu huu kwa vitendo.
 
mimi nilishajiandaa:

kwa kumpigia Dr. Slaa na Chadema, nilitarajia Tanzania mpya yenye mkakati mpya wa kiuchumi wa kumuwezesha Mtanzania. Kwa ujumla nilitarajia maisha na changamoto bora kutoka kwa Rais wangu Dr. W.P. Slaa.

Lakini pia nilikuwa nimejiandaa kwa hali ngumu kama Kikwete na CCM yake wangerejea madarakani: Sishangai mimi kuona sukari inauzwa Tshs. 2500. nilijua, na ni hali niliyoitarajia. sijutii wala kujilaumu.

hao waliotarajia Kigoma kugeuzwa Dubai ndo watajuta sasa na ndoto zao za linacha.

hata bajaj 400 imeshindikana
 
2015 ni mbali sana lakini hata ikifika utarajie kweli kitu kutoka kwa NEC na mafisadi kama hamna dhamira ya kweli kutoka kwenye system iliyopo?

Hatimaye naona mwanga...................wananchi wameanza kuelewa ili waseme kwa nguvu hatuwataki. tunataka maisha bora yanayoendana na rasilimali zetu nyingi.
 
Jk ni kiongozi mzuri sana kwenye media..ana sura nzuri kwenye magazeti na kalenda as well...lakini kiutendaji hayuko competent...hafai kwa karne hii yenye changamoto nyingi!
 
mimi nilishajiandaa:

kwa kumpigia Dr. Slaa na Chadema, nilitarajia Tanzania mpya yenye mkakati mpya wa kiuchumi wa kumuwezesha Mtanzania. Kwa ujumla nilitarajia maisha na changamoto bora kutoka kwa Rais wangu Dr. W.P. Slaa.

Lakini pia nilikuwa nimejiandaa kwa hali ngumu kama Kikwete na CCM yake wangerejea madarakani: Sishangai mimi kuona sukari inauzwa Tshs. 2500. nilijua, na ni hali niliyoitarajia. sijutii wala kujilaumu.

hao waliotarajia Kigoma kugeuzwa Dubai ndo watajuta sasa na ndoto zao za linacha.

hata bajaj 400 imeshindikana

Kuna tofauti kubwa kati ya kutegemea mazuri na ukapata mabaya
na
kujiandaa kwa mabaya ambayo yatatokea,ni sawa na kutunza chakula wakati wa masika kikufae wakati wa kiangazi

Life halikamatiki mtaani saivi
 
Kwa ujumla wetu Tumuombe MMUNGU Kwa kusali na kufunga;
Kwanza atusamehe kwa uovu wote unaofanyika hapa kwetu!

Atusamehe hata kwa woga na upofu tulio nao.

Atusamehe hata pale tunapo ona kwamba ufisadi na rushwa si uovu bali ni HAKI.

Asamehe UOVU WOOOTE.

Kisha tumuombe airudishe nchi kwenye Mamlaka yenye hofu kwake na mikono ya wazalendo,
Pia aikabidhi nchi kwa viongozi wazalendo na wenye uchungu na wananchi.

HAKIKA MUNGU WETU NI WA HAKI ATAJIBU OMBI LETU ANAVYO PENDA.
 
hamna jipya kaandamaneni mhesabu siku:rain:

Tunaelewa huwezi kumsaliti mmeo. Jitahidi uangalie picha za Watanzania wenzio walivyoungua. Ndo utajua kuwa huyo mmeo unayemtetea ni mtenda dhambi wa kila aina. Tuombe damu inayoungua tarime mara iirudie familia yako tuone utasema nini. Mchakato unaanza.
 
Tutafute solution ya matatizo yetu Tanzania lakini tusitegemee kuwa Chadema wanauwezo au kuna kiongozi yoyote ndani ya chadema mwenye akili timamu
 
Whomever comes along, tutatue matatizo haya mbona mhusika mkuu anakuwa kama karogwa???
 
image002.jpg
 
Hawa wazee ndo wagumu kubadilika,ona jimbo la tarime wamerudisha tena Ccm,angalau yule wa chadema alikua akiwatetea bungeni mpaka tume ikaundwa kuchunguza hayo maji huyu Nyangwine wao ndo kimya
 
Kikwete ana miaka mingine mitano, kama itaisha, ya kufanya adventure. Kwake yeye urais ni adventure.
 
Najua tunao few ignorant people in Tanzania na a lot of uneducated Tanzanians. CCM haikushinda uchaguzi 2010. Hawa tunawona hapa chini sijui tuseme nini wako tayari kulipwa pesa zao wenyewe ili wateswe tena na tena. Kama kuna mtu anawafahamu tunaomba tuwatafute na kupata video clips sasa, tupate feedbacks za maisha yao, tuzipost humu JF

 
Last edited by a moderator:
Picha zote ziko kwenye maktaba ya channel ten ,na kule LEAT hapo Dar we fuatilia tu, waambie wakupe video clips za kipindi cha pambanua wiki iliyopita utaziona tu. Japo hiyo ch 10 inasemekana ya RA lakini kuna wazalendo watakupa tu mh. NIWEZE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom