Kila aliyehusika na kupotea kwa Ben Saanane na Azori Gwanda laana imtafune yeye na kizazi chake

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Hili wala hatutaki kukificha kwa sababu kila siku tukiwakumbuka ndugu zetu hawa tunabubujikwa machozi yaliyojaa maumivu makali na huenda hata damu hutokea kwenye machozi haya. Tunajua waliohusika na kuwapoteza hawa watu ni wanadamu na wala si wanyama, Laana ya mwenyezi Mungu iwatafune milele na ikiwezekana Mungu awape adhabu kali humu duniani na akhera, apukutishe pamoja na vizazi vyao.

Kila mtu ukikaa unajiuliza kosa la la Ben na Azory ni lipi kiasi cha kuwatowesha kabisa wakaacha familia zao? Kwani sheria za nchi hazipo mpaka kuwatowesha? Bado narudia kwa maumivu makali tena ikiwa wote Azory na Ben familia zao nimebahatika kuzitembelea zinatia huruma na unaweza kuzungumza na wazazi wa hao vijana ukajikuta unalia uwenyewe,Laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie mafedhuli wote waliohusika na kutoweka kwa vijana wote, ikiwezekana wapoteze na wao na familia zao.

Uwe kaburini,uwe duniani Mungu akuadhibu kwa matendo haya na tena ulaaniwe. Hatuwezi kubaki kulia kila siku kwa sababu ya mafedhuli machache ambayo na yenyewe ni mizigo ya kesho kama si leo.
 
Duh..Mbona una hasira sana mkuu? Pole sana na watalipwa stahiki zao kama waligusa damu yayeyote kati yao na ikiwa hakua na hatia.
 
we unamjuwa vizuri mbowe au unaongelea ushabiki? hivi ukijakutolwa ushahidi utafichawapi sura yako maana unamtetea kama unamjua kiundani saaaanaaaaaaaaa
Hivi hata kama ingekua kweli, kuchoma kituo cha mafuta ni la kutisha kiasi kwamba mtu aitwe Gaidi? Hivyo vituo vilichomwa? Ushahidi ingekuwepo kama tukio lingefanyika.

Magaidi wako Afughanstan huko na Lebanon na siyo Tanzania. Huku ni maugomvi tu ya kisiasa
 
Hivi hata kama ingekua kweli, kuchoma kituo cha mafuta ni la kutisha kiasi kwamba mtu aitwe Gaidi? Hivyo vituo vilichomwa? Ushahidi ingekuwepo kama tukio lingefanyika.

Magaidi wako Afughanstan huko na Lebanon na siyo Tanzania. Huku ni maugomvi tu ya kisiasa
Ndugu unafurahisha sana yaani ungefurahi kama wangechoma kabisa vituo ili uwepo ushahidi? you are not serious na ujue alikuwa anafadhiri ugaidi uwe unaelewa pia
 
Back
Top Bottom