kila akimuona mganga wake analia machozi kama kafiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kila akimuona mganga wake analia machozi kama kafiwa!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Midavudavu, Feb 6, 2012.

 1. M

  Midavudavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamaa mmoja alikuwa na tabia ya kutembea na watoto wa shule. Ikagundulika kuwa amempa mimba mwanafunzi. Akafikishwa mahakamani. Baada ya kuona kafikishwa mahakamani akaenda kwa mganga kuloga ili amgeuza kuwa mwanamke. Mganga akaifanya kazi yake barabara. Ilipofika siku ya kesi yake jamaa akamwambia hakimu kuwa yeye ni mwanamke na hivyo hahusiki na mimba ya huyo mwanafunzi. Hakimu akaamuru wazee wa baraza na daktari wakathibitishe hilo analosema mshtakiwa. Kweli ilithibitika kuwa jamaa ni mwanamke na hivyo hakimu akamuachia huru. Sasa ikawa kimbembe kwani alipokwenda kwa mganga wake ili ambadilishe ili awe mwanamme tena mganga akamwambia haiwezekani kwani via vya uzazi alivyomuwekea vilikuwa nya mke wake mdogo na bahati mbaya ameshafariki na amezikwa navyo. Jamaa kambembeleza sana mganga amrejeshee vitu vyake lakini bado mganga akawa anasisitiza tu kuwa alipaswa kuja na vile vitu kabla mkewe hajafariki. Ila kwa kumsaidia tu akamwambia aje aishii na yeye achukue nafasi ya mke mdogo aliyefariki. Jamaa akaja mbogo haiwezekani hilo, mganga akasisitiza tena afanye hivyo haraka kwani anakaribia kujifungua kwa kuwa huyo mkewe ambaye ni marehemu alikuwa mjamzito. Malimwengu haya jamani, jamaa analia kila akimuona huyo mganga na anangoja kujifungua ili amkabidhi mganga mwanae. je, kwa mwanaume uchungu wa kuzaa na kufungwa upi una nafuu?
   
 2. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Copy and paste, halafu ni ya zamani kwelikweli.
   
Loading...