Kila akikutana na mpenzi wake wa zamani analia

F9T

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,674
4,942
Wa salaam wakuu.

Nina rafik yangu ambaye mwishon mwa mwaka jana 2015 kuna girl walianza nae uhusiano, kwa madai ya jamaa ni kuwa wanapendana sana na huyu girl.

Sasa kilichonileta jukwaan ni kuwa jamaa anadai huyu girl wake huwa anakosa amani hadi kupelekea kulia kila wakikutana na x boyfrnd wake, jamaa anadai kitendo hicho kimekuwa kikimsononesha sana kwan alikuwa anampango wa kumwoa huyu girl lkn sasa anakata tamaa, kwan kitendo hiki kimekuwa kikijirudia mara kwa mara, anasema kila akimwuliza girl sababu ya kulia kila akikutana na x boyfrnd, bint anamjibu kuwa "basi tu, lakin haya yote ni mapto".

Nimemshaur ajaribu kumweka girl mazingira ya mbal na huyo x boyfrnd wake, jamaa anadai kuwa inamuwia vgumu kwan ni majiran sana kiasi kwamba hawawez kupita wiki bila ya kuonana yaan huyu girl na x boy wake.

Wakuu naomben ushaur wenu ili 2weze kumpatia huyu rafki yangu yaan anaumia sana koz anampenda sana girl.
 
Last edited by a moderator:
Mwili uko kwa rafiki yako halafu akili(moyo) ziko kwa x wake.

Swali hivi kinachoendesha mapenzi ni mwili au akili(moyo).
 
Muambie rafiki yako msome kwanza manake elimu dunia ni muhimu sana. Mkikua ndio mjiingize kwenye mapenzi. Kuna mbunge aliimba mapenzi na shule ni mlenda na pilau.
 
Anakumbuka show ya x wake ilivyokua matata kulinganisha na ya rafiki yako
 
Analia kivipi? kuna kulia kwa ghadhab na kuna kulia kwa donge au mahabat...ukiweza kujua hilo basi utajua hatua gani uchukue.
 
wakati mwingine mapenzi ukiyaendekeza utakuwa mtumwa na mfungwa katika jela ambayo haina msamaha wala huruma. Mapito ni mengi na mengi huumiza sana lakini unadhani atalia mpaka lini? Mwambie aamke katika usingizi, usiote muda huu bali asimame na aianze upya safari ya mapenzi.
 
Back
Top Bottom