Kikwete Yupo Addis Ababa, AU Hajue Yeye Next? Kikao Kuhusu JK/Pinda Kinafanyika Lini?

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
116
Kikwete na viongozi wa Afrika hatimae wameenda kumzungumzia Gbgbo wa Ivory Coast. Raisi aliejipatia ushindi kupitia Tume ya Uongo kama hiyo ya Kikwete. Kikwete na wenzie kama Mugabe na Museven na pia Gaddafi wote wapo Addis Ababa, Ethiopia kutatua swala la Gbagbo na imeonekana mpaka sasa kuna mgawanyiko ndani ya Africa Union. Hivi Maraisi fake wa Africa kwanini wasijiondoe madarakani mpaka vikao vya kuwatishia kwa jeshi au mpaka mapinduzi ya wananchi yaje? Hii demokrasia ya Africa kwanini inakumbwa na Blockage kila Nchi? Hivi leo wanamzungumzia Gbagbo wakati Egypt wanamfukuza mzee mshauri wa AU. Hii kweli ni Irony ya aina yake kwamba madikteta wanafanya vikao wakati nchi zao wananchi hawawataki. Kuna haja ya kuwa na African Union? Ingekuwa vizuri AU iundwe endapo kuna demokrasia ya kweli Africa yote Ukichunguza viongozi wote na ndege zao zote na misafara yao yote huko Addis Ababa weekend hii utaona kwanini Wafrika hawataki? Wanaishi na kusafiri kama CEO's wa Makampuni ya High Grade Performances. Sasa tunaona kama watatoa statement zozote kuhusu Mapinduzi ya Tunisia na Egypt? Kwani si yanakuja katika zao tukianzia Tanzania...Bara la Africa linaongoza kwa vikao vya Wizi wa Demokrasia kulinganisha na Mabara yote Duniani. Solution sio vikao AU ni: Ajira kwa wananchi wao, Wizi na Rushwa kumalizika, Constitution zinazolinda Freedom of Speech and Express na kikubwa ni Rights of the people.

"Kikwete angekuwa mmoja wao Kiongozi kutokwenda Addis Ababa"

U.N. chief urges Africa to be firm against Gbagbo | News by Country | Reuters
UPDATE 1-Ivory Coast's Gbagbo is not president, ECOWAS says | News by Country | Reuters
Mubarak meets army as Obama urges reform | Reuters
 
Kwa kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hivi sasa ni mfumo unaofuatwa kote duniani basi vyama vya upinzani na asasi za kiraia havina budi kuomba nafasi zao katika taasisi mbalimbali za kimataifa kama EAC, AU na UN ambako maamuzi mengi hufanyika yenye maslahi makubwa kwa vyama tawala tu.

Vyama tawala visihodhi taasisi za kimataifa kunakofanyika maamuzi yenye maslahi kwa washikadau wenye itikadi tofauti nao kisiasa.
 
Kwa kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hivi sasa ni mfumo unaofuatwa kote duniani basi vyama vya upinzani na asasi za kiraia havina budi kuomba nafasi zao katika taasisi mbalimbali za kimataifa kama EAC, AU na UN ambako maamuzi mengi hufanyika yenye maslahi makubwa kwa vyama tawala tu.

Vyama tawala visihodhi taasisi za kimataifa kunakofanyika maamuzi yenye maslahi kwa washikadau wenye itikadi tofauti nao kisiasa.

Naona hii ungeiweka kwenye post yake peke yake ili watu waijadili pekee bila kuichanganya na hoja ya JK kuwa Addis
 
Back
Top Bottom