Kikwete,Waziri Mkuu na Said Mwema Bado Hili Mtatujibu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete,Waziri Mkuu na Said Mwema Bado Hili Mtatujibu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josephine, Feb 11, 2011.

 1. Josephine

  Josephine Verified User

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kikwete,Waziri Mkuu,IGP uongozi wenu utaheshimika sana kama utawala wa Sheria utafuatwa.Hatuwezi kuendelea kubebana, kuvumilina ,kwa upendo na Amani kama Haki za Msingi za Mtanzania hazipatikani.

  Kikwete, Viongozi wako hawajaelewa kwamba watanzania wanaonyesha uvumilivu mkubwa sana kwa kupoteza na kunyimwa haki zao za Msingi.

  Labda tu nisema wapo watu ambao kwa namna moja ama nyingine watakapo hitajika kutoa taarifa watazitoa bila uwoga na kwa uwazi. kinachotufanya tuvumilie haya,ni kwasababu tunajua ni harakati za kile tunachokitafuta ambacho ni Uhuru wa Kweli,na si Uhuru Tulionao sasa.

  Kwa Taarifa za Waziri Mkuu na Viongozi wote ambao bado wanafanya ushabikii juu ya swala la kupoteza maisha ya watu kwa kupigwa Risasi na polisi hili siku yaja Hukumu yenu itaanikwa.Hakuna anayeleta Mfarakano Bali ni ukosefu wenu wa Busara na kutojiamini katika Lile Mnalolifanya.

  IGP umekuwa ni mtu kigeugeu unaposhirikishwa mambo na taarifa nyingi umezipata na kushiriki mazungumzo mengi kwa njia ya simu hasa ya uvunjifu wa haki za msingi,Na hata swala la Arusha ukweli unahujua na hili hutalikwepa.

  View attachment 22718
  Hiki ni Chumba ulichoamuru wewe au yeyote aliyehusika niwekwe, chumba hiki hakikuwa Lock up,hivyo niliweza kupiga picha na kufuatilia matukio yote.IGP nilikuharifu hili kupitia msaidizi wako.
  View attachment 22719

  Kikwete na IGP hawa ni baadhi ya vijana wenu ambao kwa namna moja au nyingine kama Mahakama ambayo itakuwatayari kutenda haki ili wale walioumizwa na kupata majeraha makubwa hawa ni miongoni mwa mashahidi.Na si hivyo tu bado ushahidi upo na utazidi kutafutwa.

  View attachment 22720

  Huyu ni Muhudumu aliyetuhudumia majeruhi na watu kadhaa kufa mikononi mwake.
  Kama Mnataka Amani ya kweli,kuweni wakweli na tendeni Haki,Amani siyo maneno ni tunda la Haki na Haki zinatolewa.

  View attachment 22721

  Maneno yenu yasiyo na ukweli yanavuruga Amani ndani ya mioyo ya wengi kwani bado wanamajerahaa na maumivu makali.

  Rai yangu kwenu Viongozi kuweni wakweli kwani Ukweli upo na siku itafika na kuuweka Hadharani.

  Vitisho vyenu na majigambo hayatalisaidia Taifa hili hata kwa wale wanaochangia hapa,Taifa litajengwa na wale walio wawazi na wakweli.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wewe Josephine mapenzi ndio yanakusababishia kovu. Endelea kuvumilia tu kwa sababu umejitakia wenyewe. Kama unapenda kuendesha hoja ungeendesha hoja hizo na IGP kabla ya kukiuka AMRI halali.
  Heri wewe umepata kikovu, watoto wa wenzako wamepoteza maisha kwa jinsi mlivyowarubuni! Mtajibu kwa Mungu wewe mpenzi wako na wenzenu.
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Are you serious? Amri halali ni ya IGP kutengua taratibu za mtiririko wa majukumu. Mh. hoja iliyopo ni uhalifu wa dhahiri kwa raia wasiokuwa na hatia na ushadi upo. Kama unanaghaghania AMRI halali ni kwa sababu AMRI batili ipo. Na ya IGP siku ile ilikuwa batili. Kwa faida yako amri halali inazingatia mantiki ya kuitoa na madhara yanoweza kutokea.

  Uliyetoa mada kama ilivyoletwa/andikwa naomba ufanye kila njia uandike artcles kwenye mitandao hata magazetini kwa sababu IGP hakufanya kitu hata ulipomshirikisha. Halafu wote uliowataja ni wapuuzi fulani ambao wanaficha vichwa kama mbuni wakidhani hawaonekani. Hiyo ni fursa nzuri ya kutenganisha kichwa na kiwiliwili. NaKupongeza sana mchango wako MUNGU AKUBARIKI. Kuna kamsemo kanasema when the success is just at the corner you will be confronted heavily; but it is the time you do not need to give up but fight on. Learn from TAHRIR SQUARE.
   
 4. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  He! Mapenzi kivipi?
  IGP na Josephine wanagombea Mume au?
  Sijakuelewa !
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mama wetu wa kwanza,

  Nianze kwa kuziombea kwa Mungu roho za mashujaa wetu, na pia kukupa pole kwa maumivu na majeraha makubwa (kama tulivyoona Jan 5 na kwenye picha hapo juu) yaliyosababishwa na utawala wa kidikteta unaoendelea na kushamiri Tanzania.

  Nina matumaini makubwa kwamba uhuru wa kweli uko mlangoni..Movement ukombozi dhidi ya uongozi wa mabavu ilianzia Arusha, then Tunasia na Misri etc. Sasa inarudia Tanzania ili kukamilisha ukombozi wa kweli.

  Tumenyonywa, tumenyanyaswa na kudharauliwa vya kutosha na mafisadi, madikteta na wakoloni weusi nchini Tanzania.
  Their days are numbered.
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Pinda sasa amegeuka wakala wa mashetani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  mimba yako ilitunga kwenye mbio za mwenge, ukanywesha maji ya kijani na utakufa tarehe 5/2
   
 8. Josephine

  Josephine Verified User

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Asante Nimefurahi hata wewe umesoma.
   
Loading...