Kikwete: Watu wanamiliki viwanda vya kutunga Uongo Tanzania!

cqapa kazi jk. chama kisichopenda maendeleo ni CHADEMA, JK weka wazi, na kiwanda cha uongo ni gazeti la TANZANIA DAIMA.
Tukisema mmeolewa na CCM mtasema tuna kiwanda cha kutunga uongo? Kama na wewe unaunga mkono mipasho hii ya JK basi Tanzania cha cha Upinzani Chadema pekee
 
Sishangai maneno aliyoyasema mkuu wa kaya, napata shida kwamba katika yote aliyosema Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeona ya ku-amplify ni hayo ya mipasho.....

Vipi kama ufafanuzi ungejikita katika faida itakayopatikana pindi daraja likikamilika...kwa mfano foleni itapungua kwa kiwango gani pale ferry.....mkazi wa kigamboni atatumia muda kiasi gani kufika mjini badala ya sasa......NSSF itaingiza kiasi gani kwa mwaka kama marejesho ya mkopo wao....

Hivi kweli balozi Sefue nae anamwonea haya Salva Rweyemamu??? Je si jukumu la wasaidizi kumsaidia kiongozi hata pale anapochemsha????
Wajifunze kwa Kibaki wa Kenya ambaye kazungukwa na vichwa vya ukweli sio vichwa maji kama wa Magogoni....

Aaaaagghhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Hivi alivyoahidi meli kule ziwa Nyasa, hakuwa na taarifa kuwa ni ziwa la Malawi?
:becky:

kule Tanga aliahidi kubadilisha Tanga kuwa Mji mkuu wa Viwanda Tanzania, cha ajabu mpaka sasa hakuna hata kiwanda kimoja kilicho fufuliwa achilia mbali kujengwa na vilivupo vinazidi kufa

 
“Watu wana viwanda vya kuzalisha uongo. Wanashinda wanasambaza uongo kwenye mitandao, kila mahali. Wamepata hata kusemakuwa mimi nimemuuzia George Bush eneo la Kigamboni. Bush aje kufanya nini Kigamboni?''

Kwa hii kauli ni ushahidi tosha JK huwa anapita humu Jamvini. Hata hivyo kwa jinsi alivyoitoa hiyo kauli inawezekana ikawa kweli.
 
Juzi juzi Morogoro alisema anadata za watorosha nyara na amepewa kitambulisha chekundu cha jamaa wa usalama wa taifa akatoe photocopy kumbe ni fafa alionyesha driving licence ya zamani .


Kama hadithi yake ya La Cairo Hotel...
 
Hii Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inafanya nini pale Ikulu? Hiyo nhotuba yote si itatolewa yote na TBCCCM kwenye taarifa ya habari na kesho kuandikwa kwenye HabariLeo, Uhuru na Daily News? Kulikuwa na haja ya kuitoa kama Press Release? So what?
 
Sishangai maneno aliyoyasema mkuu wa kaya, napata shida kwamba katika yote aliyosema Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeona ya ku-amplify ni hayo ya mipasho.....

Vipi kama ufafanuzi ungejikita katika faida itakayopatikana pindi daraja likikamilika...kwa mfano foleni itapungua kwa kiwango gani pale ferry.....mkazi wa kigamboni ataumia muda kiasi gani kufika mjini badala ya sasa......NSSF itaingiza kiasi gani kwa mwaka kama marejesho ya mkopo wao....

Hivi kweli balozi Sefue nae anamwonea haya Salva Rweyemamu??? Je si jukumu la wasaidizi kumsaidia kiongozi hata pale anapochemsha????
Wajifunze kwa Kibaki wa Kenya ambaye kazungukwa na vichwa vya ukweli sio vichwa maji kama wa Magogoni....

Aaaaagghhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Like father like son, and again, Birds with same feathers fly together.

Kwa ufupi, Kurugenzi yote imeshaambukizwa mipasho na baba yao
 
Hizi hela zinazojenga hili daraja ni kodi za watanzania, uongozi wa magamba walishindwa kusimamia vizuri fedha zetu.
 
Katika hili Dr wa ukweli anahusika vipi? taja uongo ambao Dr. wa ukweli amaewahi kuzalisha
Ikiwa mpaka sasa hivi haujaweza kutofautisha anapoongopa au kuzungumza ukweli yule babu,sina cha kukusaidia mtanzania mwenzangu we endelea kula matango pori.
 
Katika hili Dr wa ukweli anahusika vipi? taja uongo ambao Dr. wa ukweli amaewahi kuzalisha

mkuu Makyomwango, kuna Mingoi na Rejao, nahisi wameathirika na SLAAPHOBIA,hawawezi changia mada bila kumtaja tena kwa kumuogopa Dr.Slaa, nawaonea huruma sana. tena kama Mingoi na jazba zake wamuangalie sana 2015 ataweza kujinyonga
 
Last edited by a moderator:
1.Shutuma za kutaka kuuawa
2.Uongo wa kuingizwa makontena ya kura
3.Kuibiwa kura katika uchaguzi 2010 uku akijua fika maeneo mengi hakufika katika kampeni na wala hawakusimamisha hata mjumbe wa nyumba 10
4.CCM wameingiza silaha za kivita kuikabili CDM
5.Kuwasawishi watu kutomtambua prezidaa wakati anamzimikia kishenzi na alienda kugonganae chai ya jioni ikulu na akaomba take away ya Josephine


Mwana Mpotevu, bado unataka nyongeza?

Watu kama wewe napata shida sana kuamin kama jamaa hawapigi mashine! Mbona unanyevukwa namna hiyo?
 
Rais amepata kizunguzungu gani? Kama yeye kasema hayo basi naona Rais wetu ana mawazo ya masafa mafupi zaidi kuliko nilivyomdhania. Hayo ni maneno ya kuwaambia wananchi kweli? You need to grow up Mr. President!
 
sijaona cha ajabu alicho ongea jk, kaongea ukweli mtupu.
Hapahapa jamvini kuna watu ni mstari wa mbele kupinga na kukejeli lila serekali inacho fanya hatakama ni kizuri.
Kila mtu ana mazuri na madhaifu yake, tusifie panapo stahili na kukosoa panapo stahili.
 
Kama ni kitendawili hebu tukitegue. Hebu tujiulize CCM siku zote wamekuwa wakidai CDM ni chama kinachofanya vurugu kwenye mikutano yao.

Safari hii kule Nyololo, Iringa, kwenye shughuli za Chadema za kufungua tawi lao, picha zimewaumbua,zikionyesha polisi wakimuua mwanahabari, sasa kwa mazingira hayo ni nani mwenye kiwanda cha uongo, ni CCM au CDM?

Mfano wa pili, Chadema siku zote wamekuwa wakisema kuwa umasikini wa wa-TZ, unatokana na ufisadi wa kutisha wa viongozi wetu, lakini viongozi wetu wamekuwa wakilikanusha hilo.

Lakini mwezi wa 6 mwaka huu, benki kuu ya Uswsi ilitangaza rasmi kuwa, kwenye mabenki ya nchini mwao, vigogo 6 toka nchini mwetu, wameficha shilingi bilioni 315, jambo ambalo halijawahi kukanushwa na kiongozi yeyote wa nchi hii. Hata hivyo hadi leo wameshikwa na kigugumizi, hawataki kuwataja watu hao, walioficha pesa hizo, wala kuwachukulia hatua za kisheria.

Katika mazingira hayo ni nani mwenye mtambo wa uongo, ni CCM au ni CDM?

TAFAKARI, UTAPATA JIBU, HALAFU CHUKUA HATUA!!
 
Back
Top Bottom