Kikwete: Watu wanamiliki viwanda vya kutunga Uongo Tanzania!

Muongo number moja anaeshikilia rekodi hiyo ni Dr Slaa,huyu babu anakipaji cha hali ya juu na amekatika mshipa wa noma.Anaweza kuzusha lolote kwa maslahi yake binafsi hafai,hafai wakuogopwa kama ukoma.

Kamfundisha hawara yake. Hapo patamu huku mshkaji huku demu. Chezea wewe familia ya waongo.
 
Jk bana,kwa mipasho hajambo! Kwa hiyo na hii mipasho ni press release kutoka ikulu!!
 
Daraja hilo la Kigamboni ambalo wazo la kujengwa kwake lilibuniwa kwa mara ya kwanza zaidi ya miaka 30, tokea mwaka 1978, wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, linajengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 214.6 na litakuwatayari katika muda wa miezi 36 ijayo, ingawa muda huo unaweza kupungua na kubakiamiezi 30.

yeah hadi msahihishwe!! mlitaka kujifanya kana kwamba mmebuni wazo zima nyinyi na tuwashukuru! miaka 30 iliyopita? whaaat! Mlitaka kufuta kabisa jina la Nyerere ili mjipe ujiko.. na Stielger's Gorge nayo ije..
 
Muongo number moja anaeshikilia rekodi hiyo ni Dr Slaa,huyu babu anakipaji cha hali ya juu na amekatika mshipa wa noma.Anaweza kuzusha lolote kwa maslahi yake binafsi hafai,hafai wakuogopwa kama ukoma.

atawaumiza sana mwaka huu si unakumbuka uongo wa richmund, Epa n.k
 
siamini kama hayo maneno yanatoka ikulu,very cheap words,yale maneno ya president obama kwa mitt romney yanamfaa pia JK,''he shoot first and aims later''
 
Muongo number moja anaeshikilia rekodi hiyo ni Dr Slaa,huyu babu anakipaji cha hali ya juu na amekatika mshipa wa noma.Anaweza kuzusha lolote kwa maslahi yake binafsi hafai,hafai wakuogopwa kama ukoma.

Nakubaliana na wewe kwa 100%
 
Muongo number moja anaeshikilia rekodi hiyo ni Dr Slaa,huyu babu anakipaji cha hali ya juu na amekatika mshipa wa noma.Anaweza kuzusha lolote kwa maslahi yake binafsi hafai,hafai wakuogopwa kama ukoma.
Uongo gani alioutunga Dr.Slaa ule wa EPA au Richmond?. Kwani ungekaa kimya bila ya kuandika huyo aliyekuazima PC yake utumie mara moja angekutimua?
 
Tupe mifano ya uongo wake walau mitano tu
1.Shutuma za kutaka kuuawa
2.Uongo wa kuingizwa makontena ya kura
3.Kuibiwa kura katika uchaguzi 2010 uku akijua fika maeneo mengi hakufika katika kampeni na wala hawakusimamisha hata mjumbe wa nyumba 10
4.CCM wameingiza silaha za kivita kuikabili CDM
5.Kuwasawishi watu kutomtambua prezidaa wakati anamzimikia kishenzi na alienda kugonganae chai ya jioni ikulu na akaomba take away ya Josephine

Mwana Mpotevu, bado unataka nyongeza?
 
Mfano wa kiwanda cha uongo ni kile chama ambacho mbunge wake wa viti maalum "aliproduce" uongo kuwa waziri fulani amefumaniwa guest house na mkono wake umekatwa kwa panga. Lakini kiwanda hicho cha uongo kilisahau kuwa waziri anaweza kuonyesha mkono wake kuwa haujakatwa na panga.

Kiwanda hicho pia kilishawahi kusema kimeona kontena la silaha na kura za wizi mpakani, ikabainika ni uongo product.

Mfano wa kutopenda maendeleo ni kitendo wa viongozi wa chama fulani kuhamasisha wananchi mkoa wa Tanga kukataa kushiriki katika shughuli za koboresha huduma za afya na kitendo cha chama hicho kusabaisha vurugu zenye lengo la kufanya shughuli ya sensa isifanikiwe...
 
Jk bana,kwa mipasho hajambo! Kwa hiyo na hii mipasho ni press release kutoka ikulu!!
Kwa mipasho huyo jamaa hajambo utadhani Mzee Yusuph vile, huo ni kama wimbo anaanza kuimba huyo subiria muda si mrefu Isha Mashauzi(Nape) atakuja na kiitikio cha huo wimbo. Mungu kawajaalia kwenye suala zima la mipasho.
 
Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali haiwezi kudhulumu wananchi wake na hivyo watu wote ambao wanastahili fidia kutokana na ujenzi wadaraja hilo na mji mpya wa Kigamboni watalipwa haki na stahiki zao.

Hapo kwenye RED, nendeni mkawaulize wale wababu wastaafu wa EAC, Askari waliopigana WWII na wahanga wa GONGO LA MBALI na MBAGALA.
 
Asante prezidaa...hivi wale "magamba" washajiondoa wenyewe!!...aaah...unamjua mmiliki wa "do..once"...au ushakumbuka sababu ya umaskini wetu!?....mshahara nao umepanda kati ya 15%-20%...naskia na waalimu wote washalipwa madeni yao eeh!!...pia tuna "bodaboda" za kupeleka akina mama hospitali...na...pia......
 
Mods tafadhali sana hii thread msiitoe ili tuweze kuidentify aina mpya ya viwanda nchini - viwanda vya uongo...
 
1.Shutuma za kutaka kuuawa
2.Uongo wa kuingizwa makontena ya kura
3.Kuibiwa kura katika uchaguzi 2010 uku akijua fika maeneo mengi hakufika katika kampeni na wala hawakusimamisha hata mjumbe wa nyumba 10
4.CCM wameingiza silaha za kivita kuikabili CDM
5.Kuwasawishi watu kutomtambua prezidaa wakati anamzimikia kishenzi na alienda kugonganae chai ya jioni ikulu na akaomba take away ya Josephine

Mwana Mpotevu, bado unataka nyongeza?

1. Ulitaka mpk auawe ndio uamini?
2. Kama unadhani ule ni uongo, mbona hamkumshtaki?
3. Zilizoibiwa ni kura za Urais, ulitaka afike asimamie mwenyewe?
4. Hilo nalo ni kweli tupu. Na ndio maana wamefyata. Ya uongo kama yale ya Nape tayari yako mahakamani
5. Hii ya 5 ni mipasho kama hiyo tulioletewa toka ikulu. Sato Pra-sato!
 
Mfano wa kiwanda cha uongo ni kile chama ambacho mbunge wake wa viti maalum "aliproduce" uongo kuwa waziri fulani amefumaniwa guest house na mkono wake umekatwa kwa panga. Lakini kiwanda hicho cha uongo kilisahau kuwa waziri anaweza kuonyesha mkono wake kuwa haujakatwa na panga.

Kiwanda hicho pia kilishawahi kusema kimeona kontena la silaha na kura za wizi mpakani, ikabainika ni uongo product.

Mfano wa kutopenda maendeleo ni kitendo wa viongozi wa chama fulani kuhamasisha wananchi mkoa wa Tanga kukataa kushiriki katika shughuli za koboresha huduma za afya na kitendo cha chama hicho kusabaisha vurugu zenye lengo la kufanya shughuli ya sensa isifanikiwe...

Woga ni adui mkubwa sana na ni dhambi kubwa sana. kuwa wazi kama una uhakika na hoja yako
 
yeah hadi msahihishwe!! mlitaka kujifanya kana kwamba mmebuni wazo zima nyinyi na tuwashukuru! miaka 30 iliyopita? whaaat! Mlitaka kufuta kabisa jina la Nyerere ili mjipe ujiko.. na Stielger's Gorge nayo ije..
Ahadi na utendaji ni vitu viwili tofauti,hao aliopanganao Nyerere kwa wakati huo sidhani kama leo hii wapo au walishatenga pesa za mradi huo.Kuacha kumpa hongera JK ni dhuluma ya fadhila,labda Nyerere na timu yake walifikiria daraja la mbao kwa wakati huo maana hata teknolojia na ubunifu wa 1978 ni tofauti na 2012.Tunazungumza tunachokiona sasa hivi si hadithi za Nyerere au nabii Mussa.
 
Asante prezidaa...hivi wale "magamba" washajiondoa wenyewe!!...aaah...unamjua mmiliki wa "do..once"...au ushakumbuka sababu ya umaskini wetu!?....mshahara nao umepanda kati ya 15%-20%...naskia na waalimu wote washalipwa madeni yao eeh!!...pia tuna "bodaboda" za kupeleka akina mama hospitali...na...pia......

Yakheee, kadude ka kugongea like kamejificha lkn wastahili weye.

Halafu hebu nikumbushe, si huyu mtoa mipasho alisema ataweka hadharani majina ya viongozi wa dini wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya?
 
Lazima niseme ukweli, mimi huwa sipendi kwa kiongozi wa juu kutoa lugha zenye mahadhi ya kimipashomipasho, mimi ninachojua wanasiasa mara nyingi huwa wanapingana, sasa kwa kiongozi ambaye unakuwa uko madarakani inapendeza sana kutekeleza majukumu na ahadi zako halafu wananchi tutajionea wenyewe na hivyo wapinzani wake watakosa cha kusema au watatafuta jambo lingine la kubwatukia! na ni vizuri mtu akalisemea jambo baada ya kuwa limeshakamilika na sio likiwa katika hatua changa za awali- yaani mimba haijatunga bado unatamka jina la mtoto na jinsia yake!
 
Back
Top Bottom