Kikwete: Wapinzani ndio wanaochochea vita dhidi ya Malawi

Status
Not open for further replies.
HESHIMA ya taifa letu barani Afrika inaporomoka.

Nakumbuka kipindi cha Kambarage, kauli zake zilikuwa

kama moto nyikani, waandishi wa kitaifa na kimataifa walitambua.

Kumbuka majibu yake pale Jomo Kenyatta na ata pale Accra na Addis.

Waliokuwepo enzi hizo watakumbuka namna ukombozi wa Afrika ulivyokuwa

ni agenda kuu ya Kambarage na vita dhidi ya mikakati ya mabeberu.

Kauli zake ziliwapasua vichwa mabeberu na hata kuogopa encounter naye.

Ngoja niwape mkasa huu:

Nafahamu wengi wenu mwambkumbuka marehemu J>F Kennedy, aliwahi funga safari

mpaka USSR kukutana na Nikita Khrushchev, akiamini amejipanga na kwa vile yeye ni Mmarekani na

taifa lenye nguvvu angetawala mahojiano na kudictate vitu. Yaliyomsibu huko ni makubwa

hatosahau, kwa maneno yake huku akitamani kulia alitamka, "He walked all over me, made me look like a fool"

Kwa muda mrefu sana hakukuwai kutokea rais wa USA kukutana na raisi wa USSR, na hii ilidumu kwa muda

wa miaka mingi, Ndipo JFK alipoamini ana uwezo na nguvu ya kumface kiongozi wa USSR

Kisa hiki ni kukuonesha namna gani viongozi wengine huwa wamejiandaa na kujipanga kwa level za juu mno wanapokutana na maraisi wenzao na media za huko.

Haya unayoyasema ndiyo ambayo wamalawi kwenye blog zao walimuandaa Joyce Banda kumkabili Jakaya Kikwete. Joyce angeonyesha unyenyekevu basi angeshambuliwa kuliko maelezo ukilinganisha kwamba walimlaumu kwamba amezoea kuwanyenyekea heads of state wenzake hasa pale alipoinama kumsujudu Queen Elizabeth of UK wakati wako level moja ya heads of state.

Kilichompa ujasiri na kinachompa ujasiri mtut yeyote hata wewe unapokuwa mahakamani ni ukweli wa hoja yako.

Kama hoja yako ni ya kuungaunga kwa kuongozwa na vijazba viwili vitatu kama vya humu JF basi kamwe huwezi kuwa jasiri. Utakuwa jasri kwa statement mbili za kwanza. Journalist wakitandika maswali critical ujasiri wote unayeyuka kama barafu ambayo wazungu wanaita melt away.
 
Mimi naamini watanzania wengi hatuipendi nchi yetu.

Wala huitaji kuitisha kura ya maoni kujua hilo,

angali tunavyoharibu na kufuja pesa na mali ya uuma.

Mtanzania anashirikiana ana mgeni kumwelekeza namna ya kuliibia

au kulihujumu taifa kimapato. Hili sijawahi kuona nchi yeyote yenye

kusaka maendeleo dunia hii. Tembelea shanghai uone mapenzi yao na kujivunia

kwao juu ya nchi yao. Sasa hivi pale ndio kuna bandari kubwa duniani, kuanzia

mjini hadi mitaani raia wa pale wanazungumzia na kusifia namna gani wanayashinda

majiji mengine tena yaliyokuwa yametangulia kimaendeleo.

Tungekuwa na mapenzi na nchi yetu, tusingeruhusu hata raisi wetu hawe na kauli

zilizokosa mashiko nje na ndani ya nchi. Hii ni kama kuudhihirishia ulimwengu kuwa

sisi tu wa kiwango cha chini. Raisi anasema serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe,

raisi yuyo huyo anasema wapinzani wanachochea vita wakati waziri wake wa mambo ya nje na mwenyekiti

wa kamati ya bunge ye usalama na mambo ya nje ndio waliotoa kauli zinazoashiria vitisho na vita.

His this MAN on top of his game??????

Does he really pay attention to developments of various events in the country leave alone the rest of the world.

Is this a consequence of too much travel that he has become a stranger in his own country?
 
One day our grandchildren will look at us and be amazed of what kind of people we must have been.
 
Tukiambiwa tuna rais msanii tunakuja juu! haya ni maneno ambayo usingetegemea kutoka kwa kiongozi wa nchi anaejua kabisa waliotamka ni wenzie kwenye serikali na chama
 
Nashindwa kuelewa ni nini kinalisibu taifa langu.

Nikija nyumbani naona maendeleo kiasi kule ukanda wa mjini na

wa pwani kuanzia seaview mpaka bahari beach.

Nikija ule ukanda wa uwanja wa ndege kuzunguka mpaka bandarini nabaki nimeduwaa.

Yaani pako vile vile nilivopaacha yaani ni DUNI, na sasa hapa kipande cha kulia mwa barabara ya

Nyerere mpaka ubungo napo kuna makazi yameibuka, nimeambiwa ni tabata na kibangu.

Mji wetu umejipanga na kudhihirisha matabaka yaliyopo.We are brewing a social crisis kama yaliyojitokeza

kule Rio de Janero
 
Rais pamoja na waziri mkuu wote ni waongo sana, kila wafanyapo mahojiano lazima waongope kitu. Naona hili ni fundisho kwetu ili wakati tunapochagua viongozi wapate midahalo ya kutosha ili japo kubaini nani ana uwezo mzuri hata wa kujieleza tu na mingineyo mhimu
 
Napendekeza kile kitengo cha kurugenzi ya habari IKULU kipanguliwe

ama kivunjwe kabisa. Mpaka sasa sijaona kazi walioifanya kwa ustadi na weledi.

Sitaki hata kuzungumzia zile press release zenye email ya ... @yahoo.com

sitaki hata kujivunia zile picha za Rais & David Beckham, Rais na Boyz II Men

na hata zile za safari kwenye mabembea, na za juzi juzi kwenye mashamba ya mananasi
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kubwa ni kuwa kila kitu sasa hivi Tazania tunageuza kuwa siasa, matokeo yake ni kukosa mwelekeo wa pamoja kama nchi maana kila mmoja anakuja na lake, bila kujali madhara yake kwa taifa, ila maslahi binafsi ya msemaji ie umaarufa kwa kuwa tu na wewe umesema na watu wakakukuunga mkono kwa ushabiki tu na siyo kwa kuelewa faida na hasara za suala husika.
 
Nina wasiwasi labda huyu bwana ameshaafikiana makubaliano fulani na huyu mama wa Malawi labda kumuachia ziwa lote na yeye kupewa ile kitu yake anayoipenda sana tumuangalie sana huyu bwana!
kumuachia ziwa lote na yeye kupewa...maziwa mawili (hii yangu)
Huoni kama hiyo biashara inalipa, moja kwa mawili? ....teh teh teh!
 
Source: BBC

...anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.

AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.

My take:
Lowassa, Membe, Sitta ni Wapinzani?

Hata mimi nimesikia, kakuongeza hapo, ... Eti ni wapinzani wenye uchu wa madaraka... Binafsi sijawasikia wapinzani wakitoa matamko kuhusu huo mgogoro na malawi au labda JK anazungumzi wapizani wake kisiasa ndani ya chama chake anacho kiongoza. Mimi nimesikia na kusoma katika magazeti kauli za makada wa chama chake ambao ni Sita, Membe na Lowasa. Na hawa nao wapizani?
 
Kumbee! Tunashindwaje sasa?
Kwa sababu viongozi wetu ni dhaifu, wazembe, silly, watu wa kulalamika, watu wa kutafuta mchawi wetu, watu wa kutembeza bakuli, watu wa kufadhiliwa hadi suti, watu wa :smile-big:kuchekacheka, :lalala:watu wa kukanusha ya ndani na :nod:kukubali ya nje, :crying:watu wa kulialia, :lying:watu wa kusema uongo, :plane:watu wa safari, :yawn:watu wa kusinzia bungeni na baadaye:clap2:kuunga mkono hoja kwa asilimia 100.... All in all, watu :blah: :blah::blah:
 
ni kwa nini mgazeti yote ya tanzania yaliyoripoti hii ktu jana yaliruka kipengere hicho alichosema jk kwamba ni wapinzani na wenye uchu wa madaraka....kwa nini hawakuandika.....bli vyombo vya habari vya nje ndio vimeandika na kusema hilo!!!
 
ni kwa nini mgazeti yote ya tanzania yaliyoripoti hii ktu jana yaliruka kipengere hicho alichosema jk kwamba ni wapinzani na wenye uchu wa madaraka....kwa nini hawakuandika.....bli vyombo vya habari vya nje ndio vimeandika na kusema hilo!!!

Mkuu,

Ni kweli haikuandikwa kama bolded headline lakini Ansbert Ngurumo jana kwenye Tanzania Daima aliiweka kama sehemu ya article yake. (Click Here)
 
ni kwa nini mgazeti yote ya tanzania yaliyoripoti hii ktu jana yaliruka kipengere hicho alichosema jk kwamba ni wapinzani na wenye uchu wa madaraka....kwa nini hawakuandika.....bli vyombo vya habari vya nje ndio vimeandika na kusema hilo!!!

nadhani aliteleza ulimi wahariri wakaitwa boardroom fasta.
 
President wetu anasumbuliwa na jinamizi la upinzani yaani ata wale wa CCM wamekuwa wapinzani?.
 
JK asipoboil kwa muda huwa anaweza kupasuka hivyo mwacheni apumue jamani. Kupumua kwa JK lazima kutoe harufu yenye maswali kama tunayoyajadili. Jiulize aliposema hayo alikuwa anafikiri nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom