Kikwete: Wape zanzibar wanachokitaka tuishi kwa amani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Wape zanzibar wanachokitaka tuishi kwa amani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Jun 21, 2012.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nimefuatilia kwa ufupi mjadala wa bajeti unaoendelea katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na kugundua kwamba hali ilipofikia ni mahala ambapo Wazanzibar wanataka kuvunja Muungano ili wafanye mambo yao kivyao. Mengi yanasemwa lakini kwa ufupi jamaa hawataki tuendelee na umoja huu tulionao bila kujali chochote kinachodaiwa kama sababu ya kuendelea na umoja huu.

  Uamuzi huu umetawala mawazo ya viongozi hao kiasi kwamba hata wasio na sababu za msingi wanataka uvunjike ama kwa maneno ya moja kwa moja au kwa kejeli.

  Wawakilishi wengi wanaongea kwa uchungu wakidai sababu kuu ya matatizo yao yote kitaifa ni Tanganyika iliyojivika kilemba cha Tanzania. Kwa uelewa wangu baadhi wana hoja za msingi japo wengine hoja zao hazina msingi zaidi ya kwamba hawautaki tu.

  Mtazamo wangu ni kwamba nafasi ya kuujenga muungano kwa kuondoa kero zilizopo ulitumiwa vibaya na viongozi wetu husika waliojaa uvivu kama baadhi yetu, kwa kupokea mishahara ya bure pasipo kufanya kazi waliyopaswa kufanya.

  Ifuatayo ni mifano ya kero na uzembe uliofanyika:-


  • Kuhusiana na kile kinachoitwa "Double Taxation" kinachohusisha bidhaa zinazotoka nje na kupitia Zanzibar kabla ya kuingia Bandari ya Dar es salaam ni swala ambalo lingeweza kutatuliwa miaka mingi iliyopita kwa namna rahisi kabisa kama vile kuweka viwango sawa vya kodi/ushuru na kuvisimiamia kwa haki. Kama kuna sababu yoyote nzito inayolazimisha tofauti kuwepo ilikuwa ni jukumu la viongozi wanaoshughulikia muungano kuwaelimisha wananchi juu ya hali hiyo na kwa jinsi gani inakuwa vigumu kulazimisha usawa ili wasihadaike endapo kutakuwa na vuguvugu kama hili la sasa. Majibu ya maswali ya kero yangeweza kujibiwa kitaalam na kiutendaji badala ya kisiasa kama vile waziri wa Fedha kujifanya hajui kama kuna kiwango fulani cha kodi ambacho hulipiwa bandarini bidhaa zinapotokea Zanzibar.
  • Mambo ya kodi za watumishi wa Muungano waliopo Zanzibar sijui tatizo ni nini maana mchango wa Zanzibar katika kulipa mishahara hiyo ungejulikana wazi ingekuwa rahisi sana kutatulika. Ukijua serikali ipi inachangia kiwango gani na inastahili kukusanya kipi kwa kuzingatia vitu kama huduma nk. Haiingii akilini pia kudai kodi nzima kwa mishahara ambayo wewe si mlipaji.

  Siwezi kuelezea yote kwa sasa lakini inasemekana kauli za viongozi hawa zinawaweka katika hali ngumu sana Watanganyika wanaoishi Zanzibar kwani kuna mitaa ambapo wanatupiwa vijembe ikiwa ni pamoja na kutishiwa kwamba watatimuliwa ili kurejesha nchi ya watu kwa wenyewe.

  Nimetembelea Zanzibar mara kadhaa na kujifunza jamii ya kizanzibar inavyoishi na kufikiri. Ninachoweza kusema ni kwamba kama kweli taasisi za Intelligence zinafanya kazi zake vizuri watamshauri rais achukue maamuzi magumu na kuruhusu Zanzibar ijitenge ili tujenge namna nyingine ya ushirikiano kama ilivyo kwa Rwanda na Burundi ambao waliwahi kuwa pamoja na Tanganyika katika German East Africa.

  Serikali yenyewe inaweza kupuuza impact ya kauli za viongozi lakini mitaani mambo si rahisi sana kwa wabara kwa kuwa hawawezi kutofautisha anayetania juu ya Uamsho na anayetishia kwa nia hasa. Kumbukeni issue ya makanisa.

  Let us discuss this guys:- Kwa nini tusipige kura ya maoni nchi nzima? Wanaotaka Muungano na wasioutaka waruhusiwe kupiga kampeni kushawishi wananchi na kura itakapopigwa kwa haki, washindwa washirikiane na walioshinda kukamilisha zoezi ama la kutengana kwa amani au kuujenga kwa dhati na si hizi blaa blaa. Au wakuu mnaonaje?
   
 2. m

  mzaire JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 3. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Sometimes nahisi imani inashape hadi Ubongo. Ndo kusema wewe ulichokiona hapo ni ukafiri tu? Halafu nyie watu mbona ukafiri wa watu wengine unawakera sana (mnaofuata dini ya kweli kwa 100%)? Is it possible kwamba na nyie mnatamani kuwa makafiri lakini mnaogopa jamii inayokuzungukeni?
  This is too much u know!.... Kila kinachojadiliwa mwisho wake ni dini, ukafiri... hakuna mengine. Umewahi kusikia hao wanaoitwa makafiri wanakushambulieni nyie kwa jinsi mnavyoishi na imani yenu? Utashangaa nikikwambia baadhi yao hata hawajui kama mna-exist hapa duniani. Wako busy na mambo yao wakati nyie mnapoteza muda kuwatukana na kutaka wajihisi wanyonge. Cha ajabu baada ya muda mnaanza kulaumu wanapendelewa. St*** fo**.
   
Loading...