Kikwete:Wanaoua albinokuanza kutajwa kwa kura mwezi huu

Tatu

JF-Expert Member
Oct 6, 2006
1,100
313
Claud Mshana

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa, maandalizi ya zoezi la upigaji kura za maoni za kung'amua wauaji wa albino na vikongwe, limekamilika na litazinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Akizungumza jana kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa Februari, Rais Kikwete alisema kuwa maandalizi ya kutekeleza zoezi hilo yamekamilika na kwamba, waziri mkuu atafanya uzinduzi rasmi wa zoezi hilo mwishoni mwa wiki ya kwanza ya mwezi huu.


Alisema kuwa alitoa maagizo ya kufanyika kwa zoezi hilo mwezi Desemba mwaka jana kwamba wananchi wapige kura kutaja majina ya waovu hao, akiwa na dhamira ya kuwapa nafasi wananchi kushiriki kikamilifu.


"Maandalizi ya kutekeleza uamuzi wangu huo yanaelekea kukamilika, mheshimiwa waziri mkuu atafanya uzinduzi rasmi wa zoezi hilo mwishoni mwa wiki ya kwanza ya mwezi Machi, 2009 na zoezi lenyewe la kupiga kura kufanyika kuanzia wiki ya pili ya Machi, 2009."


Alifafanua kuwa katika zoezi hilo pia wauaji wa vikongwe, majambazi wa kutumia silaha na wauzaji wa dawa za kulevya nao watahusishwa.


Alitaja utaratibu wa kuendesha zoezi hilo utakuwa ni kufuata kanda na kwamba mikoa imegawanywa katika kanda saba ambazo ni Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza na Shinyanga.


Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yenye mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma; Kanda ya Kati (Dodoma na Singida), Kanda ya Kusini (Lindi na Mtwara), Kanda ya Magharibi (Kigoma na Tabora), Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara), na Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Pwani na Morogoro).


Aliongeza kuwa wakuu wa mikoa yote nchini wameshapewa mwongozo wa jinsi ya kutekeleza zoezi hilo na kutaja miongoni mwa mambo watakayotakiwa kuzingatia ni pamoja na kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi hilo, upigaji kura ufanyike mwezi Machi kwa tarehe zitakazopangwa kwa kuzingatia kanda hizo.


"Kamati za ulinzi na usalama za mikoa zikiongozwa na wakuu wa mikoa zisimamie zoezi hili kwa makini. Kadhalika, kamati za ulinzi na usalama za wilaya zikiongozwa na wakuu wa wilaya zitaongoza utekelezaji katika wilaya zao na kushirikisha serikali za vijiji na mitaa," alisema Rais Kikwete.


"Napenda kuitumia fursa hii kuwasihi Watanzania; wake kwa waume; vijana na wazee tujitokeze kwa wingi kuwataja watu wanaojihusisha na maovu hayo katika jamii. Kura ni siri, hakuna atakayejua umemtaja nani. Hata msimamizi wa kituo hawezi kujua," alisema.


Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete ameagiza viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuwashughulikia watumishi wote wazembe wanaosababisha matatizo ya mlundikano wa madai ya walimu na watumishi wengine wa umma.


Kikwete alisema kuwa mlundikano wa malimbikizo ya madai ya watumishi wa umma husababishwa na uzembe wa wakuu wa kazi wasiojali maslahi ya walio chini yao.


Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alisema kuwa sehemu kubwa ya madai ya malimbikizo ya walimu yanahusu stahili zao za uhamisho, kupandishwa madaraja na likizo na kuongeza kuwa panapotokea migogoro hiyo, wale waliosababisha malimbikizo hayo hawaonekani kuwa ndiyo wakosaji bali serikali kuu ndio huonekana na huingilia kati kuokoa jahazi.


"Napenda kusema kuwa matatizo wayapatayo walimu ndiyo wayapatayo watumishi wengine wa umma katika wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali, hivyo watumishi wote wa idara za serikali wanaosababisha kero hizo wachukuliwe hatua mara moja," alisema Kikwete.


Rais alisema pia tabia ya watu kukaa katika kituo kimoja kwa muda mrefu, huzaa tabia za kufanya kazi kwa mazoea na hivyo kuagiza watu walioko katika kituo kimoja kwa muda mrefu, wahamishwe.


"Nimeagiza watu walio kituo kimoja kwa muda mrefu wahamishwe, kuwahamisha mara kwa mara kutasaidia kuondoa usultani," alisema bila ya kudokeza jaribio la mgomo wa walimu lililotikisa nchi mwishoni mwa mwaka jana, wakati wakishinikiza kulipwa kwa madai yao ya zaidi ya Sh16 bilioni.


Kwa mujibu wa Rais Kikwete alipofanya ziara na kuongea na viongozi wa kisiasa na kiutendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, walikubaliana kuwa malimbikizo ya madai ya malipo ya stahili mbalimbali yapatiwe ufumbuzi, kwani yamekuwa chanzo cha mivutano kati ya serikali na walimu.


Alisema mivutano hiyo haina lazima wala sababu akisisitiza kuwa, kama wahusika katika idara za utawala na fedha katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Wizara ya Utumishi na Wizara ya Fedha na Uchumi wangetimiza ipasavyo wajibu wao, kusingekuwa na malimbikizo hayo.


"Nilielekeza kuwa kama halmashauri haina pesa za uhamisho, wasiwahamishe watumishi wao; wamekuwa wanafanya hivyo na kulimbikiza madeni makubwa ambayo yamekuwa yanalipwa na serikali kuu mara nyingi baada ya walimu kuchachamaa. Serikali kuu imekuwa inafanya hivyo kuepusha shari, bahati mbaya hiyo imegeuka kuwa mazoea," alisema Kikwete.


Rais alisema kuwa hali hiyo imejengeka na kuonekana kuwa kumhamisha mtumishi kutoka kituo kimoja kwenda kingine wilayani, ni wajibu wa serikali kuu kugharamia uhamisho huo na matokeo yake ni malimbikizo na madai yasiyokwisha yanayozua migogoro ya mara kwa mara.


"Niliagiza mtindo wa kuhamisha walimu bila ya kuwa na fedha za uhamisho ukomeshwe mara moja... ni marufuku kufanya hivyo na agizo langu hilo haliwahusu walimu tu, bali watumishi wote wa umma. Kiongozi au mhusika yeyote atakayekiuka agizo hili, alipishwe yeye gharama za kumhamisha mtumishi huyo," alisema rais.


Kuhusu madai ya likizo, Kikwete alisema hali ni ileile kwani fedha ambazo zilipaswa kugharamia likizo kama hazikutengwa, madeni yatazidi kuongezeka siku hadi siku na kusisitiza kutengwa fedha za kutosha za likizo kwani mapumziko ni muhimu kwa wafanyakazi.


Kikwete pia alizungumzia suala la kuwapandisha watumishi vyeo bila kuwarekebishia mishahara yao, kuwa ni upungufu wa kiutendaji ambao alisema ni lazima ukomeshwe mara moja.

Source: Mwananchi.

This is very disturbing coming from the president. I think this is playing with people's lives. We have different police force and state body to carry investigations but the pres. comes with this approach.

Can you convict someone in the court just buy votes?

JK refuses to take some of FISADI's to court like AC and Dr. IR with all the evidance he got but he wants to vote on peoples who kill Albinos, I don't get it all. Not sure where we are heading as a country.
 
Apa kutakuwa na mkinzano wa kisheria kwa sababu kama wanataka iwe effective lazima watu wapelekwe mahakamani, na mahakamani wanataka ushahidi, sasa sijui kama ushahidi wa kura utakubalika? Hii imekaa kisiasa zaidi!
 
Huu ni usanii mwengine ambao unaonyesha udhaifu wa Utwala wa CCM, maana haielekei wala hakuna haki hapo,yaani mkimchukia mtu basi ndio mnaweza kumgandamiza, yaani hata kijiji kinaweza kumwangamiza balozi na hata mkoa unaweza kumwangamiza mkuu wake, ,naona hapa CCM wanajimaliza kabisa ,maana wasijwe kupata kigugumizi cha kuwataja walioshinda kwa kura ,lazima watabadili matokeo ,Tume ya CCM haijawahi kutangaza mshindi.

Shime wananchi huu ni wakati mwengine wa kuwapiga na chini CCM kura yako ipeleke kwa mkuu wa wilaya Mkuu wa mkoa na mbunge wa CCM wote hao wanawalinda mafisadi.
Hata Mawaziri washindiliwe humo humo.
 
Source: Mwananchi.

This is very disturbing coming from the president. I think this is playing with people's lives. We have different police force and state body to carry investigations but the pres. comes with this approach.

Can you convict someone in the court just buy votes?

JK refuses to take some of FISADI's to court like AC and Dr. IR with all the evidance he got but he wants to vote on peoples who kill Albinos, I don't get it all. Not sure where we are heading as a country.

Apa kutakuwa na mkinzano wa kisheria kwa sababu kama wanataka iwe effective lazima watu wapelekwe mahakamani, na mahakamani wanataka ushahidi, sasa sijui kama ushahidi wa kura utakubalika? Hii imekaa kisiasa zaidi!

...tatizo limejikita mizizi ndani ya jamii husika kiasi kwamba inabidi sheria zipindishwe, ...baada ya kura, ndiyo uchunguzi utafanyika ili 'watuhumiwa' waje fikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Kuna waliokwisha kamatwa red-handed kuhusika na mauaji au attempting kuua.... wameshuhudiwa wakiwa na madamu au na baadhi ya viungo. Hawa wamefanywa nini hadi leo hii? Au ndio yaleyale ya 'jamaa yetu' aliyekutwa na USD idadi ya ajabu tunasema bado hakuna ushahidi haupo wa kutosha kumsulubu?

Ndio nchi yetu ya amani hiyo, na wananchi wake watulivu kama nini! chochote kwenye ardhi hii na juu ya vichwa vyao ukiwa na nafasi ya kufanya we unapeta tu.
 
Jamani mie sijamwelewa ndugu Rais
Kuna Usalama wa Taifa, Polisi, Vituo vya Polisi hadi vijijini, kuna CID nk wote hawa wameshindwa kujua ukweli wa mauaji haya ? Mbona hajaja kutupa uhuru wa kuongelea Mgombea binafsi ,ununuzi wa mitambo ya Dowans , mambo ya EPA na hasa kagoda ?
 
Huyu anakumbusha mambo ya shule ya msingi.Yaani ukipigiwa kura hakuna kujitetea.

Sitakua nimemkosea Rais heshima kama nikihoji Upeo wake wa kufikiri.

Je,rais amezingatia chuki binafsi baina ya mtu na mtu.Ni nini madhara ya hizo kura? Rais kweli amepima na kuona hilo ndio suluhisho? He want to encourage people to abandon the rule of law?

Kuna tofauti gani kati ya kitendo hiki na kile alichofanya waziri mkuu?

Hapa lazima kutakua na uonevu,hata kama kutakua na umakini lakini wataumia watu wengi wasio na hatia,na inawezekana wahusika wakapeta kiulaini kabisa,ila sheria itakua na nafasi ipi hapo?
 
Ina maana watakaopatikana na kura nyingi watachomwa moto au ndio watakapelekwa mahakamani?? Au ndio uchunguzi dhidi yao utaanza??

Ama kwa hakika mtu yeyote anaweza kuwa raisi wa nchi hii!! (I mean mwizi yeyote).
 
Hivi Huyu Muungwana hana Washauri!!,Naogopa nafikiri sasa Mkuu amepatwa na Ugonjwa unaomuondolea sifa za kuongoza Watanzania....Hii inaonyesha ni kiasi gani utawala wa Sheria unapindwa,Wanasheria msaidieni Mkuu,hatuwezi kuongozwa na Jazba kuna sheria na vyombo vya usalama ambavyo vinaweza kufanya kazi kwa ushahidi kuliko kura zitakaowataja akina Mengi bila Ushahidi!!
 
Kikwete anazidi kunisikitisha... duh! yaani hii ya kura ni mpya kabisa maanake hai fit popote iwe sheria (katiba) ama chini ya mti..hata nashindwa kuelewa hizi vote zitaweza vipi kusaidia...
Mauaji haya hayafanywi kimiujiza, watu 173 tayari wameisha kamatwa na ushahidi tosha kabisa wa kuwasimamisha mahakamani, hadi leo hii serikali imewaweka rumande tu tena nje ya sheria!..

(UNICEF condemns these heinous acts as a systematic violation of individual human rights that must be dealt with decisively," the agency said in a news release.
Tanzanian authorities have arrested 173 suspects, including five policemen, in connection with the murders, and are offering protection to albinos throughout the country. Tanzanian President Jakaya Kikwete has also condemned the attacks and called for tough action against the killers. UNICEF lauds those measures, but is calling on the judiciary, the media, religious leaders, politicians and communities to bolster the response and weed out deeply-rooted superstitious beliefs that incite the murders.)

Hapa Canada tayari kimeanzishwa chombo (NGO) kupinga Mauaji ya Albino - Tanzania (Stop the killings of Albino) na wanashinikiza serikali ya Canada kutopeleka msaaada wowote kwa serikali yetu..Pia Immigration and Refugee Board of Canada tayari imekwisha toa sheria (112) kuwapa hifadhi hawa jamaa lakini ndio hivyo ten (mpaka wafike huku)..
Zaidi ya yote hayo kila siku wana matangazo yao ktk radio za hapa..tena mbali na matangazo kuna kipindi maalum cha kutuma salaam....Yaani inauma kusikia mtu akiomba kuitaka serikali ya Canada kuwachukua hao Albino toka mikononi Cannibals..
Yaani sisi wote machoni mwa hawa jamaa tunaonekana kuwa ni Cannibals!.....damn.
 
Sasa mnapoambiwa CCM imepoteza dira mnafikiria masihala ,kila mmoja anaamua anavyoona tu ,ni juzi tu nilisema tutaona memngi baada ya mbabe wa CCM kutembeza mkong'oto kwa walimu ,raisi kaamua kumfukuza ,hakujakaa vizuri dc mwengine anamuunga mkono aliefukuzwa ,hivi hizi hamuoni kama si dalili nzuri katika nchi ,watu hawa hawakushinda kwa ridhaa za wananchi hivyo wanajiamulia na kujifanyia watakavyo maana hawana uchungu na nchi hii kabisa, kwenda kusema wananchi wapige kura kwa wanaowatuhumu kwa mambo hayo ,mimi sikutegemea kama kweli raisi amesema hayo ,hadi sasa badu kabisa sijaamini ,aidha mshauri wa raisi aliekuwepo karibu hafai au anatumika kumzamisha raisi ,ndio maana yake ,yaani wamepanga huko kwenye vikao vyao ,kisha wanampa raisi katangaze kwenye hotuba yako ya mwisho wa Mwezi ,jamani mumeisoma ile picha ya Mama Maria Nyerere na Kikwete ,kwa kweli yule mama kwa jinsi anavyomtazama Kikwete ,ni kama anamwambia hujui kuongoza nchi ikiwa mambu yenyewe ndio haya.
 
Waomba watumie 'darubini' kukamata wauaji
Na Brandy Nelson, Mbeya

WAZEE wa mila (machifu) wa makabila ya Wilaya ya Mbeya mkoani hapa wameiomba serikali iwape ruhusa ya kutumia 'darubini' zao ili kuweza kuwakamata wauaji wa maalbino, wapiga nondo na kuwahamishia mimba wanaume wanaowapa mimba wanafunzi ili kukomesha tabia hizo.


Waliyasema hayo jana katika mkutano na mkuu wa mkoa uliohudhuriwa na machifu zaidi ya 100 kutoka Wilaya ya Mbeya Vijijini na jiji katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Igawilo Uyole nje kidogo ya Jiji la Mbeya.


Walisema kuwa wanashangazwa na tabia ya serikali kutowashirikisha viongozi hao katika matukio mbalimbali yakiwemo ya uhalifu, ya kuwasaka wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), upigaji nondo ambao umekithiri mkoani hapa na watu wanaowapa mimba wanafunzi na kuwaharibia maisha.


Mwenyekiti wa wazee wa mila wa wilaya, Shayo Masoko (chifu mkuu ) alisema kuwa wameamua kuandaa mkutano huo na kumwita Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile baada ya kuona kumekuwepo na ongezeko la matukio ambayo hayaipendezi jamii na serikali imekuwa ikifanya jitihada zake kwa kutumia gharama kubwa bila mafanikio.


"Sisi mkuu wa mkoa tumekuita hapa tunataka tuongee na wewe kwa niaba ya serikali yetu, kwani kumekuwa na matukio mengi mabaya, lakini nyinyi kama serikali mmekuwa hamtushirikishi sisi wazee wa kimila sijui kama mnatudharau au hamtambui kama tuna uwezo mkubwa ambao tumepewa na Mungu wa kuweza kuyamaliza matatizo hayo,"alisema.


Chifu Masoko alisema kuwa machifu hao wana uwezo mkubwa wa kukomesha matukio hayo kama serikali itawashirikisha na kuwapa ruhusa ya kukemea na kutumia 'darubuni' zao kwani wazee hao wana kamati zao za ufundi ambazo wamepewa na Mwenyezi Mungu.


"Tumelisikia tukio la hawa ndugu zetu maalbino sisi tuna uwezo wa kuhakikisha wanakamatwa wahalifu wote na hawa wapiga nondo pia hawatushindi, kwa kupitia 'darubini' zetu tunaweza kusababisha wakamatwe au kuwavunja vunja miguu ili kukomesha matukio hayo."


Alisema kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuisaidia serikali katika masuala kama hayo zaidi ya machifu, hivyo ni vema serikali ikachukua hatua za haraka katika kuwaruhusu ili waweze kutumia 'darubini' zao na sauti zao ili kuweza kukomesha tabia hiyo na serikali isiingie gharama kubwa katika kutafuta wahalifu hao.


Naye chifu mkuu wa Tarafa ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini, Rocket Mwanshinga alisema kuwa hata kwa wale wanaume wanaowapa mimba wanafunzi mashuleni, machifu hao wana uwezo wa kuwahamishia mimba hizo ili iwe fundisho kwa wanaume wengine na kupunguza tatizo la mimba mashuleni.


Alisema kuwa kama machifu wanasikitishwa na ongezeko la wanafunzi kupata mimba wakiwa shuleni na baadaye wanaume wanaowapa mimba huwakataa na maisha ya watoto hao kuharibika, hivyo dawa ni mimba hizo kuzihamishia kwa wanaume hao ili iwe fundisho kwa wanaume wengine .


Akizungumza baada ya kuwasikiliza machifu hao, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile alisema kuwa serikali inawatambua na inawathamini sana viongozi wa jadi na kwamba, inatambua kuwa machifu wana nafasi kubwa katika maendeleo ya jamii.


Aidha aliwashukuru machifu hao kuandaa mkutano huo na kumwita, kwani tangu alipokuwa kiongozi hajawahi kuhudhuria mkutano kama huo na kwamba, aliwataka machifu hao kuendelea na juhudi zao za kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za kijamii.


Katika mkutano huo ajenda sita zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na mauaji ya albino na upigaji nondo, utovu wa nidhamu kwa watu wachache waliokosa busara, usalama wa viongozi, mapungufu ya ushirikiano kati ya serikali na wazee wa mila, manyanyaso kwa jamii na maombi kwa serikali.

My take: I dont know,in which direction are we heading now! Hadi mkuu wa mkoa naitwa na washirikina kupewa alternative? Si serikali haiamini katika ushirikina? Yaani ndiyo tumefika huku?
 
Ninaweza pata wapi hii hotuba nzima ya rais ya tarehe 28 feberuari 2009?
 
Sasa kama si kushindwa kwa Utawala wa CCM ni kitu gani ? haya tusubiri Sasa tuwe na serikali ya washirikina. Yaani mambu yetu mwaka huu lazima yaandikwe kwenye genuine books,ni viroja tu kimoja baada ya kingine na haya hayafanywi kwa bahati mbaya ili mjue kuwa ni mambo yanayotayarishwa ili kuwasshugulisha wapinzani na wananchi kwa ujumla ,lakini kuna Wanaume wa kazi CUF wameanza kuwasha moto kuwa hawa CCM waondoke tu ,mida wao umeshakwisha na wasiwapotezee wananchi muda wao wa kuendelea na hatua ya kujikwamua hapa walipo.
 
Jamii ya Kitanzania inazidi kudidimia kwenye lindi la ujinga mkubwa usio na kifani.Tatizo la kuuliwa maalbino ni kipimo tosha kuwa tuna ujinga mkubwa zaidi kuliko tunavyodhani.
 
Kama hata mkuu wa mkoa anaweza kukaa na kukubali kujadili jambo kishirikinashirikina unategemea nini? Hivi siku watu wakiibuka na imani kwamba ili kusolve tatizo lazima tupate viungo vya mtu mwenye rangi nyeusi kabisa itakuaje? Maanke huku ndiko mambo yanakoelekea sasa,alternative za kishirikina? M tired and sick!
 
HIZI KURA ZIKIPIGWA MJUE TUMEKWISHA: JAMANI APATIKANE MBUNGE WA KUANDAA HOJA BINAFSI KUM-IMPEACH RAIS KWA KUKIUKA KATIBA. MUNGU WANGU; KURA ZA MAONI ZA NINI? Fukuza IGP, DGI, DCI, Ma RC wa Mikoa husika, kama utasikia Albino anakufa. Huko siyo kukiuka haki za binadamu maana hawa ni wateule wa kisiasa, wameshindwa kufanya kazi, Rais ameondoa mkono wake.

Yeye mbona alichukia REDET walipotangaza kura za maoni kuwa amepoteza mvuto? Si nao walichukua kura za maoni? Tumekwisha.
 
Back
Top Bottom