Elections 2010 Kikwete: Wakuu wa mikoa msivuruge uchaguzi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079
kikweteafya.jpg

Rais Jakaya Kikwete

RAIS Jakaya Kikwete amewataka wakuu na wakurugenzi wa mikoa na wilaya kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa wa haki na huru.

Aliwatakata kuhakikisha kuwa uchaguzi huo hauharibikii mikononi mwao na wahakikishe wanawapa wagombea wa vyama nafasi sawa ya kunadi sera zao bila bughudha wala vitisho.

Kikwete alitoa rai hiyo jana wakiti akifungua semina ya maelekezo ya kuelekea uchaguzi mkuu ujao Oktoba 31, mwaka huu iliyowashirikisha viongozi hao katika ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma jana.


Aidha, Kikwete aliwataka watendaji hao kuendelea na shughuli za serikali kama kawaida na kusisitiza kuwa wakati wa uchaguzi serikali hailali bali shughuli zake zinaendelea kama kawaida huku akiwazuia watendaji hao kwenda likizo.


"Mkutano huu ni wa kuangalia mbele. Tunakwenda katika uchaguzi, serikali hailali na haiendi likizo. Hilo ni muhimu, hakuna kwenda likizo", alisema Kikwete.


Alisisitiza akisema: "La msingi ni kuhakikisha uchaguzi hauharibiki. Ukiharibika umeharibika mikononi mwetu, nisingependa kuona uchaguzi unaharibika mikononi mwetu:

Wagombea wasinyimwe nafasi ya kumwaga sera zao na wananchi wapate nafasi ya kushiriki kampeni na fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka".

Alisema mchakato wa uchaguzi huo tayari umeanza kwa baadhi ya vyama kufanya uteuzi wa wagombea wake ambapo kwa mujibu wa ratiba yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), itafanya uteuzi Agosti 19 na kampeni kuanza Agosti20 mwaka 2010.

Awali Kikwete aliwaambia watendaji hao kuwa miaka mitano ya utawala wake ina mafanikio makubwa yanayojieleza.


Alisema mafanikio hayo yapo katika nyanja za barabara, elimu, afya na maeneo yote waliyodhamiria akieleza na kwamba bajeti ya mwaka wak fedha 2010/11 ni ya kukamilisha ahadi zao.


Akimkaribisha Rais Kikwete, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema watendaji hao wamejitahidi kutekeleza majukumu yao na kwamba, ana imani kuwa Kikwete atashinda katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na watendaji hao kuendelea kumsaidia katika awamu ijayo.

Awali, Waziri wa Nchi tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Celina Kombani alisema semina hiyo itawaelekeza la kufanya wakuu wa mikoa na wilaya wanaotaka kugombea nafasi katika uchaguzi mkuu ujao ambapo Mkurugezni wa NEC Rajabu Kiravu alitoa semina.


Wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakilalamikiwa na vyama vya upinzani kuwa wanavikandamizwa vyama vya upinzani wakati wa uchaguzi.


Baadhi yao wamekuwa wakituhumiwa kutumia ubabe wa kuwanyima uhuru wa kufanya kampeni baadhi ya wagombea kwa kisingizio kwamba wanahatarisha amani.

Tayari vyama vikuu vya upinzani nchini vimeionya serikali kuhusu maandalizi duni ya Uchaguzi Mkuu ujao na kutoa angalizo kuwa iwapo kutatokea vurugu kutokana na maandalizi hafifu CCM itabeba lawama kwa kuwa inaweka mazingira hayo.

Wanasema wanasikitishwa na kitendo cha serikali ya CCM kushindwa kuweka mazingira mazuri ya Uchaguzi Mkuu huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikitangaza tarehe ya uchaguzi huo kuwa ni Oktoba 31, mwaka huu.

Wanasema moja ya rafu ambayo inafanywa na serikali ya CCM ni kwamba mpaka sasa hajatoa kanuni za sheria mpya ya gharama za uchaguzi wala sheria yenyewe hawaijui kufuatiwa kufanyiwa marekebisho baada ya serikali kuingiza kinyemela vifungu tata vya kuilinda.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kutokana na umuhimu wa Uchaguzi Mkuu ni hatari kwa taifa kubakiza miezi michahe kuingia katika kipindi hicho bila wadau muhimu kama viongozi wa vyama vya siasa kujua sheria, kanuni na maadili yanayotawala uchaguzi huo.

Alisema awali, waliposikia sheria mpya ya garama za uchaguzi walifarijika wakiwa na matumaini kwamba, ina nia njema ya kupunguza gharama za uchaguzi, lakini baadaye wamebaini kwamba sheria hiyo imewekewa vipengele vya kukandamiza vyama vya upinzani na kuitafutia nafasi CCM kutawala milele, jambo ambalo ni kuweka mwanya wa mgogoro katika uchaguzi.

Alitaja kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyotoa kwamba takrima haikwepeki kuwa ni sababu nyingine inayowapa hofu ya maandalizi hafifu ya uchaguzi huo kwamba, tafsiri yake ndio kiini cha CCM kusaka bilioni 50 kwa ajili ya uchaguzi huo.

Hatua ya Rais Kikwete kuzungumza na wakuu wa mikoa, wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri kuzungumzia uchaguzi anafuata nyanyo za Rais Benjamin Mkapa, ambaye alifanya hivyo mwaka 2005 na kusema kuwa baadhi ya vyama vya siasa vimeanza kuandaa vijana, ili kufanya fujo na vurugu wakati wa uchaguzi.

Rais Mkapa alisema fujo na vurugu ni adui mkubwa wa juhudi za kujenga mazingira mazuri ya amani na utulivu katika uchaguzi na kwamba haiwezekani kuwa na uchaguzi huru na wa haki, katika mazingira ya fujo na vurugu.


Rais Kikwete amekuwa akifanya semina mara kwza mara na wakuu wa mikoa na wilaya. Mara alipoingia madarakani alikutana nao mjini Arusha katika ukumbi wa Hoteli Ngurudoto.


Hata hivyo pamoja na kukutaa nao mara kwa mara baadhi ya wananchi wamekuwa wakiona semina hizo hazina tija kutokana na viongozi hao kuendelea kuvuruga kazi zao. 



Kikwete: Wakuu wa mikoa msivuruge uchaguzi
 
Nimeona tangazo kwenye baadhi ya magazeti ya leo uhusu dirisha dogo lauandikishaji wa wapiga kura ambao utasimamiwa na afisa mwandikishaji ambaye atakuwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika.

Mpiga kura anatakuwa aende na picha mbili za ukubwa wa passport zenye mwonekano nyuma wa kijivu. Utaratibu huu unaanza tarehe 1 Julai 2010 na kuisha tarehe 10 Julai 2010.

Hakuna utaratibu mwingine kwa maana ya checks and balances kuraibu abuses zinazoweza kujitokeza. Hili mnalionaje na hii semina inayoendelea sasa Dodoma . Can we say that kuna instructions wameenda kuchukua?
 
Nimeona tangazo kwenye baadhi ya magazeti ya leo uhusu dirisha dogo lauandikishaji wa wapiga kura ambao utasimamiwa na afisa mwandikishaji ambaye atakuwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika.

Mpiga kura anatakuwa aende na picha mbili za ukubwa wa passport zenye mwonekano nyuma wa kijivu. Utaratibu huu unaanza tarehe 1 Julai 2010 na kuisha tarehe 10 Julai 2010.

Hakuna utaratibu mwingine kwa maana ya checks and balances kuraibu abuses zinazoweza kujitokeza. Hili mnalionaje na hii semina inayoendelea sasa Dodoma . Can we say that kuna instructions wameenda kuchukua?

Mimi naamini kabisa haya maneno ya Kikwete ni kujiosha tu mbele ya Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, lakini lazima kutakuwa na abuse chungu nzima ambazo zitalenga kukipa ushindi mkubwa CCM. Mpaka hapo tutapokuwa na NEC ambayo si kitengo cha CCM na vyombo vya dola vitakuwa huru kuhakikisha haki katika chaguzi zetu inatendeka badala ya kuifagilia CCM basi chaguzi zetu zitaendelea kujaa matatizo chungu nzima kwa faida ya CCM.
 
Hakuna mwenye ugomvi na kura za urais ingawa hatkuridhika na uongozi wako kwa kipindi cha miaka 5. lakini looh sijuwi ni shekh yahya au ni nani aliyetolowesha maji?.

Ila kwenye ubunge lazima mkipate cha moto mwaka huu.
 
Hii kweli si-hasa! Of course lazima aseme, lakini anaujua ukweli. Ma-RC, Ma-DC, Ma-DAS na Ma-RAS wote tayari wameshapewa circulars zao jinsi watakavyovuruga uchaguzi kwa manufaa ya Chama Tawala. JK anayasema hayo kujikosha mbele ya International Community.

Kumbukeni ya Kawe 1995. Wale waliokamatwa pale Tanganyika Packers, wakiwa na TZS 6 M, ambazo zilitayarishwa kuwahonga mawakala wa vyama, pamoja na masanduku 6 ya kupigia kura ambayo tayari yalikuwa na kura ambazo zilikuwa zimepigwa. Ile kesi iliishia wapi? Kuna yeyote aliyewajibishwa? Au ninyi ni wepesi wa kusahau?

Hawakuanza leo wala jana, na wala hawatakoma leo wale kesho, kuvuruga uchaguzi. Ndio maana Makamba alikwishasema, ushindi kwa CCM ni lazima 2010! Anajua anachokisema.

Hii ni demokrasia kiinimacho.

Kwa hasira sita-sign leo!
 
Back
Top Bottom