Kikwete uvumilivu wa wananchi una ukomo wake na dalili zimeanza kujitokeza waziwazi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete uvumilivu wa wananchi una ukomo wake na dalili zimeanza kujitokeza waziwazi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Feb 13, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu kikwete,

  Naandika ujumbe huu nikiwa kama nabii ninayeleta ujumbe mwema kwako. Sijatumwa na Mungu au mtu yeyote. Nimetumwa na nafsi yangu inayolia na kulitakia mema taifa letu la Tanganyika na Tanzania kwa ujumla. Mimi ni raia wa kawaida mwenye kipato cha wastani. Ninaishi mtaani ambako kuna mchanganyiko wa watu wenye uwezo wa kimaisha tofauti na elimu tofauti. Ninapenda sana kuchangamana na makundi tofauti ya watu, kuanzia umri, elimu, kipato, imani, n.k. Jambo moja ambalo kamwe usitake kulibeza kama bado unahitaji kuendelea kukalia kiti hicho ni hali mbaya ya maisha. Wananchi wanalia. Wanajuta kwa nini walikuchagua wewe. Huo ndio ukweli hata kama hupendi kusikia hivyo. Popote uonapo mkusanyiko wa watu jina lako haliachwi kutajwa kwa mabaya. Hata wachache wanaoendelea kukutetea sasa wanaona aibu kufanya hivyo maana nao nafsi zao zinawanyoshea vidole. Maongezi mengi yanahusu huduma za umeme, maji, bei za vyakula, mikopo ya wanafunzi, dowans, epa, n.k. Katika maongezi yote niliyoshiriki, kila mwongeaji alihusisha hali hii mbaya ya maisha na ugoigoi wa uongozi wako. Maongezi ya aina hiyo yapo kwenye mabaa, vituo vya daladala, ndani ya daladala, hotelini, makazini, nyumbani, n.k.

  Ushauri wangu kwako ni mdogo tu. Chukua hatua sasa, mapema iwezekanavyo kabla wananchi hawajalipuka. Kimya kingi cha watanzania kitakuwa na mshindo utakaoandika hostoria duniani. Usidhani unafiki wa kuimba 'nchi yenye amani na utulivu' utakusaidia. Inawezekana unajidanganya kwamba watanzania hawana hulka ya kufanya fujo. Kama ndivyo unavyowaza, basi unajidangaya. Hakuna mwanadamu duniani anayeweza kuvumilia mateso siku zote na dalili zimeanza kujitokeza waziwazi. Nakuomba uchukue hatua sasa kunusuru taifa. La sivyo, wewe pamoja na familia yako na wapambe wako anzeni kufikiria maisha mtakayoishi baada ya wananchi kucharuka.

  Nimeandika kama utani, lakini huo ndiyo unabii wangu kwako leo.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hongera kwa kujipa cheo cha UNABII,pia kwa kuwa na UNDUGU na jeikei!hop atajuzwa
   
 3. i

  ibange JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wandugu tuache ushabiki wa upande wowote. watanzania mijini kwa vijijini wamechoshwa na ugumu wa maisha na wanaichukia sana serikali. kama uchaguzi ungefanyika leo na wav waruhusiwe kujiandikisha jk hawezi kushinda. lazima serikali ichukue hatua la sivyo yatatokea ya misri
   
 4. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi kwani kikwete ndo anaongoza Tz au Salma? mwambieni Salma jamani siku akiamua tu mafisadi watashughulikiwa....Msimulaumu kiwete mlaumuni Salma rais wetu...
   
 5. P

  Proud Patriot JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  u mean ROSTAM?
   
 6. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gosbertgoodluck
  Umeandika vizuri lakini nani alikuambia sikio la kufa linasikia dawa?!
  Unamaliza muda na nguvu zako kushauri dawa!.
  Wataka mkulu arekebishe nini?
  -Hawezi kureverse hasara iliyopatikana kwenye mikataba yote mibovu
  -Hawezi kufufua watu wote wanaokufa/waliokufa kutokana na huduma mbovu mahospitalini, polisi, mahakamani nk
  -Hawezi kuwakamata wahalifu wakubwa wa uchumi wetu
  -Hawezi kurudisha imani ya wananchi kwa serikali
  ANGUKO limeishatokea kinachotafutwa ni mahala pa kuangukia.!
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  LAITI NINGALIKUA RAIS KIKWETE NISINGEKAA HATA ZAIDI YA LISAA MOJA
  BAADA YA RIPOTI YA JUMUIYA YA NCHI ZA ULAYA KUWEKA WAZI
  KWAMBA NIKO MADARAKANI KIMABAVU KWA WIZI KURA:


  Kwa kweli wananchi inabidi tufike mahala tujiulize kwamba hizi nafasi za kuchaguliwa mtu, kwa mantiki kabisa kidemokrasia, ni (a) nafasi za AJIRA BINAFSI KWA YEYOTE ANAYEJIMEGEA KAKIPANDE au (b) ni fursa tu yenye dhamana kubwa na ridhaa ya wananchi ukawatumikie??

  Kama jibu sahihi ni bee hapo juu sasa iweje mtu uwe umeuchubua tu ofisini hata baada ya RIPOTI YENYE UJUMBE NZITO NA NYETI kama ule uliowashilishwa na Jumuia ya Nchi za Ulaya?? Na unapoendelea tu kujing'ang'aniza hivo hivo wapiga kura wapende wasipende, ilmradi tu kuna wazo liliwahi kutoka kwamba rais huongoza kwa awamu mbili, ndio tuseme kwamba uso wa aibu ulishakutoka siku nyingi au ndio kusema kwamba nawe unajaribu kuwapima Wa-Tanzania kwamba watakufanya kitu gani sio??

  Laiti ningalikua rais Kikwete wala nisingejiruhusu nafsi yangu kuendelea kukaa hata kwa lisaa moja zaidi tangu Jumuiya ya Nchi Ulaya itoe ripoti yake inayobaini wazi madai yetu ya muda mrefu kwamba CCM IMEIBA SANA KURA KOTE TANZANIA BARA NA VISIWANI; katika ngazi zote za uchaguzi.

  Nasema hivyo kwa sababu kwa binadamu ambaye bado angependa kujitunzia heshima yako hauwezi kuendelea tu kuchapa usingizi huko kwenye ikulu ya watu kana kwamba hakuna chochote kibaya kilichotokea wakati tayari ni kwamba hauko madarakani kwa ridhaa wananchi. Cha zaidi, hao wenzetu waliotoa ripoti yao pindi wanapoendelea kukuona madarakani wanashindwa tu kukuambia kwamba KWA NINI UGEUZE NAFASI ZA UTUMISHI KWA UMMA KUWA AJIRA BINAFSI kwako kama alivyofanya Mubara??

  Pengine ndio maana Marais walipokutana Africa Union na kuhoji kwa nini watu waondolewe madarakani kwa njia ya maandamano zaidi badala ya kwa njia ya SANDUKU LA KURA, nikasoma habari kwenye internet inayowakejeli marais hawa ile mbaya juu ya madai yao hayo. Mwandishi huyo alikua akisema kwamba katika mataifa mengi sana wananchi hawajawahi kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa zaidi ya miaka ishirini au salasini huko.

  Kwa kuangalia kwa haraka haraka kauli hii mtu utadhani ni upuuzi mtupu tu ndio unaoongelewa hapa lakini ukizama zaidi kwenye kufiki utakuta kwamba kuna ukweli mzito mno nyuma ya hayo madai ya mwandishi huyo. Kwa mfano, itakua vipi mtu aliyeshinda kwa kishindo kama Hosni Mubarak (Asilimia 93 % kwenye uchaguzi wa mara ya mwisho) aliyekataliwa tu na Wa-Misri kiduchu asilimia 7 % akafikia mahala akatimuliwa na 'Nguvu ya Umma' madarakani hata kabla ya kufikia nusu ya awamu yake hiyo nyingine??

  Na tukirudi hapa nyumbani ni lazima tukajiuliza kwamba mbali huu wizi wa kura wa hivi majuzi wazi wazi kabisa kwa Rais Kikwete, je huko mwaka wa 2005 pamoja na ushindi kwake hivi ni kweli huyu ndugu KWELI KABISA alipata huo ushindi wa kishindo kwa asilimia hiyo hiyo 87 % au ndio haya haya tulioyaona mwaka jana??

  Kwa kweli ni kero, chukizo na udhia wa kila aina ambayo ni sharti lisawazishwe haraka mno ili heshima ya mwananchi KUJICHAGULIA KIONGOZI anayependezwa naye iweze kurejae nchini.
   
 8. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Jamani msiwe mnaota ndoto za mchana!
  Watanzania ni watu wavumilivu mnoo na uvumilivu wao hauna ukomo.
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  crapiest
   
 10. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda u-specify uvumilivu wa kitu gani? Lakini ukweli ni kwamba uvumilivu hasa wa shida una mwisho wake! Watu wameshachoka kuvumilia tabu za maisha zinazoletwa na JK na CCM yake na kama hatachukua hatua dunia itashuhudia ya Misri na Tunisia
   
 11. D

  Dopas JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani Jk alishinda? Japo ni kiongozi wa nchi lakini ni kwa kura ya wizi aliyoshirikiana na tume feki ya uchaguzi na usalama wa taifa.

  Any way hali halisi ndo hii, tukumbuke ni miezi miwili tu bada ya uchaguzi. Bado kuna miaka 4 na miezi 8. Kama uchovu umeingia kwa kasi sasa je hadi ifike walau nusu ya muda wake huyo bwana hali itakuwaje? Nadhani lawama za yote hayo sio kwa Jk, ila kwa wote waliopokea rushwa na kumrudisha yeye katika ofisi ambayo naamini asingepewa tena angeshukuru.

  Wapo wengi waliousaliti utu wao na mapenzi yao kwa nchi wakatanguliza matumbo yao, wakiwepo baadhi ya viongozi wa chama cha wafanyakazi waliofuta maandamano, sijui walishikiswa kitu? Kwa ujumla kilio cha watanzania kiwaendee wote waliopokea rusha ndogo na kubwa kutoka kwa CCM. Kwa upande mwingine ni vema pia wananchi waliovalishwa vitenge na kofia za ccm waone wenyewe kama wanakumbukwa kwa lolote. Wapo wengine walichangia kwa hili; baadhi ya wanamuziki wa kisasi kipya, baadhi ya waandishi wa habari, na wengine wengi tunaowafahamu waziwazi waliotaka hali hii ya leo itokee. Halafu eti wanalia pamoja nasi, wajionee aibu wenyewe.
   
 12. n

  nyantella JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wow here we go "Crap, Crapper, Crapiest" , life is so sweet!
   
 13. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  MwanaJF Ibange hapo penye red pana ujumbe-hivi unataka tuamini kwamba jk alishinda katika uchaguzi wa 31.10.2010???? Ukweli uko kwenye ripoti ya EU; hata ikitokea uchaguzi mwingine atatumia mbinu hizo hizo!! Wengi wanawaza ya Tunisia na Misri!!!!! Pole!!!!!!! Tanzania imevamiwa na UFISADI PAPA!!!!!!!!!! Hatima ni taifa kuangamia tu kwa sababu watu wake si kama watu wa Tunisia na Misri!!!!!!!!! Kule Tunisia na Misri kujitoa muhanga ni hali ya kawaida!!!!!!!!!!! Wabongo hawataki shida; wako radhi kwenda uchi lakini usiwaletee balaa-ingawa wa-Arusha ndiyo wana damu ya wana wa Mumbi across the border-labda hao, lakini oto waliowasha uko wapi????????? Mafisadi wamekwisha fanya utafiti na kujua jinsi ya kuwakalia na kuwatafuna wabongo-mbona Rostam anaendelea kutamba na kuendelea kuweka sisiemu na serikali yake mfukoni, nani anafyata mkia?????Pole sana Tanzania-ni mpaka Mungu aingilie kati na kuondoa roho ya woga inayotumiwa na majini ya sheikh kumlinda jk na kutawala nchi hii kwa roho ya hofu wakidhani ni wapenda amani!!!! Wazee wa hekima wana usemi kwamba HAKUNA AMANI PASIPO KUWEPO HAKI !!!!!!!!!!!! Sasa hivi ni dhuluma kila mahali mpaka bungeni waziri mkuu anadiriki kudandanganya taifa kwa mambo ambayo yeye mwenyewe anajua kuwa ni hatari ya kulipua bomu la machafuko nchini!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. m

  mzambia JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  :clap2::coffee::horn: KIKWETE ENDELEA TU ILI UWEKE HISTORIA TZ
   
Loading...