Kikwete: Utekelezaji wa ahadi zangu umeshaanza!

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
[h=6]"watatusema sana kila zuri letu kuwa baya ,tuendelee kutumia maoni yao mazuri kuijenga tanzania ya wote..,

Sasa mgao wa umeme umepungua sana,gesi inapatikana mjini kama nilivyohaidi ILI KUPUNGUZA MATUMIZI YA MKAA..,

Zile meli tatu zimeshawasili na SASA zinaungwa..,

Daraja la kigamboni na kilombero yanajengwa..,

Tunapunguza foleni Dsm kwa upanuzi wa barabara na barabara za juu kama muonavyo..,

Ahadi zangu zote ninazo na hakuna hata moja ambayo mpaka sasa sijaanza kuigusa hata ya matrekta ya bei nafuu ishafika, na hapa mbeya mnakumbuka niliahidi kutatua shida ya maji sasa leo nazindua mradi na maji..,

Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI.."

JAKAYA KIKWETE _ AKIZINDUA MRADI WA MAJI JANA-MBEYA.
[/h]
 
HAhahahahahahahahahahahahahahahahahahahhhhhhhhahhahahahahahhahahah duh!
 
Kwa hiyo anaongozwa na mawazo ya wapinzani,basi cdm chama tawala mabwepande wapinzani
 
Hotuba nzuri sana Dhaifu katoa! Hicho ndo kipimo cha kuweza kujua kama jamaa anazo au hanazo ..pesa! Hayo maji yalitakiwa yawepo tangu miaka ya 80, Hizo barabara ilishaongelewa sana lakini hela wanapiga tu! Na ahadi yao ya Kuwapungunza Wanyakysa kimyakimya hajaiongelea?
 
Suala la kuyatumia mawazo ya wapinzani kuijenga nchi yeye amelichukulia kama ni kuwakomoa wapinzani lkn ideally hvyo ndivyo inavyopaswa kuwa.Ayatumie mawazo ya CDM wafanyakazi na wakulima tupate maisha bora.
 
JK na maneno yake mie huwa nashangaa kabisa huwa anawaza nini for sure
 
Bei ya mazao pia asije akayakimbia,korosho,pamba ,aje miundombinu..kila kanda na mikoa,sio dar tu,aje sekta afya...asikilize matatizo yote,X ray hakuna hospitali karibu zote za wilaya,aje madawa......
 
Kwa nini haongelei Ufanisi wa mradi wa maji Dar?

Watu wako tayari kuwa na foleni hata miaka 5 mingine ijayo lakini wanahitaji maji leo tena saa hii.

Mgao wa umeme umepungua na mfuko wa Edward Lowassa unazidi kutuna.
Kwenye hotuba za bajeti kila mwaka,
mnaongelea kufuta tatizo la umeme,
kwenye utekelezaji,
mnaongelea mgao kupungua,
Lengo ni kufuta mgao Mr Dhaifu.

Haya lini Kigoma itakuwa Dubai ya Tanzania?????
Yale matrekta,pikipiki za kichina!
Ukweli ni kwamba wanaongeza skrepu za vyuma Tanzania
ili wakija kufungua viwanda vya kuyeyushia vyuma ziwe nyingi.
 
Nasikia na zile bajaj za kina mama wajawazito zimefika? Kigoma nayo ishaanza kuwa kama Dubai, Biharamulo ni Mkoa tayari, Maandalizi ya barabara za juu na chini yanaendelea. Kaazi kweli kweli!
 
Nasikia na zile bajaj za kina mama wajawazito zimefika? Kigoma nayo ishaanza kuwa kama Dubai, Biharamulo ni Mkoa tayari, Maandalizi ya barabara za juu na chini yanaendelea. Kaazi kweli kweli!

Usisahau Meli Ziwa Tanganyika, Nyasa, Victoria na ahadi nyingine kedekede
 
Mwanza alituahidi train ya umeme dar -mwanza 2hrs bado nakumbuka
 
hiyo ya daraja akiiweza itakua dili sana itakua ndio legacy yake kwamba chini ya utawala wake kigamboni walipata daraja no other president has even come close to doing so...na nasikia yuko busy anataka dili ya mtwara iwe up and running by 2015.. mzee anataka aache legacy...lakin akumbuke pia katika utawala wake watu wasio na hatia wameuawa, kuteswa na kudhulumiwa pasipo na sababu yoyote, ameshindwa kutatua migomo mbalimbali bt akifanya hata 80% ya ahadi alizotoa then BIG UP to him...
 
​wakipata misaada kama hiyo tanzania itakuwa paradise lakini ccm mipesa wao wanakula

Ile inayomlipa yaya wa hawara umeshaizungumzia? Anakula per diem kubwa kuliko manager wa kampuni yako.
 
Aseme ashawafunga mafisadi wangapi so far! - Mambo ya kesi kuwa mahakamani ni janja ya nyani.
 
Back
Top Bottom