Elections 2010 Kikwete utaongoza vijiji bila miji mikubwa?

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Kikwete atakua Raisi wa vijijini tuu? Ili Raisi uheshimike lazima uwe na support kubwa ya wasomi na miji mikubwa ya nchi yako, kinyume chake unakuwa Raisi kivuli. Tumezoea kuona kwenye nnchi za wenzetu zenye vurugu serikali ikitawala miji mikubwa na midogo hutawaliwa na wapinzani, ajabu hapa kwetu ni kinyume, kwa mara ya kwanza Raisi aliye madarakani anajua fika miji mikubwa yote yenye maendeleo haiko mikononi mwake, hii ni aibu.

Arusha Mjini, Jiji la Mwanza, Dar es Salaam, Musoma Mjini, Iringa Mjini, Mbeya Mjini, hii ni fedheha na tunafahamu fika hata kwingine mlibwagwa vibaya lakini umeiba. Unaongoza nchi ipi mheshimiwa Kikwete? unaongoza vijiji huku miji umewaachia wapinzania wako? Hii ni fedheha iliyoje, na bado tutakuadabisha kila kukicha. Ukienda Mwanza na ndege unafahamu fika ukitua tu uwanja wa ndege umekanyaga ardhi ya CHADEMA, Ukienda Kilimanjaro vivyo hivyo, Mbeya pia, Iringa Pia,Musoma nako. Kweli kidonge ni kichungu lakini inabidi ukimeze tu
 
Miji mingi Tanzania serikali za mitaa zitaundwa na CHADEMA pale ambapo pana mbunge wa CCM,MADIWANI WENGI NI WA cHADEMA.Nasikia hata Rostam atakuwa anaongozwa na madiwani wa chadema mwenye taarifa za uhakika za madiwani igunga atuletee
 
Kikwete ni rais wa Bushmen wasiojua nini maana ya maisha, yaani watu wanaoishi vichakani wasiojua ni kwa sababu gani wako duniani. Hawa watu hawajui maana ya maendeleo na isitoshe hawajui maendeleo yatawasaidia kitu gani. Kikwete akae akijua kuwa miji yote iliyochukuliwa na CHADEMA hana chake, hakuna cha majengo ya CCM wala viwanja vya CCM, vyote vilijengwa na wananchi kipindi cha chama kimoja hivyo ni lazima virudishwe kwa wananchi wote bila kupendelea. Ni lazima virudishwe serikarini. Kikwete kaa ukijua kuwa tunaanza na CCM KIRUMBA MWANZA, kisha tutaelekea SHEKH AMRI ABEID ARUSHA. Utakoma kipindi hiki Kikwete.
 
Kwa mtazamo wa ilikuwa bora MSH kuliko ARS, namaanishi Ndesa pesa na Mrema wa Maua, kwa sabab chama cha makapeto ndo kilikuwa kinaongoza Arusha mjina na Pinzani ndicho kilichokuwa kinaongoza Moshi Mjini. lakini tujiulize hapo kabla Kilimanjaro na Arusha ipi ilistahili kuwa jiji? Jibu ni kilimanjaro, japokuwa chama tawala kilijaribu kikishindwa kuifanya ARS kuwa ktk hadhi ya Majiji Africa, nina Imani kuwa kwa Sasa Inawezekana kwa sababu kuwa tumempata kiongozi mwenye hekima na mtazamo makini Godbless Lema. Tuwashukuru wananchi kwa kuweza kujua Good n evil!! Pale singida, Tanga, dodoma, pwani na mikoa ya jirani ,, wasubirie msoto wa miaka mingine mitano, wanasingida wanakumbuka walishikwa na njaa mpaka wakafikia hatua ya kula mizizi, hiyo hawakuina ni uzembe wa utawala mbovu..leo wamewachagua wale*2 walio washindisha njaa na kuwalaza njaa..


kama wanajamii tunasema viongozi makini ni wale wanaokubalika mjini na vijijini, but kama hukubaliki mjini (kwa wenye elimu) hata hao unaowaongoza huko vijijini ni bure kwa maana MJINGA hawazi kumwongoza MPUMBAVU an vice versa...
 
JK ni kiongozi wa wajinga,wale ambao hawajui raisi na uongozi wa nchi kwa ujumla wanahusika vip na kuzorota au kustawi kwa hali zao za maisha,wale wasiojua maamuzi ya kijinga anayofanya Jk na wenzie ktk kulipora taifa kuanzia kura hadi rasilimali.wasiouona utendaji mbovu wake,wale wasioona matumaini ya wao kustawi kimaisha ndio maana sehemu nyingi zenye maendeleo ya kiuchumi na kielimu wamemtosa kabaki na wale wasiojua wanafanya nini huku duniani wala hawajui serekali inatakiwa iwafanyie nini zaidi ya kofia,khanga na pombe kutoka ccm na kusubiri uchaguzi mwingine wapate hivyo hivyo.Na cha ajabu wao wanajua CCM ndio serekali,wanaamini bila ccm hakuna serekali.Hamjasikia kuna mama mmoja katika kupiga kura kadai aonyeshwe picha ya Nyerere?anagalia watu wanavyorudi nyuma kiakili kuliko matarajio yalivyo?
 
Back
Top Bottom