Kikwete usipozingatia haya ccm bye bye

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,275
391
Rais wangu Kikwete, na Mwenyekiti wangu wa chama cha Mapinduzi. Kwanza kabisa pole na mawazo, kwani najua ni wewe pekee unaeteseka na hali ya kisiasa na uchumi wa nchi yetu ilivyo sasa, hao uliowapa vyeo wanafurahia na kufikiria zaidi mambo yao binafsi bila hata kuwaza na kujali hatma ya watanzania masikini. Rai yangu kwako ni kwamba, kwa mambo yanayoendelea kila kukicha yanazidi kuleta mpasuko na kupunguza urafiki kati ya watanzania na ccm unayoiongoza. Naogopa itafika wakati ccm itakuwa na maadui nchi nzima kama ifuatavyo.
1. CCM tayari ilishaleta dhulma kubwa kwa wananchi wa pemba mwaka 2001, polisi na askari jeshi waliuwa raia kwa silaha, walichoma moto nyumba zao, kuna baadhi ya watu walishuhudia mama zao, dada zao na mama zao wakiuliwa ama kubakwa mbele ya macho yao, kwa dhulma hii serikali ya ccm haikuwahi kukubali kosa wala kuomba radhi wapemba na hivyo ccm kukataliwa moja kwa moja kisiwani humo

2. Kwa kutumia askari polisi hao hao, watu wa arusha wamepigwa mabomu, wameuliwa, wamedhalilishwa sana na kusumbuliwa kwa kufunguliwa kesi na serikali. Wakati serikali inatumia nguvu, chadema wanatumia siasa ya maneno kuzidisha hasira za wananchi dhidi ya serikali ya ccm, arusha ambayo ilikuwa ngome ya ccm imepoteza mvuto mjini hapo sasa

3. Kupitia polisi hao hao wamelipua mabomu na kupiga risasi tarime na kuua raia wasiokuwa na silaha. Wananchi wanazidi kuongeza hasira kwa ccm na serikali yake.
4. Askari hao hao wamepiga mabomu wazee wasiokuwa na silaha yoyote wazee wa A.mashariiki wanaodai mafao yao.

5. Serikali hiyo hiyo imepiga mabomu wanafunzi wa udsm zaidi ya mara tatu ndani ya awamu hii ya jk kwa issue ambazo zingepatiwa ufumbuzi kwa maneno rahisi tu.

6. Kwa jinsi spika wa bunge anavyoendesha mijadala Bungeni kwa kutumia attitude negative kwa baadhi ya wabunge, wabunge hao wanatumia udhaifu wake huo kumchochea ili avurugike kihisia na kufanya wananchi waone ccm wananatetea maovu na upinzani ndio uonekane unatetea wananchi
7. Wakati viongozi wa chadema wana uwezo wa kuwasilia online mda wote juu ya move za mambo muhim ya nchi na chama chao, ccm haina viongozi na wanachama wa aina hiyo, na kama wanao hao wachache basi hawana forums za kufikishia ujumbe au kupeana taarifa muhim kwa muda mfupi, hadi wakutane kwenye vikao vya kikatiba au kanuni za chama na jumuiya zao, kitu ambacho kinachelewesha utetezi wa baadhi ya hoja zinazohitaji utetezi wa haraka.
8. Viongozi wengi baada ya kupewa madaraka wanageuka kuwa mabosi, kuwapata ni shida, kuwafikishia matatizo ni ngumu, wanakuwa warasimu sana, na si watumishi wa watu tena. Wapinzani wanapokwenda kwa wananchi wnakuwa wanyenyekevu, rahisi kuwafikkishia kero, kero walizopewa wanasikika wakizizungumza, ccm inaongeza uadui kwa kutojibu majibu ya kuleta matumaini juu ya kero hizo hasa pale bungeni.
Haya na mengine mengi yanaongeza uadui na si wapenzi wa ccm siku hadi siku, na sumu inazidi kuenea nchi nzima
 
Nashangaa kama ni kweli wanayoyafanya polisi ni maagizo toka juu basi hatupo salama
 
Back
Top Bottom