Kikwete unawakumbatia wa nini? Mwema, Othman, Chagonja, Zoka?

kuna wengine wamempima kwa viatu- viatu alivyovaa ni vikubwa,tena sana-hata kutembea vizuri hawezi. yaani watanzania tumembebesha mzigo mtu ambae hana uwezo kabisa na huo mzigo, wala hawezi hata kufikiri mbinu za kumfanya aweze kubeba japo kidogo kidogo, full mzigo umemweka chini. angekuwa mzungu nafikiri angeshajiuzulu, ndio maana sana sana amebaki kutumia jeshi kama kinga yake, sumu ya udini, walio wa dini yake wasione huu udhaifu wamtetee n.k. mi naomba tu Mungu atufikishe salama hadi tutakapotua huu mzigo, maana yeye ndio amegeuka mzigo kwetu.
 
[COLOR=#ff0000 said:
FIRE THEM; KWANINI HAWAONDOLEWI?[/COLOR]
Kwanini wao wenyewe hawaondoki!!?

!

Yaan wewe ndio umepotea kabisa,tangu lini chizi akajichizisha?yaan huyo kumwambia awafukuze hao ni sawa na kumwambia na yeye mwenyewe ajifukuze,hapo cha kufanya ni kumuondoa huyo kiwete wenu ndio tatizo litakuwa solved,lakini umfukuze kibarua umuache fundi huo ni uonevu kabisa.
 
Mzee Mwanakijiji, kwenye historia ya Tanzania tawala zilizopita kabla ya Kikwete zimefanya ukandamizaji mkubwa sana dhidi ya raia wake, kuna rais yeyote aliyepita kuanzia Mwl Nyerere, Mwinyi, Mkapa ambaye aliwafukuza kazi wakuu wa uslama wa taifa kutokana na ukandamizaji wa raia.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni kwanini Rais Kikwete hataki kuamini kuwa timu yake ya usalama nchini inaliangusha taifa na haina maono mapya ya kusimamia usalama? Matukio kadhaa yaliyotokea nchini ndani ya mwaka huu peke yake yanathibitisha kubomoka kwa mfumo wa usalama. Kikwete amekuwa na watu hawa kwa karibu miaka sita sasa na matukio yaliyotokea chini yao ingekuwa nchi nyingine hawa wangekuwa wa kwanza kuondolewa. Hivi hadi nini kitokeeawa ndio atajua watendaji hawa wa vyombo vya usalama ni janga kwa taifa?

Hivi hadi aje kusikia kuna waziri kauawa au kundi la wabunge wametekwa nyara? Inawezekana vipi watu hawa wakaendelea kuaminiwa kusimamia usalama nchini wakati matukio ya kutisha na yanaendelea kutokea na sasa imefika mahali kwa kweli ni point of no return? Mwisho wa siku itabidi waanze kutumia mbinu za kimafya kwani mbinu za kawaida za kiusalama zimeshindikana! Wameshindwa na hawawezi tena!!

FIRE THEM; KWANINI HAWAONDOLEWI?
Kwanini wao wenyewe hawaondoki!!?

Mara nyingi tunalaumiwa kwa kukosoa tu na kuwa hatupendekezi nini kifanyike; well wafukuze hawa kwanza kama hatua ya kwanza halafu waingize watu ambao wanaongozwa na weledi na siyo urafiki au ujamaa na wewe! Au mtatuambia tusubiri kutoa maoni kwenye tume ya katiba mpya!

Nadhani kabla ya kukimbilia kufukuza viongozi, tujiulize kwa nini matukio haya yanatokea? kuna watu wako nyuma vurugu na mauaji haya hizi? PONDA, wanasiasa nao wanalo la kujibu kabla ya kukimbilia kuilaumu Serikali. Wanasiasa wanaotumia mbinu hizi kama njama za kujitwalia madaraka watambue kuwa hata azma yao ikifanikiwa nao wataishia huko huko.
 
Kama mpaka hapa tulipofika kama nchi halafu wewe huoni hoja ya hawa viongozi kujiuzulu,basi either ni mmoja wao
au una maslahi binfsi katika udhaifu wao huu kiutendaji.
hawa hustuka tu wanapoona bomu limetua ju ya paa lake na kuua watu kadhaa ndio huuona ubaya,na wakiuona hulalamika hao ambapo wakati huo hakuna wa kuwasikiliza usikauke sauti yako mkuu.
 
Hivi ni kwanini Rais Kikwete hataki kuamini kuwa timu yake ya usalama nchini inaliangusha taifa na haina maono mapya ya kusimamia usalama? Matukio kadhaa yaliyotokea nchini ndani ya mwaka huu peke yake yanathibitisha kubomoka kwa mfumo wa usalama. Kikwete amekuwa na watu hawa kwa karibu miaka sita sasa na matukio yaliyotokea chini yao ingekuwa nchi nyingine hawa wangekuwa wa kwanza kuondolewa. Hivi hadi nini kitokeeawa ndio atajua watendaji hawa wa vyombo vya usalama ni janga kwa taifa?

Hivi hadi aje kusikia kuna waziri kauawa au kundi la wabunge wametekwa nyara? Inawezekana vipi watu hawa wakaendelea kuaminiwa kusimamia usalama nchini wakati matukio ya kutisha na yanaendelea kutokea na sasa imefika mahali kwa kweli ni point of no return? Mwisho wa siku itabidi waanze kutumia mbinu za kimafya kwani mbinu za kawaida za kiusalama zimeshindikana! Wameshindwa na hawawezi tena!!

FIRE THEM; KWANINI HAWAONDOLEWI?
Kwanini wao wenyewe hawaondoki!!?

Mara nyingi tunalaumiwa kwa kukosoa tu na kuwa hatupendekezi nini kifanyike; well wafukuze hawa kwanza kama hatua ya kwanza halafu waingize watu ambao wanaongozwa na weledi na siyo urafiki au ujamaa na wewe! Au mtatuambia tusubiri kutoa maoni kwenye tume ya katiba mpya!

Watu wafanye vurugu makusudi halafu serikali ifukuze viongozi?
 
Mzee Mwanakijiji, kwenye historia ya Tanzania tawala zilizopita kabla ya Kikwete zimefanya ukandamizaji mkubwa sana dhidi ya raia wake, kuna rais yeyote aliyepita kuanzia Mwl Nyerere, Mwinyi, Mkapa ambaye aliwafukuza kazi wakuu wa uslama wa taifa kutokana na ukandamizaji wa raia.
kwa hiyo tatizo ni mfumo na kama ni mfumo basi ni ccm ndio yakuiondosha,kama nimekuelewa lakini.
 
Thubutu mjiuzulu nyie kwa kushindwa kulea familia wakati wa ujana sasa mnakimbilia ndoa za uzeeni. Mtajiju! TZ itasimama daima!
 
Lakini msisahau kuwa Mwana kijiji huko nyuma alipinga sana OTHMAN kuwa DG TISS soma hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/12174-rashid-othman-umeshindwa-jiuzulu-9.html

Nyingine hii hapa:
https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/169-rashid-othman-ndiye-boss-wa-usalama-3.html

naomba MODS muifunge hii thread kwa sababu naona haina tija kwani mleta hoja ana befu lake binafsi na TISS boss.

Kumbe chuki binafsi tu na uchu wa madaraka? baaaaaaas.
 
Mfumo wa Usalama ukivurugukika wa kulaumiwa sio vyombo vya Usalama pekee,

kuna mfumo wenyewe, kuna wana siasa, kuna wananchi wote wanapaswa kubeba dhamana hii. Hata Marekani ilipopigwa na Osama haina maana vyombo vyake ni dhaifu. Boko haram ya Nigeria haina maana Nigeria ni dhaifu kiusalama
 
anyways labda ningeomba nieleweshwe haya yafuatayo,
hivi mfano mpango wa kufanya fujo, kama ule wa mbagala ambao unatokea as a blink of an eye hapa polis inawezaje kuzuia? ama je mauaji ya L.B angewezaje kuyazuia? je polis wanawezaje kuzuia haya?

to me nilifikiri kwamba fujo ama uhalifu wa aina yyte ule mpaka kuwepo na ushahidi wa kiuteligensia unaoweza kthibitisha kutaka kutokea kwa fujo ama uhalifu huo halafu wakaingilia kudhibiti nje na hapo ni ngumu sana.

kwangu mm sioni kwanini watu hawa wafukuzwe kazi bali naona inawalazimu sasa kuongeza wigo wao hasa kwenye mambo ya kiintelijensia hasa kwa upande wa haya yenye vuguvugu la udini.
 
Lakini msisahau kuwa Mwana kijiji huko nyuma alipinga sana OTHMAN kuwa DG TISS soma hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/12174-rashid-othman-umeshindwa-jiuzulu-9.html

Nyingine hii hapa:
https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/169-rashid-othman-ndiye-boss-wa-usalama-3.html

naomba MODS muifunge hii thread kwa sababu naona haina tija kwani mleta hoja ana befu lake binafsi na TISS boss.
Mwanakijiji amerukia mbali badala ya kuutizama mfumo kiasi kwamba hata wakija wengine mambo ni yale yale.
 
Tunajuaje labda wanasiasa wameshauriwa kiusalama lakini hawashauriki? kuwaondoa viongozi wa vyombo vya ulinzi katika mazingira haya haitatusaidia tutakuwa tunatibu matokeo badala ya chanzo.

Ukitibu chanzo utakuwa umetibu mfumo lakini ukitibu matokeo utakuwa utoa kafara baadhi kwa kuwajibika kwa matokeo.
 
Back
Top Bottom