Kikwete, unasaka ukatibu mkuu wa umoja wa mataifa?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,875
2,000
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliuza kila siku kutokana na mwenendo wa Raisi wetu katika maswala mbalimbali ya kimataifa.Ukifuatulia kwa makini utagundua huyu mheshiimiwa ana-interest zaidi na maswala ya kimataifa pengine kuliko hata maswala ya kitaifa.

Kwa kifupi,Raisi Kikwete anaonekana kufanya juhudi kujijengea jina zuri na hata kukubaliki kimataifa na hasa mataifa ya Ulaya na Marekani.Pengine hii ndio sababu ya Raisi wetu kusafiri mara kwa mara hata pale ambapo angeweza kuwakilishwa na wasaidizi wake.

Pia,ni wazi utendaji wa Raisi Kikwete kimataifa ni mzuri ukilinganisha na utendaji wake kama Raisi wa nchi.Inawezekana kabisa akawa anaingilia hata majukumu ya waziri wake wa mambo ya nje.

Kwa kuangalia juhudi hizi nimejikuta najenga hisi labda bwana mkubwa kuna kitu anakitafuta katika anga za kimataifa na hapa anachotafuta pengine ni nafasi ya ukatibu mkuu wa umoja wa mataifa.Kwa mtu aliekuwa Raisi wa nchi nafasi pekee anayoweza kuitafuta kwa kufanya jitihada kubwa sana sana ni ukatibu mkuu wa UN na sidhani kama kuna post nyingine zaidi ya hiyo.

Ifahamike tu kuwa ukitataka kupata ukatibu mkuu wa UN ni lazima ukubalike na ufahamike kimataifa hasa katika maswala ya Diplomasia na zaidi mataifa makubwa yakukubali.

Ni mtazamo tu kwa kuangalia mazingira husika.

Time will tell!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom