Kikwete umetutukana waongea kiswahili, utuombe samahani, Pole wana UDOM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete umetutukana waongea kiswahili, utuombe samahani, Pole wana UDOM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gotolove, May 3, 2012.

 1. g

  gotolove Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku ya mei mosi mkuu wa kaya hukututendea haki Watangatanga aah sorry watanzania kumbe. Katika hotuba yake ndefu katikati yake uliongelea sana juu ya watu wanaosoma au waliosoma BA Kiswahili na BA English kwamba ni fani zisizo na ajira nchini na kwamba ndio watu wanaounda kundi la watu wengi wasio na ajira nchini. Rais alisema asilaumiwe kwa watu hao kukosa ajira kwani watu hao wanasoma masomo yasiyo na soko kwenye ajira.

  Alisema ukisoma ukisoma Kiswahili au kiingereza unaishia kuwa mkalimani tu na kwamba kazi kama hizo hazihitaji kuajiri watu wengi. Sipendi kuwakumbusha mengi lakini kwa waliosikia wanajua alichosema zaidi.

  Mimi nasema ametuzalilisha na kututukana kwani najua fani hizo wanasoma watu ambao wanapata mkopo wa Bodi ya Mikopo ambao unatokana na kodi za watanzania. Yeye kama rais pia ameidhinisha mikopo kwa wanafunzi wa kozi kama hizo.

  Kwanini ameziita fani hizo ukalimani tu? Je haoni pia kuwa amekidhalilisha kiswahili ambacho tunahangaika kukitangaza kwa wenzetu wanaojua maana ya uwajibikaji (Ulaya, Amerika, nk.)?

  Halafu nimekumbuka pia kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa kimoja kati ya vyuo vikuu nchini ni Prof wa Kiswahili. So mh president anataka kutuambia kuwa na huyo hakustahili kuwa pale? Atuambie maana mm najua kuwa ukimuacha VC, mmoja wa DVCs wa UDOM amesoma kiswahili . So rais aseme naye hastahili kuwa pale.

  Kwann UDOM wanaongozwa na mkalimani? Au ndio maana migogoro ya kiuongozi haiishi pale? Kuna watu wanaitwa Waswahili kutokana na kutumia kiswahili, je nao waanze kuona aibu? Wapo wanaotumia nguvu nyingi kupromoti kiswahili, waache?
   
 2. m

  maggy Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahaaa! ya ki Miss kwa ajili ya kuongea kwenye mashindano ya u miss lol!
  au wazee wa pwani
   
 3. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Imebidi ni sign in, aiseee, ss pale wanafanya nn hao BA KISW? Na yule prof wa kisw ambaye amewekwa kwnye fedha? Inabidi aangalie tena.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  acheni uchovu someni sayansi bana, komaeni...ona matusi haya!!
   
 5. l

  lemikaoforo Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unshangaa nini na ww,yeye aliyesoma uchumi kusaidia nini tz,genttleman degree yake inmtosha yeye haiwezi kumsaidia mtz yeyote labda kwenye ngoma ya mdundiko
   
 6. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo hawastahili mkopo?
   
 7. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Kikwete ameutukana utaifa wake...
   
 8. luck

  luck JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 771
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  Kama rais aliongea hivyo mimi sioni matusi wako wapi hapo.
  Tatizo watanzania tunapenda kudanganywa tunapenda kuambiwa kile tunachoka kukisikia!.Hilo alilolisema ndo ukweli wenyewe!

  Tatizo mtu akisema ukweli anaonekana mbaya.Hiyo ni changamoto kwa wazazi wahimize watoto na vijana wao wasizikimbie numberz! Na nafikiri english medium ndo chanzo kikubwa cha haya yoooote! Watoto kutwa kucha wanajifunza lugha tu!
   
 9. N

  Nekanache New Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilitegemea kama kiongozi angeeleza mikakati gani ameweka ya kucreate ajira katika maeneo hayo! Kama vijana wakilalamika, na kiongozi akalalamika,nani anamsaidia mwenzie?
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kama umesoma Kiswahili, njoo nikupe kazi ya kutunga mashairi.
   
 11. C

  Cape city Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yupo right president...angalieni coz za kusoma kwa wakati uliopo...
   
 12. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  shemiji yake mlacha prof. kasoma nini vile?
   
 13. A

  Andrew Jr JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Labda hakuna uhusiano kati ya kiswahili na fedha
   
 14. s

  sugi JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Kwani humu jf kuna watu waliosoma BA kiswahili?
   
 15. b

  bigmukolo Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimesikitika sana mi nimesoma ba kisw ling na mkopo juu af nakuja kuambiwa hakuna ajira da!...tz maendeleo ya kisw hayawezekani
   
 16. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  Kiswahili,kingereza tanzania utata mtupu. Bila walimu walio hitimu BA za lugha nani atafundisha lugha hizi sekondari?
   
 17. Nelsweeter

  Nelsweeter Senior Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu hampendi ukweli, habari ndio hiyo, labla mkawe wakalimani kwenye mihadhara ya dini, ila Kiswahili si dili tena kwani hata ukalimani unahitaji uwe competent na lugha zaidi ya moja
   
 18. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  jamni mi nimesoma biashara ila napingana na hii hoja..mbona tanzania tunapeleka walimu wa kiswahili nchi mbalimbali kama lubya,miari,ujerumani marekani na china au mmesahau hii lugha siku hizi inatumika hadi umoja wa mataifa...mkataa chao mtumwatupende vyetu bana ...unaambiwa chuo irani washafanya mtihani mmoja na havard wa science na wanafunzi wa iran waliongoza...tukikuze na kukithamini lugha yetu..ama mnataka kenya watuzidi
   
 19. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ninavyojua mimi! wanaosoma
  Ba education, b.education ndio wanaoenda kutufundishia wanetu!
   
 20. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hata hivyo kusema hivyo ni ubaguzi wa wazi kabisa,ambao hata Heslb wanaendelea kuufanya.Sote tu watanzania,ya nini kusema wa sayansi nampa mkopo na arts hapati? Ulitoa ujumbe huo tangu akiwa darasa la kwanza? Au wanaibuka sasa? Ni ubaguzi na zinahitajika juhudi za kuupinga!
   
Loading...