Kikwete;Ujamaa,Kujitegemea na Azimio la Arusha ni Imani Yetu, bila Matendo ni Bure!


Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,494
Likes
394
Points
180
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,494 394 180
Mh. Kikwete,

Wakati unagombea Urais kupitia ndani ya Chama Chako n hata kwa Taifa zima, ulijiuza kama muumini mkamilifu wa TANU na CCM pamoja na Itikadi zake na kuwa wewe ni muumini na mtifu kwa Imani za Kijamaa za CCM.

Nasi kama Wanachama wa CCM ambao ni waamini wa Ujamaa na Azimio la Arusha, tukakuchagua kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama chetu CCM.

Nao, kama Watanzania na Taifa ambao pamoja na kuwa si wanachama wa CCM, lakini ni waumini wa Sera za Ujamaa, Itikadi zake na Azimio la Arusha, kwa nguvu za Asilimia 80, wakakupa kura, kuthibitisha tulichokiamua sisi WanaCCM na kukupa dhamana ya kuwa Rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ujamaa na Kujitegemea ni dini ya Watanzania. Azimio la Arusha na mafundisho mengine yote kuhusu Taifa letu na Imani yetu uliyotupa Umoja, Mshikamano na Amani tunayoifurahia, ni matunda ya sisi kuwa Waumini wa dini yetu.

Sikatai, bado tuna safari ndefu kufika katika utimilifu, na katika safari hii, kuna majaribu mengi na vikwazo vingi na ndio maana bado hatujaweza kuufikia Ujamaa kamili na baadhi yetu wameanza kupotoka Imani na kubadilisha dini.

Sasa swali langu kwako, je ni lini ulikata SHAURI na kuachana na dini yetu? Je ulipokuwa unajinadi ulikuwa unatulaghai kumbe mwenzetu ushabadili dini?
 

Forum statistics

Threads 1,237,691
Members 475,675
Posts 29,297,649