Kikwete: Uamuzi wa Dodoma kuwa Makao Makuu na Ujenzi wa Ikulu haukuwa wa mtu mmoja!

Kikwete n Rais anayependwa kuliko wote hii haipingiki n mtu mwenye nyota ya watu ILA KWA RAIS Magufuli atabaki kuwa Rais bora kuwahi kutokea na mwenye uthubutu mkubwa ambaye hajatokea Tanzania vitabu vitamwandika na atakuja kukumbukwa milele
jpm hana ubora wowote!sijaona alichofanikisha kwa watz hata kimoja!!narudia hata kimoja!kuwa nae ni hasara kwa taifa hili!miradi yote ilishakuwepo tangu kikwete yupo madarakani hata mimi ningemalizia miradi yote!!!
 
Kwanza shukurani sana kwa kukumbuka maneno yale. Sikutegemea kama kuna watu wanakumbuka.

Nilisema vile kwa kuangalia kwamba kila utawala mbovu unavyokuja, unashusha standards za commonly accepted behavior. Wanaofuata wanashusha zaidi.

Hebu fikiria uje upate rais Makonda au hao watu wa caliber yake.

Tutarudi kulekule kusema "bora hata Magufuli".

Siyo kwa sababu Magufuli ni mzuri sana.

Bali kwa sababu quality ya uongozi ikizidi kushuka, hata mbaya anaonekana afadhali akilinganishwa na mbaya zaidi.
Mkuu kwa maoni yako unadhani ni nani ambaye anafaa kuwa raisi ambaye ana sifa za uongozi kama. Ulivyowahi kuandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa maoni yako unadhani ni nani ambaye anafaa kuwa raisi ambaye ana sifa za uongozi kama. Ulivyowahi kuandika

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo moja kubwa, ni la kimfumo. Niliwahi kulisema hili, na nalirudia.

Tumejiwekea mfumo ambao, ili upande juu na ujulikane katika ngazi ya taifa, ni lazima ukubali kuwa muongo, mtu wa figisu, ukubali kupelekwapelekwa na walio juu yako kama mjinga.


Kwa hivyo, utakuta, watu wanaofaa, kwenye mfumo huo hawawezi kustawi. Na watu wanaoweza kustawi katika mfumo huo, hawafai.

Baba yangu aliombwa kugombea ubunge. Akasema ngoja niombe sala nipate muongozo kutoka kwa Bwana Yesu (Mzee wangu ni mtu wa dini sana).In a complex way, he was weighing the moral questions using the scale of religion.

Mwishowe akaja kusema kwamba hajapata kibali kugombea ubunge. Hususan kwa sababu kampeni za ubunge zingehusisha rushwa na uongo mwingi sana. Zingehusisha siasa za majitaka sana. Yeye alitaka kuishi maisha safi bila figisu zote hizo. Bila siasa za majitaka. Bila kupangiwa uongo wa kusema na mabosi wa chama.

Sasa mtu kama huyo mwenye integrity yake, anafaa kuongoza. Lakini, katika mfumo wetu, hizo qualities zinazomfanya awe na potential ya kuwa kiongozi mzuri, ndizo hizo hizo zinamfanya asiweze ku advance kwenye uongozi.

Kwanza kugombea ubunge tu unatakiwa utumie hela nyingi sana. Jambo la uongozi linakuwa kama biashara.

Litatokea dili la kula hela chafu za rushwa ili zisaidie chama kwenye kampeni, yeye atakataa, ataonekana mshamba. Atatengwa.

Granted, hakuna mtu safi 100%. Lakini uchafu unaotakiwa uupitie ili uwe kiongozi wa kisiasa wa kitaifa Tanzania ni mwingi sana, kiasi cha kuku disqualify ukiwekwa kwenye mizani.

Kwa hivyo, kwa sasa, walio juu, hata kama wanajitahidi, wameshindwa mtihani wa kusimamia integrity yao.

Juzi kuna kisa kimetokea Uingereza, kuna Junior Minister kajiuzulu. Kisa nini? Kuna msaidizi wa Prime Minister Johnson alikuwa anawaambia watu waji quarantine kila siku, yeye mwenyewe kasafiri mbali tu bila kuji quarantine. Kibaya zaidi, PM akawa anamtetea. Huyu Junior Minister akaona huu upuuzi, nikiendelea kuwa kwenye serikali itakuwa nakubali ujinga huu. Sitaki jina langu lihusishwe na uozo huu. Akajiuzulu.

Tanzania nani kajiuzulu kwa kupinga maamuzi ya serikali ambayo hajakubaliana nayo? Ina maana mawaziri wote wanakubaliana na maamuzi yote muhimu ya serikali?

So, to answer your question, kwa sasa, na hili si chama tawala tu, hata upinzani. Upinzani hatuoni sana haya mambo kwa sababu hawana dola, lakini kwa level yao na wao tunaona yale yale.

Tatizo ni hili.

Kwa mfumo wetu.

Wanaojulikana hawafai.Ili ujulikane lazima uwe compromised kwanza. Ukiwa compromised, maana yake hufai.

Wanaofaa, hawajulikani. Kwa sababu, ili ujulikane, inabidi uwe compromised. Na hawa walikataa kuwa compromised. Hivyo hawajulikani.
 
Jk ndie Rais pekee alietokea 'kijitonyama', jeshini, chamani na mtaani.

1982 Baba yake Mzazi aliandika barua kwenda kwa Mzee Kawawa kulalamika kwanini mwanae anahamishwa hamishwa sana 1974~1982 alishafanya kazi Nachingwea, Singida, Tabora, Znz na Dsm, akajibiwa Mzee Tulia, Nchi inaanda Viongozi wa baadae

Akiwa Kijana mdogo 1982 ndio alipewa Jukumu na Amiri jeshi kuchoma madokezo yote ya maelekezo ya vita ya Kagera na alifanya kwa uadilifu ndio sababu hadi leo hatuna 'behind the scene'ya Vita ya Kagera

Jk Ni mwanasiasa hasa, pia anaijua historia ya nchi Na chama pia vizuri.Kiujumla ametulia
 
JPM ni mtu wa kazi, Kabudi na Dr Mpango wanamjua , akihisi we ni Mpumbavu anakuchana, akihisi Mwizi anakwambia


Sasa fikiria Jk akiwa Amiri jeshi alifikia hatua hadi Mtunza Sauti anamchukulia poa
JK ni mtu wa kupiga madongo live ila utakuja kuelewa baadae kwamba kumbe alinipiga DONGO tofauti na Vijembe vya "MTU FURANI" analenga hapo hapo na ni Direct.
 


Heshima kwenu Wakuu wangu,

Leo Taifa tumeweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.

Ikulu ambayo itafanana na ile iliyopp Dar Es Salaam kwa kila kitu hadi upana wa ngazi. Tofauti ni moja tu kwamba ile ya Dodoma ina underground.

Lakini katika waliohutubia, Makongoro Nyerere na Jakaya Kikwete ndo wamefanya watu kusahau machungu ya maisha na hasira za Corona kwani wamechangamsha Ukumbi japo hata ambaye hakucheka alitabasamu kwa furaha.

Rais Mstaafu Kikwete alipo simama kuhutubia alianza na neno "Mambo"? Nikaona kila mtu hata wale Maafande wa JKT wanaojenga Ikulu wakavua kofia na kuepeperusha hewani kwa shangwe na Vifijo.

Kwenye hotuba ya rais Mstaafu Jakaya Kikwete nimegundua hili:

1. Kikwete ameshangiliwa sana na vijana wa JKT kuliko rais yoyote mstaafu

2. Kikwete amezungumzia kuwa Mwalimu hakuamua tu Makao Makuu yahamie Dodoma yeye mwenyewe, Ulikuwa ni uamuzi wa kidemokrasia na uamuzi shirikishi. Hapa aliweka msisitizo wa uongozi shirikishi na demokrasia (collective decision-making)

3. Alieleza uamuzi wake kuwa Makazi ya Rais na ofisi zijengwe Chamwino. Mawazo ya zamani ni kuwa Ikulu ijengwe Chamwino halafu ofisi ya Rais iwe Chimwaga, hiyo isingekuwa salama Rais asafiri 40km kila siku kutoka Chamwino kwenda Chimwaga na kurudi. Hii imedhihirisha kuwa uamuzi wa kuhamia Dodoma ni mchakato ambao kila Rais alikuwa na mchango wake, siyo maono ya kiongozi mmoja peke yake.

========
Rais mstaafu Jakaya Kikwete asema kuwa anashukuru kwa kualkwa kushuhudia tukio la kihistoria ,ndoto zimetimia, amesema mwaka 1971chama cha TANU kiliamua makao makuu yahamie Dodoma na ni uamuzi uliofanywa kudemokrasia ni uamuzi shirikishi.

Baada ya kutokea hilo vuguvugu la kwamba kujengwe makao makuu katikati mikoa iltakiwa kwenda kutoa maoni na mikoa mingi ikakubali karibu yote na mkoa mmpja ulikataa ambao ni mkoa wa Pwani.

Amesema mkoa uliokataa ni mkoa wa kwao ambao ni mkoa wa Pwani na amesema isingekuwa rahisi kukubali kwa kuwa walikuwa wanatoa makao makuu kwao na kupeleka Dodoma kwa watu wengine.

Amesema ni kama vile Bagmoyo walivyosikitika wakati ule wa mjerumani walipohamishia utawala Daresalaam, amesema wakati mjerumani anatawala alikuwa anatawala kutokea Bagamoyo na ndio maana jengo la Bagamoyo lile kubwa linafanana na jengo la ikulu lakini kwa kuwa walikuwa wanataka bandari
wakaamua kuhamishia Dar es alaam.

Amesema kuwa wazo lilikuwepo wakati wa baba wa Taifa akachagua Chamwino akajenga ikulu na wakati wote wazo lilikuwa makao makuu Dodoma lakini dizaini walioitayarisha ya makao makuu ya ikulu ni pale juu Chimwaga yakajengwa makao makuu ya chama lakini pia ilikuwa ikulu inajengwa pale.

Akaendelea kusema kuwa yeye alipokuwa Rais alifanya uamzi kuwa wanataka kujenga chuo kikuu kikubwa kuliko vyote Dodoma na uamuzi huo haukuwa wa kudemokrasia maana watu walikuwa wanasema mara tujenge Mwanza mara wengine tupeleke Dodoma wengine Mtwara mara wengine Mbeya ndipo yeye akafanya maamuzi kama Rais kuwa watajenga Dodoma.

Lakini sasa wataanza vipi akasema waanze palepale kwenye jengo lile ambalo chama kinalitumia kila baada ya miaka mitano na hakuna mtu anayetumia na uzuri lilikuwa lishauzwa kwa serikali baada ya kuingia kwenye vyama vingi.

Baada ya uamuzi ule palipokuwa panatakiwa kujengwa makao makuu ya serikali ndipo pamejengwa chuo kikuu na ikulu lazima ijengwe Dodoma. Ndipo Rais mstaafu Kikwete akawambia ikulu itajengwa Chamwino ikaja mjadala lakini makao makuu inatakiwa kuwa Dodoma na Chamwino ni nje ya Dodoma akajibu kuwa Dodoma ni jina tu na Rais anaweza kuamua kuwa hapa pote kuwa ni Dodoma.

Akaamua kuwa hapo iwe manispaa na kwa mzee Marechela pakawa manispaa akasema Rais atakuwa anakaa Chamwino ikulu yake ikajengwe Chimwaga, huyo Rais atakaye kuwa anatembea kila siku asubuhi kilomita karibu 40 akaona sio salama hivyo akasema ikulu yake ikajengwe kulekule Chamwino.

Na baba wa taifa aliamua kuwa ikulu ijengwe palepale Chamwino na mipango ikaanza, na majengo ya wizara yajengwe kuzunga ikulu na sasa wamepata mtu ameifanya mipango kuwa matumizi '' Hongera sana mh. Rais, Rais nakupongeza sana uamuzi wa kujenga ikulu ni uamuzi wa busara na wa hekima''

Aliendelea kusema kuwa anaungana na wengine kupongeza na viongozi wa dini jambo hili likamilike kama ilivyokusudiwa na kama mh. rais alivyokudia na ameshangaa maendeleo kwa mambo mengi yaliongezeka na majengo mengi yaliyojengwa.

Aliendelea kusema kuwa amefurahi sana kwa kuzawadiwa ndege aina ya tausi maana alikuwa nafikiria kwenda kwa mh Rais kuomba ili akawafuge kwake Msoga. lakini amepewa kabla hajaomba hivyo amefurahi sana, na amemuomba mh. Rais ampatie masaada wa ujuzi wa kuwafuga ili wasije kufa kwa kukosa matunzo bora.

Raisi Kiwete ni mwanajeshi,sasa ulitegemea wanajeshi wenzake wafanye nini_
 
Maneno ya Kikwete watu wanayatia chumvi sana na kuyapindisha kwa sababu zisizoeleweka. Yeye alitaka kukumbusha kuwa uamuzi wa kuhamia Dodoma ulikuwa ni wa nchi nzima siyo matakwa ya Nyerere tu, na kutaka kuonyesha kuwa yanayofanywa sasa kuijenga Dodoma yanatokana na uamuzi huo.

Hata kama anataka kupiga madongo, yeye ni diplomat ambaye hawezi kufanya hivyo majukwaani. Kuna wakati watu waliwahi kupindisha maneno yake ikabidi ajitokeze tena kuwasahihisha wapotoshaji; mnaopindisha maneno ya Kikwete mtaweza kumfanya ashindwe kuwa anaongea tena.
 
Nimefurahi kusikia akikiri kwamba Pwani hawakuunga Mkono wazo la Ikulu kuhamia Dodoma hakika nimefurahi sana nadhani kweli walikuwa na hoja maana Ikulu ya Kwanza ilikuwa Bagamoyo ikahamishiwa Dar es salaam na baadae Pwani ikatengwa kutoka Dar.
 
Kwa upande mwingine, unapoona mtu kama Trump alifanikiwa kuwa Rais na kuendelea kuwa licha ya kashfa nyingi zilizomwandama baada ya kuteuliwa, ndipo mtu unapoweza kuhitimisha - hakuna mfumo wa kiutawala uliothabiti na hata kuwa mfano.

Hebu fikiri tu kwa mtu kama Boris Johnson kuwa PM , ama kwa Putin kuendelea kuwa Rais wa kudumu... Lililo bora na nono kwa huyu, kwa mwingine sumu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wamekulia katika mazingira ambayo yamekuwa na kitu ambacho naweza kukiita "worst psychological torture". Kwa hiyo amekuwa psychologically tortured kiasi kwamba baada ya kuwa wamekua na kupata elimu, ndiyo wameharibika zaidi.

Mtu ana undergo "negative education" kiasi kwamba anapozidi kuongeza elimu, ndiyo anazidi kuharibika zaidi anakuwa afadhali alivyokuwa awali kabla hajaongeza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom