Kikwete: Tutawajibu wanaotusema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Tutawajibu wanaotusema!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SHUPAZA, Dec 7, 2009.

 1. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na Sadick Mtulya

  RAIS Jakaya Kikwete jana alirejea nchini akitokea Cuba na kujibu mapigo ya makada mbalimbali wa CCM wanaomtuhumu kushindwa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema anajipanga kujibu tuhuma dhidi yake kuwa anashindwa kufanya maamuzi magumu ambazo zilitolewa na makada mbalimbali wa CCM, wakiwemo mawaziri wa zamani.

  Lakini Kikwete alidokeza majibu yake kwa kusema:
  "Japokuwa ndio kwanza ninafika, sishangazwi na yote mabaya yaliyozungumzwa dhidi yangu katika kongamano hilo. Ningeshangazwa kama ningesemwa vizuri."

  Jakaya, ambaye alikuwa anarejea kutoka ziara ya takribani wiki mbili kwenye nchi za Jamaica, Cuba na Trinidad na Tabago ambako alihudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, alisema hatishwi na maneno yaliyozungumzwa kwa kuwa watu waliozungumza wanajulikana wanatoka upande gani.

  Katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Rais Kikwete alishutumiwa kwa kutochukua hatua madhubuti dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na kukiacha chama kikipoteza mwelekeo na kutekwa na matajiri wachache.

  "Japo bado sijapata taarifa vizuri kuhusu yote yaliyozungumzwa katika kongamano hilo; siwezi kushangazwa sana, lakini ninakwenda kupata taarifa kamili na kujadiliana na wenzangu kisha nitajibu mambo yote yaliyokuwa na maana na yale ambayo hayana maana na yaliyosemwa kwa chuki, tutayapuuza tu," alisema Rais Kikwete.

  Rais Kikwete alisema hashangazwi na hali iliyotekea kwa kuwa binadamu wanatofautiana kimtazamo, lakini akasisitiza kuwa anachojali zaidi ni dhamana aliyonayo kwa umma.

  "Kama nilivyosema kuwa nimedokezwa kidogo tu, lakini naomba muelewe kuwa huwezi ukamridhisha kila mtu kwani binadamu wamegawanyika katika sehemu tatu," alisema.

  "Asilimia 15 watakupenda, asilimia 15 nyingine watakuchukia na asilimia 70 iliyobaki watabaki wanaangalia upepo unaelekea wapi hivyo tusubiri kuna maamuzi tutafanya," alisema Rais Kikwete.

  Katika mkutano huo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, waziri wa zamani wa menejimenti ya utumishi wa umma, Matheo Qares alisema iwapo rais atashindwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi kabla ya 2010, CCM haina budi kumtosa na kumteua mgombea mwingine wa urais.

  Naye waziri wa zamani kwenye serikali ya awamu ya pili, Mussa Nkangaa alisema CCM sasa imetekwa na wafanyabiashara matajiri na kuachana na sera zake za kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, ndio maana imekuwa vigumu kushughulikia mafisadi.

  Katibu mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula, katika mahojiano na Mwananchi, alisema tatizo la kupeana uongozi kwa urafiki limefanya taifa liwe na viongozi wasio na sifa na kusababisha mambo yanayoendelea kutokea sasa ndani ya chama hicho kikongwe.

  CCM inaonekana kuwa katika hatari ya kuparaganyika kutokana na kuwa na makundi ambayo yanarushiana tuhuma kila kukicha. Tuhuma hizo zimekuwa zikitolewa kwenye mikutano ya Bunge na hivi karibuni zilihamia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu na baadaye mkutano wa kamati iliyoundwa kuchunguza mfarakano huo, maarufu kama Kamati ya Mwinyi na wabunge kilichofanyika Dodoma.

  Kikwete, ambaye pia amekuwa akishutumiwa kwa kufanya safari nyingi za nje zinazokula fedha za walipa kodi na huku akishindwa kutulia nyumbani kutatua matatizo mengi yanayoikabili nchi kwa sasa, alitetea safari hizo akisema ni vigumu kwake kuacha safari hizo kwa kuwa hazina mbadala.

  Na kuonyesha kuwa hawezi kuziacha, Kikwete akaongeza:"Na wiki chache zijazo ninatarajia kwenda nchini Denmark kuhudhuria mkutano wa Capenhagen."

  Ikulu pia iliwahi kutoa taarifa ya kutetea ziara hizo ikisema kuwa zina manufaa kwa nchi kwa kuwa Rais Kikwete huenda nje kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo. Ikulu ilitoa kauli hiyo baada ya wananchi kulalamika kuwa fedha nyingi hutumika kwenye safari hizo.

  Kikwete anatarajia kuongoza msafara wa watu takribani 60 atakapokwenda Copenhagen kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

  Kuhusu hali ya afya yake, Kikwete, ambaye alizidiwa nguvu jukwaani mjini Mwanza kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kufanya safari ndefu bila ya kupumzika, alisema yuko salama lakini anatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya.

  "Nilipokuwa huko nilipima afya yangu na hasa akili na mishipa ya damu na wataalamu wakaniambia nipo salama. Ninatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya," alisema Kikwete. Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa hali yake ni salama wataalamu wamemshauri kupunguza ratiba za kazi za kila siku.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tanzania: God May Be On Kikwete's Side, the Rest Are Crossing the Street
  Jenerali Ulimwengu
  7 December 2009

  http://allafrica.com/stories/200912070714.html
  opinion

  Nairobi - It must take great insouciance for someone in President Jakaya Kikwete's position to sleep well at night these days, but if the man is even slightly worried, he's not showing it.

  The Tanzanian chattering classes are clearly growing more and more restive as times passes, with too many people now saying out loud that the country is in a state of drift, that it lacks leadership.

  Were these sentiments being expressed by the official political opposition or the media, they would amount to little, seeing as it is the habit of the opposition to, well, oppose; and as for the media, what can one say of them?

  But misgivings are now to be heard from unexpected quarter, such as the clergy -- not habitually given to outspokenness -- ruling party stalwarts and the proverbial man in the street.

  When, a few months ago, the Catholic Church issued a document urging the faithful to shun corrupt politicians and to choose graft-free leaders, a hue and cry arose in some quarters in government, alleging that this was a case of blatant church interference in politics.

  Indeed, if one had seriously wanted to castigate church leaders for poking their noses into politics, one could have pointed out that, in 2005, at the height of the electoral campaigns, a senior cleric stated, ex cathedra, that Kikwete was God's own choice for president.

  Obviously the earlier statement was agreeable to ruling circles because it guaranteed a few extra votes, though nobody seemed to worry about God's reputation should Kikwete eventually disappoint.

  Last week, a seminar organised by the Mwalimu Nyerere Foundation became another forum from which the president's performance was pilloried, with participants, among them senior ruling party people, pulling no punches.

  Joseph Butiku, chief executive of the Foundation, and erstwhile senior aide to the late Mwalimu Nyerere, called on the president to free himself from the grip of "thieving" business people and provide proper leadership.

  Similar calls were made by other participants in the three-day seminar moderated by Salim Ahmed Salim, chair of the Foundation.

  It has been suggested that the deliberations at the seminar be allowed to percolate to the grassroots, where "real Tanzanians" grapple with the grim realities of daily sub-dollar existence.

  A national conference has also been mooted to craft a national consensus and vision for the future.

  The leadership of the ruling party itself looks increasingly at odds, constantly at each other's throats and with so many factions it's surprising it is still holding together.

  The only reason such a quarrelsome crowd has not completely fallen is the access it still has to government, very useful as a source of both largesse and sanction.

  Even some of Kikwete's immediate lieutenants, at various informal gatherings in Dar es Salaam, do not seem to mind who hears them say how ineffectual he is as a leader.

  He has also appeared ineffectual in dealing with the crisis in Zanzibar, so that when Seif Shariff Hamad of CUF and Zanzibar President Amani Abeid Karume decided to bury the hatched the other day, it was not clear whether the Union president had been involved or even informed.

  This on an issue he had earlier promised to handle personally.

  The president of Zanzibar -- whose ascent to the Zanizibar presidency nine years ago owed everything to CCM's pays political machinery -- nowadays pays visibly scant attention to Kikwete, skipping Cabinet meetings and other important events without explanation.

  The media, civil society and the man in the street are calling on the president to cut back on his frequent foreign trips both on account of the expense involved and the need for him to spend more time solving domestic problems instead of acting like he was the foreign minister, especially now that a real threat of famine looms in many parts of the country.

  Jenerali Ulimwengu is a political commentator and civil-society activist based in Dar es Salaam.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kheeee chuki binafsi???kazi ipo
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  haaaaaaaaaaaaaaa Rais wetu huyo si bora angeendelea kumwomba Makamba amjibie
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kikwete nae akili zake kama za Zitto Kabwe!
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Makamba naye naona amegundua kuwa anafanywa "KATIKILO"
   
 7. R

  Ronaldinho Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Wana chuki na wivu",hii mipasho ilifaa ampe sofia simba aiimbe
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hahahaha,

  Halafu Sophia Simba akisema hivi watu wanakuwa deluded kwamba kasema mwenyewe bila kutumwa/ kupewa baraka na Kikwete.

  Ulimwengu anakwambia the only reason CCM ipo kama chama kimoja sasa hivi ni the fact that wanashikilia largesse ya serikali.
   
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Sikio la kufa haliskii dawa majameni eh
   
 10. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hahaha huwa nikiwa nataka kucheka najaribu kuingia jf maana watu humu wako na character za aina mbali mbali kutokana na majibu yao mweeh!.....it is very restaurante!....LOL!
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  NB:
  - Naona hapa ameongea kama aliyeingia madarakani kwa kufanya mapinzuzi vile. Kutoka 85% waliompenda hadi 15% na wafukuza upepo 70%

  _ Hii kupenda kusafiri hata kabla hajatatua hili ni kweli kuwa linatokana na kula miguu ya mtetea wa keinyeji?

  - Ni kweli kuwa sikio la kufa halisikii dawa? kelele zilizokwisha masikioni kuwa misururu ya rais ni mikubwa kupita kiasi bado haisikii au ndio kuwa ni kula nchi kwa kwenda mbele? Fikiria kwa mataifa 195 duniani kama kila moja likipeleka Denmark watu 60 kama msafara wake, basi huo mkutano utakuwa na watu 11,700. Jamani huwaga tunajipima kulingana na uwezo wetu?

  === Sijui, labda ni chuki binafsi==
   
 12. l

  lukule2009 Senior Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na Sadick Mtulya

  RAIS Jakaya Kikwete jana alirejea nchini akitokea Cuba na kujibu mapigo ya makada mbalimbali wa CCM wanaomtuhumu kushindwa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema anajipanga kujibu tuhuma dhidi yake kuwa anashindwa kufanya maamuzi magumu ambazo zilitolewa na makada mbalimbali wa CCM, wakiwemo mawaziri wa zamani.

  Lakini Kikwete alidokeza majibu yake kwa kusema:
  "Japokuwa ndio kwanza ninafika, sishangazwi na yote mabaya yaliyozungumzwa dhidi yangu katika kongamano hilo. Ningeshangazwa kama ningesemwa vizuri."

  Jakaya, ambaye alikuwa anarejea kutoka ziara ya takribani wiki mbili kwenye nchi za Jamaica, Cuba na Trinidad na Tabago ambako alihudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, alisema hatishwi na maneno yaliyozungumzwa kwa kuwa watu waliozungumza wanajulikana wanatoka upande gani.

  Katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Rais Kikwete alishutumiwa kwa kutochukua hatua madhubuti dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na kukiacha chama kikipoteza mwelekeo na kutekwa na matajiri wachache.

  "Japo bado sijapata taarifa vizuri kuhusu yote yaliyozungumzwa katika kongamano hilo; siwezi kushangazwa sana, lakini ninakwenda kupata taarifa kamili na kujadiliana na wenzangu kisha nitajibu mambo yote yaliyokuwa na maana na yale ambayo hayana maana na yaliyosemwa kwa chuki, tutayapuuza tu," alisema Rais Kikwete.

  Rais Kikwete alisema hashangazwi na hali iliyotekea kwa kuwa binadamu wanatofautiana kimtazamo, lakini akasisitiza kuwa anachojali zaidi ni dhamana aliyonayo kwa umma.

  "Kama nilivyosema kuwa nimedokezwa kidogo tu, lakini naomba muelewe kuwa huwezi ukamridhisha kila mtu kwani binadamu wamegawanyika katika sehemu tatu," alisema.

  "Asilimia 15 watakupenda, asilimia 15 nyingine watakuchukia na asilimia 70 iliyobaki watabaki wanaangalia upepo unaelekea wapi hivyo tusubiri kuna maamuzi tutafanya," alisema Rais Kikwete.

  Katika mkutano huo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, waziri wa zamani wa menejimenti ya utumishi wa umma, Matheo Qares alisema iwapo rais atashindwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi kabla ya 2010, CCM haina budi kumtosa na kumteua mgombea mwingine wa urais.

  Naye waziri wa zamani kwenye serikali ya awamu ya pili, Mussa Nkangaa alisema CCM sasa imetekwa na wafanyabiashara matajiri na kuachana na sera zake za kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, ndio maana imekuwa vigumu kushughulikia mafisadi.

  Katibu mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula, katika mahojiano na Mwananchi, alisema tatizo la kupeana uongozi kwa urafiki limefanya taifa liwe na viongozi wasio na sifa na kusababisha mambo yanayoendelea kutokea sasa ndani ya chama hicho kikongwe.

  CCM inaonekana kuwa katika hatari ya kuparaganyika kutokana na kuwa na makundi ambayo yanarushiana tuhuma kila kukicha. Tuhuma hizo zimekuwa zikitolewa kwenye mikutano ya Bunge na hivi karibuni zilihamia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu na baadaye mkutano wa kamati iliyoundwa kuchunguza mfarakano huo, maarufu kama Kamati ya Mwinyi na wabunge kilichofanyika Dodoma.

  Kikwete, ambaye pia amekuwa akishutumiwa kwa kufanya safari nyingi za nje zinazokula fedha za walipa kodi na huku akishindwa kutulia nyumbani kutatua matatizo mengi yanayoikabili nchi kwa sasa, alitetea safari hizo akisema ni vigumu kwake kuacha safari hizo kwa kuwa hazina mbadala.

  Na kuonyesha kuwa hawezi kuziacha, Kikwete akaongeza:"Na wiki chache zijazo ninatarajia kwenda nchini Denmark kuhudhuria mkutano wa Capenhagen."

  Ikulu pia iliwahi kutoa taarifa ya kutetea ziara hizo ikisema kuwa zina manufaa kwa nchi kwa kuwa Rais Kikwete huenda nje kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo. Ikulu ilitoa kauli hiyo baada ya wananchi kulalamika kuwa fedha nyingi hutumika kwenye safari hizo.

  Kikwete anatarajia kuongoza msafara wa watu takribani 60 atakapokwenda Copenhagen kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

  Kuhusu hali ya afya yake, Kikwete, ambaye alizidiwa nguvu jukwaani mjini Mwanza kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kufanya safari ndefu bila ya kupumzika, alisema yuko salama lakini anatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya.

  "Nilipokuwa huko nilipima afya yangu na hasa akili na mishipa ya damu na wataalamu wakaniambia nipo salama. Ninatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya," alisema Kikwete. Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa hali yake ni salama wataalamu wamemshauri kupunguza ratiba za kazi za kila siku.
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Labda mimi sikuelewa kiswahili.

  Rais JK kasema ktk jamii ndivyo ilivyo 15% watakupenda,15%watakuchukia hata ufanye nini, 70% wao wataangalia upepo unavuma vipi.
  Hayo ndo kasema Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania .
   
 14. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  sizani kama anaweza kuwa na jipya zaidi ya kusema aliyoyasema. Lakini ukweli haupingiki na utaendelea kusimama. mimi ninavyojua mtu unaweza kukanusha lakini zamila inakusuta. TUNATAKA MAISHA BORA ALOTUAHIDI ILI NA SISI TUKABEMBEE JAMAICA.
   
 15. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hakuna mapigo yoyote hapo, akitaka kujibu mapigo atupatie maisha bora alituahidi na sisi tukabembee jamaica bwana. Lakini kama anaendelee kuwalea mafisadi hata akijibu mapigo yatakuwa hayama maana yoyote
   
 16. K

  Kadudu Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  issue hapa ni makundi au ufisadi?so kuna makundi ndo maana anajua hao waliosema wanatoka kundi gani?
   
 17. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Mbona kwa mafisadi hajibu mapigo? na yapi mema aliyoyafanya,mbona hatuyaoni jamani eh
   
 18. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nadharia ya Jakaya Kikwete
   
  Tulisema urais una ubia huu! Tutafanya na nani wakati wewe ndio rais?

  Chuki binafsi? Give me a break Wananchi wenye nchi wakupe madaraka then baada ya miaka 4 waanze kuwa na chuki binafsi? Kisa ati unajenga hekalu Bwagamoyo au bandari sijui nini tena airport.

  Kuua kwa kukusudia wachimbaji wa madini wadogo wadogo wa Buzwagi na Bulyankulu etc. Kuchekelea wakati pesa za EPA zinavyotafunwa na rafiki zako, Kuuza Loliondo, kuuza urithi wa walipa kodi kwa bei ya peremende - TRL, shirika la simu kuwapa bure Canadians, kumfurahia mkoloni RA anavyokomba pesa kupitia Dowans na Saga la Richimonduli. We Jakaya we tunayaona yote haya. Ulizia yaliyompata Moussa Dadis Camara. Tumefika ile point wanaita Point of no return, Nyerere alisema ukigeuka nyuma unakuwa jiwe, Je, Jakaya unataka kugeuka jiwe?
   
 19. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 3,995
  Trophy Points: 280
  Halohalo!!! JK umekuwa mtu wa mipasho sasa!? kaa mkao wa kula nyumba inaungua! Kuwadi mwenzio RA anaamisha hazina yake nje sasa!
   
 20. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Inaelekea Nyerere Foundation wamenena ya kweli ndio maana JK anashuka Dar na kuanza kuwayawaya.

  Ngoja tusubiri tuone anavyojibu hayo mapigo bila ya kufanya maamuzi magumu.

  This guy has to go maana ni wazi kazi imeshamshinda.

  Nchi haina umeme tokea aingie madarakani lakini kila kukicha yuko anabembea kutoka nchi moja hadi nyingine.

  Uraisi sio pasiport ya kuwa mtalii kwa pesa ya umma. Atuambie tu ni lini atakaa chini na kufanya kazi za Taifa??
   
Loading...