Kikwete tumia helcopta kwenda Chalinze kutupunguzia adha za msongamano kila mara! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete tumia helcopta kwenda Chalinze kutupunguzia adha za msongamano kila mara!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiroroma, Apr 18, 2009.

 1. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Inakera,inasumbua,tena inaudhi sana pale Rais Kikwete anapoenda kwao Chalinze mara kwa mara siku za mwisho wa juma kama leo asubuhi kwa msafara mkubwa wa magari,Acha kuwa ni gharama kubwa kwa Taifa ,muda ,na ujumbe anaoenda nao lipo hili jambo la kutusumbua sana sisi watumiaji wa barabara ya Morogoro.Kwanza ,magari yale yanaenda kwa kasi kubwa hatari hata kwa waenda kwa miguu.Pili,Traffic jams,magari kuwekwa pembeni na wakati mwingine watoto wadogo wanaokatiza barabara.Huu ni usumbufu usiohitajika kusababishwa na kiongozi wa juu kama Kikwete ,kwani ni gharama nafuu kuchukua helkopta ya jeshi au hata polisi kwenda mahali kama Chalinze.Sina maana ya gharama kifedha tuu bali hata usumbufu anaowapa watu wengine kama wananchi waishio kando kando mwa barabara ,askari polisi ,askari wa usalama barabarani,UWT nk nk.Si jambo geni kwa rais kutumia helkopta hata kule Marekani hutumika kumbeba rais badala ya kusumbua wananchi
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo Umenena; ni kweli usumbufu ule ungeepukwa na usalama ungekuwa mkubwa mno kama wanavyodhani; kimsingi Watanzania hatujafikia hatua ya kumuwinda rais (ukiacha pale Mbeya alipopolewa kwa mawe kwa kushindwa kutekeleza ahadi); usumbufu wa traffic kujipanga toka Dar hadi chalinze wakizuia magari pikipiki, baiskeli na waenda kwa mguu; ni costful na usmbufu wa kupoteza muda wenye toja kwa wananchi maana ukimpotezea muda mtu dk 5 is alot (labda kama WATZ hatujali muda kabisa), pia kuna swala la wapita njia wasio na hili wala lile; Kuwa karibu na nyumbani ukiwa rais haina maana basi kila siku unaenda nyumbani; unless kama inafikia wakati hatuna mtu anayeweza kuconcentrate na hivyo kufuanya kazi kwa protocol na bora liende; kweli kwa haya maelezo maanake hata mkuu hayuko conscious na watu wake; this is not the kind of president we voted by 80%
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. sii watu kule wakiona msaafara wa magari mengi ndo watamwona 'ameutaka'?

  Ha ha ha!

  2. Hata Airpot to Ikulu viongozi wangetumia tu Helkopta..haina haja ya misururu ya magari!!
   
 4. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nadhani afanye tu kama wakina Bush na Obama wafanyavyo ili kuepusha kuwakwaza wananchi maana sasahivi wana Hasira kinoma na maisha hivyo dk 1 ukiwapotezea wanaona ni siku nzima.
  Lakini washauri wake ndio walipaswa kufanya hilo au labda wapambe wanashinikiza ili tuwaone kwenye msafara wa muungwana lakini hatuwaoni wanapita kasi bora atumie hiyo Elcopta ajipitie juu.
   
 5. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mswahili kwenye mawingu mtajuaje kama ni yeye...anataka ashine..lol.. Kwanza hizo helikopta zinazoanguka daily ndio mnataka kumpandisha head of state.. Ajali za Helikopta hazinaga majeruhi.. wote kushne!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa helikopta hizi zinazobeba mikungu ya ndizi ,unalinganisha na Helikopta ya Raisi ya Marekani ,jamani tafuteni vitu vya kufananisha.Ila kwa hizi helikopta zetu naona bado hazijawa na security ya kumubeba kiongozi Mkuu wa Nchi.
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  kikwete fisadi fulani ukiona hayo magorofa aliyojenga pale kwao lugoda..utasema kweli mwalimu fufuka uone..,hapo bado bagamoyo anajenga kasiri...na pale ursino street....linajengwa kwa kasi....achilia mbali nyumba aliyopewa oysterbay na vigogo ili aondokane na lile wazo alilokuwa nao la kuwanyanganya nyumba ...amempa rizwani anakaa pale....

  hujaongelea hoteli ...VIP lounges anazojenga mbugani....

  kikwete fisadi//
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Fungu la kununua helkopta hutolea la kutosha kununua helkopta madhubuti Duniani.
  Wakati wa ununuzi wananunua helkopta nyanya ili mshiko unaobaki wakajenge kuta,kufanya ufuksa na vibinti au kuoa wake wengi kwa mpigo.

  Hawawezi kufanya uzinzi kwa fedha ya kununulia Usafiri wa anga kisha chombo hicho kikaelea kwa usalama.

  Kam walivyozinunua na wazisafirie, kwani walitununulia sisi wabeba mabox???
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  helikopta zipo ila angekuwa aanapanda tungekuwa tunaongea mengine ...kwani kati ya helicopter nne kati ya sita zilizoagizwa [nne tu ndio zimefika,helicopter mbili zilizobaki wanangoja wadanganyika msahau ili wazipige bao wafanyie uchaguzi mwakani]

  sasa kati ya helicopter 4 zilizofika 2..zimeshaanguka ndani ya mwaka mmoja...zimebaki 2 zipo grounded for technical reason ....kila pilot anaogopa kuitumia....nchi nzima tunategemea helicopter ya polisi moja iliyobaki kati ya helicopters alizoacha nyerere[zilikuwa nne...za polizi..kuna ile ya kiooo full..ilikuwa nzuri sana ,na nyingine mbili jumla tatu zipo grounded pale police airwing]

  JW walikuwa na helicopters ziliharibikia vitani....kabla ya kuja kuagiza nyingine 6 mwaka 2004....kati ya hizo zimeletwa 4 tu hadi leo na wamebambikiwa......labda kama watengezezaji watakubali kuwa responsible...wabunge wetu kimiya na waandishi!
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi hizo VFP lounges ni mali yake? Kuna mtu aliniambia pale Mugumu kuwa alikatisha safari kwenda kuserebuka kwenye hoteli ya Tudor kumbe naye ana mshiko?
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  habari ndio hiyoo mzee ..you wont get this anywhere ..than JF......wapenzi wake watarusha taulo soon watataka tulete ushahidi wa hati miliki...wakati ule waliombaga ushahidi wa majumba yake ya chalize ..mjj akatupa link ya google earth wakaakaa kimya....

  kwa hili la VIP LODGES ....I GET THE TIP FROM A VERY RELIABLE WITHHELD PERSON!!!!..hutaamini mzee...

  anyway...bora ingekuwa hivo halafu maendeleo tunayaona ....serikali ya awamu hiii perfomance ipo chini wamekalia kunufaika wao tu....wanasahau usemi ..UKILA NA KIPOFU USIMSHIKE MKONO....SASA SISI WADANGANYIKA NI VIPOFU ....TUNASHIKWA HADI MIKONO ..KWA AHADI ZA UWONGO!!
   
 12. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mungu awape moyo wa huruma, wanapokula bila kunawa wakumbuke pia wale wanaolala njaa na kufa kwa kukosa panadol kule vijijini
   
 13. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  I love jf.
   
 14. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  binafsi naunga mkono kwamba huu ni usumbufu kwa wananchi na pia inaweza kusababisha madhara kama ajali nk....lakini pia napingana na aliyesema kwamba tz haijafikia hatua ya kumlinda rais kiasi hicho, wazo ni hili: usalama wa rais YOYOTE ( and i mean YOYOTE YULE) should not be compromised at all ! hata kama ikiwa ni rais wa kisiwa chenye watu 200, lakini suala la usalama ni LAZIMA tena all the time. Sasa sina uhakika ni magari mangapi yapo ktk huo msafara wa kikwete lakini ni kweli usiopingika kwamba huyu MKWALE anakera kwa hiyo idadi ya msafara wake bana, its about time apunguze hayo magari ili kupunguza gharama "zetu sisi" pamoja na usumbufu !
   
 15. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Maudhi yapo! lakini raisi angenunua helikopa ili awe anaenda chalinze kungengalika hapa?
   
 16. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  unadhani kununua choper ni kama kununua baiskeli ? unadhani hajajifunza na ile "ndege ya rais" ambayo tuliambiwa "tutakula hata nyasi lkn ndege lazima inunuliwe" ? au unamtega mkwale babu ? sometimes, lets be careful with what we wish for ! maana huyu mkwale aka mzee wa mitoko, usije ukashangaa ananunua na chopper 2 extra tukaambiwa ni za msafara nazo ! btw ile ndege ilinunuliwa kiasi gani ? then ikagundulika original price ilikuwa ngapi ? na cost ya kuwa hewani kiasi gani ? huko kwao atakuwa anaenda kila siku, i bet u !
   
 17. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kada,

  Ndio mana nasema, wacha atumie tu hayo magari! maana ingenunua hiyo ingeitwa fisadi wa kutupwa. I guess, i was feeling a bit sorry for him as he is criticized for everything! Dalili mbaya kabisa!
   
 18. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  petu hapa,
  jamaa anadeserve hiyo criticism na kama hakujiandaa kuwa criticised then i guess atafute biashara ya kufanya. huyu jamaa ni mswahili wa ethnicity na tabia pia, na mambo mengi akiulizwa atakwambia "hata sisi tumeikuta hiyo hali ikiwa hivyo" i get so PISSED OFF akisema hivi, yaani hadi najiuliza kwani nini kazi ya rais.
  Kama ww ni kiongozi, unatakiwa uwe na imani na msimamo. iwapo unaamini kununua chopper ni suluhisho la kupunguza foleni/gharama then simamia hilo suala unaloliamini kama kiongozi na kuwa tayari kuwa criticised na kujitetea kwa nini huo uamuzi ni mzuri. Lkn leo hii hawa viongozi wetu (wa kupeana) ukiwapinga hoja, utaambiwa unataka kumng'oa madarakani na ushuzi mwiiiiingi usiokuwa na maana!
   
 19. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Mambo mengine ni kweli yanakera sana, kwanza kutusababishia kuchelewa tunakoenda kwa foleni, pili msafara anaoambatana nao na gharama zake. Issue nyingine ni hii ya kusindikizwa na kupokelewa Airport na makamu wa Rais, Waziri Mkuu,na utitiri wa viongozi wengine hata kama ameondoka kwa masaa mawili. Mkuu wa nchi anahitaji kusindikizwa na kupokelewa,lakini sidhani kama ni busara kwa viongozi wote kujaa airport!!
   
 20. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I hear you!
   
Loading...